Lini tutaamua kuwa na Jeshi la Polisi lenye weledi

Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
3,183
7,645
Kati ya taasisi zinazolitia aibu Taifa letu ni Jeshi la Polisi. Jeshi hili limekosa weledi wa kutambua wajibu wake mkuu.

Genge la Majambazi
Kuna wakati Jeshi hili limethibitika kuwabambikizia watu kesi. Hili limewahi kusemwa hata na Marais wa awamu mbalimbali. Jeshi hili limewahi kuua watuhumiwa wakiwa mikononi mwao. Na hili limekemewa hata na Rais Samia. Jeshi hili limewahi kuwanyang'anya pesa wafanyabiashara wa madini na kisha kuwaua.

Matukio ya uovu mkubwa kiasi hiki hufanywa tu magenge ya ujambazi. Polisi wanaacha wajibu wao wa msingi wa kuwalinda wananchi dhidi ujambazi, kwa wao wenyewe kugeuka kuwa majambazi na wauaji. Kinachosikitisha zaidi, ni viongozi wao kuwatetea wakati wote.

Kundi la Wala Rushwa
Katika tafiti za kila mwaka za kutambua taasisi zinazoongoza kwa rushwa, nyakati zote, Jeshi la Polisi huwa ndiyo taasisi inayoongoza kwa rushwa.

Nguvu Bila Maarifa
Matendo mengi ya Polisi huashiria matumizi makubwa ya nguvu bila akili. Mahali panapohitaji kutumia akili hata kwa kiasi kidogo, ndipo utagundua uwezo mdogp wa Jeshi la Polisi. Ushahidi wa yule RPC ni mfano hai. Fikiria kuwa yule ni RPC. Hao polisi wa kawaida wapoje?
 
Nasubiri waanze zamu zaokuzungukia madrasa na sunday school zote nchini sio dar pekee kote hadi kwimba kigoma uvinza katavi etc
 
Kutokujua kusoma na kuandika sio tatizo, jambo kubwa hawafuati sheria zao ,hapo tu mbona kama wanafuata sheria walizojiwekea au zilizowekwa wala wasingekuwa na shida na wangeheshimika tu,leo imefika polisi wakinyukana wenyewe kwa wenyewe wananchi wanashangiria,polisi akigongwa wananchi wanashngiria,polisi wakitiwa mbaroni bado wananchi wanaona ni sawa iliyopitiliza,yaani lolote linalowakuta polisi ,mwananchi anaonekana kufurahia japo korohoroho au ndani ndani,..

Inatakiwa wakuu wa jeshi hili wajitathmini kwa nini yote haya yanatokea myaani hata Mkuu wa jeshi hilo akistaafu bado atarushiwa madongo,kunani ???
 
Kati ya taasisi zinazolitia aibu Taifa letu ni Jeshi la Polisi. Jeshi hili limekosa weledi wa kutambua wajibu wake mkuu.

Genge la Majambazi
Kuna wakati Jeshi hili limethibitika kuwabambikizia watu kesi. Hili limewahi kusemwa hata na Marais wa awamu mbalimbali. Jeshi hili limewahi kuua watuhumiwa wakiwa mikononi mwao. Na hili limekemewa hata na Rais Samia. Jeshi hili limewahi kuwanyang'anya pesa wafanyabiashara wa madini na kisha kuwaua.

Matukio ya uovu mkubwa kiasi hiki hufanywa tu magenge ya ujambazi. Polisi wanaancha wajibu wao wa kuwalinda wananchi dhidi ujambazi kwa wao wenyewe kugeuka kuwa majambaji na wauaji. Kinachosikitisha zaidi, ni viongozi wao kuwatetea wakari wote.

Kundi la Wala Rushwa
Katika tafiti za kila mwaka za kutambua taasisi zinazoongoza kwa rushwa, nyakati zote, Jeshi la Polisi huwa ndiyo taasisi inayoongoza kwa rushwa.

Nguvu Bila Maarifa
Matendo mengi ya Polisi huashiria matumizi makubwa ya nguvu bila akili. Mahali panapohitaji kutumia akili hata kwa kiasi kidogo, ndipo utagundua uwezo mdogp wa Jeshibla Polisi. Ushahidi wa yule RPC ni mfano hai. Fikiria kuwa yule ni RPC. Hao polisi wa kawaida wapoje?
Ni baada tu ya kubadilisha katiba na kuondokana na ccm.
 
siku mtakapopata wapinzani wenye nia kweli ya mabadiliko na si wafanyabiashara,amini nakwambia kila kitu kita switch kunakotakiwa.
 
Kwanza naumia wanapo waita jeshi la polisi, jeshi bila nidhamu nisawa na mwendawazimu kuoa.
 
Kati ya taasisi zinazolitia aibu Taifa letu ni Jeshi la Polisi. Jeshi hili limekosa weledi wa kutambua wajibu wake mkuu.

Genge la Majambazi
Kuna wakati Jeshi hili limethibitika kuwabambikizia watu kesi. Hili limewahi kusemwa hata na Marais wa awamu mbalimbali. Jeshi hili limewahi kuua watuhumiwa wakiwa mikononi mwao. Na hili limekemewa hata na Rais Samia. Jeshi hili limewahi kuwanyang'anya pesa wafanyabiashara wa madini na kisha kuwaua.

Matukio ya uovu mkubwa kiasi hiki hufanywa tu magenge ya ujambazi. Polisi wanaacha wajibu wao wa msingi wa kuwalinda wananchi dhidi ujambazi, kwa wao wenyewe kugeuka kuwa majambazi na wauaji. Kinachosikitisha zaidi, ni viongozi wao kuwatetea wakati wote.

Kundi la Wala Rushwa
Katika tafiti za kila mwaka za kutambua taasisi zinazoongoza kwa rushwa, nyakati zote, Jeshi la Polisi huwa ndiyo taasisi inayoongoza kwa rushwa.

Nguvu Bila Maarifa
Matendo mengi ya Polisi huashiria matumizi makubwa ya nguvu bila akili. Mahali panapohitaji kutumia akili hata kwa kiasi kidogo, ndipo utagundua uwezo mdogp wa Jeshi la Polisi. Ushahidi wa yule RPC ni mfano hai. Fikiria kuwa yule ni RPC. Hao polisi wa kawaida wapoje?
Jeshi la mkoloni tangu lini likawa na akili.

Ukiona taasisi inabeba watu waliofeli shule ujue hao watu wanaenda kutumika na watawala kwa maslahi yao binafsi.
 
Back
Top Bottom