Lini Serikali hii sikivu itakamilisha ulipaji wa malimbikizo kwa wafanyakazi?

TEMILUGODA

JF-Expert Member
Feb 11, 2012
1,374
1,500
Tangu awamu ya sita ilipo ingia madarakani wafanyakazi tulishuhudia baadhi yao wakianza kulipwa malimbikizo yao ya muda mrefu Sana,lakini baada ya muda mfupi tena Ni kama zoezi hili limekwama tena

Mimi kama mfanyakazi naomba serikali ilipe malimbikizo ya wafanyakazi Hawa kwa sababu Kuna kukatisha tamaa na kukosa utulivu kwa wafanyakazi Hawa.

Pamoja na kudai malimbikizo hayo,watumishi kwa wingi wao wamepandishwa madaraka ya kazi kwa wingi tangu 2015 kwa mara ya Mwisho japo Kuna kundi ambalo lime kosa kupandishwa kwa makosa ambayo yalijitokeza kwa kuchelewesha kuwapandisha na kuleta mkanganyiko na hatimaye kupandishwa kimakosa mwaka 2018 na kujikkuta mwaka huu wanaachwa na kupitwa walio watangulia kwenye ajira.

Yote kwa yote Malimbikizo yalipwe tu ili kuboresha maisha ya wafanyakazi.
 

Retina

JF-Expert Member
Mar 6, 2015
876
1,000
Wafanyakaz wa umma kazi wanayo!Upandishaj wa madaraja mpaka uhonge ndio unapandishwa ukizubaa utajikuta umeachwa mshahara na mtu aliyeajiriwa miaka minne baadaye.Likizo unaenda baada yw miaka minne unalipwa huu ni upuuz.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom