Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,192
- 25,493
Leo nimeikumbuka Ripoti ya Timu Maalum ya Kukagua na Kuhakiki Mali za CCM ya mwaka jana. Timu hiyo iliongozwa na Katibu Mkuu wa sasa wa CCM, Dkt. Bashiru Ally Kakurwa. Ripoti hiyo ilikabidhiwa kwa Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dr. J.P.J.Magufuli.
Rejea hapa:https://www.ippmedia.com/sw/habari/ripoti-ya-mali-za-ccm-mikononi-mwa-magufuli. Kuanzia kukabidhiwa kwa Ripoti hiyo (inayotajwa kuwa na ufisadi wa kutisha; Ripoti ambayo Musiba amedai anayo), kumekuwa na kimya kirefu. Kwangu mimi, ufisadi na wizi hauna mahali pa kufanyika. Ufisadi na wizi uliofanyika ndani ya CCM hauna tofauti na ufisadi na wizi sehemu yoyote nyingineyo.
CCM, hadi sasa, imewaburuza mahakamani wahusika wangapi wa ufisadi na wizi huo? Wangapi wamechukuliwa hatua za kinidhamu kichama kutokana na Ripoti hiyo? Kwakuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa, Mhe. Rais Magufuli anaongoza vita dhidi ya ufisadi na wizi kwenye Serikali yake, utekelezwaji wa mapendekezo ya Ripoti hiyo ya mali za CCM ingekuwa ni fursa muhimu kwa CCM kumuunga mkono Rais Magufuli kwa vitendo.
Hayatuhusu lakini ni ya muhimu!