Lini bajeti yetu itakuwa mkombozi wa mnyonge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lini bajeti yetu itakuwa mkombozi wa mnyonge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sammosses, Jun 15, 2012.

 1. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #1
  Jun 15, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Serikali kupitia wizara yake ya fedha hutangaza bajeti ya makisio ya mapato na matumizi kila mwaka wa fedha wa serikali.Hotuba hiyo ya bajeti huenda sambamba na mabadiliko bei ya bidhaa muhimu zinazo tegemewa sana katika maisha ya binadamu.Hali hii husababisha tabaka la wanyonge kuishi maisha magumu yanayo sababishwa na mfumuko wa bei.Imekuwa ni hali ya kawaida sasa kwa serikali yetu ya awamu ya nne kushindwa kudhibiti mfumuko wa bei tangu kuingia kwake madarakani.

  Ukiangali kodi inayokatwa kwenye mishahara imeongezeka(PAYE),hali ambayo inazidi kumgandamiza mfanyakazi huyu,ilihali kulikuwa na malalamiko kutokana na kodi iliyokuwa inakatwa kabla ya bajeti kutangazwa ambayo ilionekana ni kubwa inayo msababishia mfanyakazi kupambana na hali ngumu ya maisha.Kodi ya PAYE imeongezeka lakini mishahara imebaki pale pale,wapi nchi inawapeleka wananchi wake.

  Kodi ya vinywaji ambavyo wanyonge watendelea kuona kama ni anasa na kuwatenga kimatabaka kwa kushidwa hata kuweza kuhimili kununua soda ambayo ndiyo ilikuwa kimbilio lao.Mkulima naye anazidi kuachwa mbali huku kauli mbiu iliyonadiwa kwenye ilani ya uchaguzi ya 2010-2015 ikizidiwa kunadiwa kinadharia zaidi kuliko implementation yake.

  Kwa mantiki hiyo basi kutokana na serikali kujikita zaidi kulipa madeni kwa asilimia 70% na shughuli za maendeleo kutengewa asilimia 30%,ni lini basi mnyonge huyo atakuja kukumbukwa na serikali yake iliyo sikivu katika kumsikiliza mwananchi huyu kwa kutenga bajeti itakayoleta unafuu wa maisha.


  Mambo ni mengi sana yanayo tia kichefu chefu kutokana na mnyonge huyu kusahaulika.Tukijaribu kuangalia mkulima wa kawaida huyu ndiyo amesahaulika kabisa ndani ya nchi hii,huwezi kuamini mpaka leo serikali kupitia bodi yake ya pamba imeshindwa kutangaza bei ya pamba kutokana na kulumbana na wanunuzi,hali ambayo inazidi si kumchosha tu mkulima bali na kumkatisha tamaa ya kuliendeleza zao hili.Hatuoni juhudi za makusudi kwa serikali yetu katika kumkomboa huyu mkulima.Serikali iliwahi kutoa ahadi ya kutoa ruzuku kwa mkulima miaka miwili imepita serikali imeshindwa kuwafidishia wafanya biashara walioambiwa waongeze bei na serikali itafidia ongezeko hilo.

  Hali hii itakwenda mpaka lini ilihali matumizi mabaya ya pesa za serikali yanazidi kuongezeka japokuwa waziri wa fedha amesema yamepungua,wakati sisi wananchi ndiyo tuona kwa macho yetu na haitaji kuambiwa wakati tuna mboni za macho.Mimi nimeona machache lakini yapo mengi ambayo naamini wana JF wataungana nami katika kuyasemea ili kumnusuru mnyonge huyu aliyekosa msemaji ,mara baada ya wawakilishi wao kuwatupa na kuwasahau.Ubunge ni dhamana waliyopewa na wananchi na dahamana hiyo hukumu yake tunaijua sisi wapiga kura.Inasikitisha mbunge kuwakebehi wapiga kura wake kwa matumizi ya simu za mkononi na kusahau wajibu wake wakuwatetea ili ushuru huu upunguwe kwani mawasiliano si anasa kama navyotaka kutuaminisha.
   
 2. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #2
  Jun 15, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Hadi tutakapotumia vizuri kura zetu na kuchagua watu wenye uchungu na nchi hii
   
 3. charminglady

  charminglady JF-Expert Member

  #3
  Jun 15, 2012
  Joined: Apr 16, 2012
  Messages: 17,858
  Likes Received: 1,132
  Trophy Points: 280
  Mkuu vipi kuhusu kodi ya mapato kama yenyewe haijaongezeka bora nikafanye biashara. tafadhali naomba ufafanuzi!
   
 4. S

  STIDE JF-Expert Member

  #4
  Jun 15, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 999
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Viongozi waliowekewa vifuu vya nazi ndo wanapanga bajeti ya Taifa, unategemea nini!!?

  Acha tukamuliwe hadi akili ikae sawa ili 2015 tuzibue masikio na kufanya maamuzi ya msingi!!!
   
Loading...