Lindi yamzika Sheikh Mpigania Uhuru Sheikh Hassan Mohamed Said Kinyozi

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
18,953
27,100
Kama tusingeandika historia yetu waliokuwa hawapo hiki kizazi kipya kisingeijua historia ya Sheikh Hassan Kinyozi.

Tungemzika Sheikh Hassan Kinyozi kama tunavyowazika masheikh wetu.

Tusingeliweka jeneza la mwalimu wetu mabegani na vifua mbele tukijua kuwa tunamzika shujaa aliyepigania uhuru wa Tanganyika.

Toka jana baada ya kuweka historia ya Sheikh Hassan Mohamed Said Kinyozi mtandaoni wasomaji wanauliza nini kimesababisha sisi kutokuwa na historia ya mashujaa wetu?
 
Attachments

  • IMG-20221116-WA0140.jpg
    IMG-20221116-WA0140.jpg
    105.9 KB · Views: 16

Mocumentary

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
670
1,637
Mzee wetu leta historia, vizazi vijavyo vitajifunza mengi kuhusu wazee wao kupitia wewe.
 
Mnachihangu

JF-Expert Member
Oct 22, 2022
890
971
Mohamed saidi huku kusini wengi sana walishiriki kuupigania huo uhuru kwa namna tofauti tofauti kuanzia vita kama majimaji na babu zangu mimi walipigana hivyo hatari ambavyo walikuwa wanacheza na risasi na japo wengi wao walìshatangulia mbele za haki ila hautakuta sisi wajukuu zao tunaanza kudai majina yaandikwe kwenye vitabu tupo cool kabisa,sembuse hao wadai uhuru wako waliokuwa wanadai huku wanacheza bao na kuuza kahawa sokoni uhuru uliodaiwa kilaini sana
 
Mnachihangu,
Niruhusu nikushauri njia bora ya kufanya mjadala.
Umetoa mawazo mazuri ambayo mimi yamenipa uwanja wa kuchangia.

Tatizo ni lugha uliyotumia imesimama katika kejeli., ''wadai uhuru wako.''
Mimi sina wadai uhuru wangu.

Wapigania uhuru walikuwa wazalendo wa Tanganyika.
Umeandika ''wacheza bao na wauza kahawa.''

Kucheza bao na kuuza kahawa ni mila ya watu wa Pwani.
Ukikejeli unaonyesha dharau.

Ikiwa wewe umekaa kimya kuhusu mashujaa wa Maji Maji huwaadhimishi hakuna wa kukulazimisha uwaheshimu lakini huna haki ya kuwakataza wengine kuwaenzi mashujaa wa Maji Maji mfano wa ''Abdulrauf'' Songea Mbano na ''Khadija'' Mkomanile.

Umepata kusoma katika historia ya Maji Maji majina hayo yakitajwa kikamilifu?
Ushajiuliza kwa nini?

Unajua kuwa katika makumbusho ya Maji Maji Mahenge Songea kuna kaburi la majemadari 67 waliozikwa kwenye kaburi la halaiki na wajemadari wote hao ni Waislam?

Ushajiuliza kwa nini iwe hivyo?

Je, Unajua majemadari hawa kabla ya kunyongwa waliletewa mchungaji kutoka Peramiho jina lake Johann kuja kuwabatiza?

Soma historia ya wazee wako wa kusini walionyanyua silaha kupigani uhuru wao uifahamu.

Hii itakuweka wewe katika hali ya kuweza kufanya mjadala wa maana na kujiweka mbali na kejeli.
 
Awakener

Senior Member
Dec 28, 2018
125
51
Mzee Mohammed samahani kama nitakuwa nimetoka nje ya mada ila ninahitaji kitabu au vitabu vyenye historia ya pwani ya Afrika ya Mashariki kabla ya ukoloni iwe kwa mji mmoja mmoja au yote kwa ujumla.
Mwenyezi Mungu akuzidishie uzidi kutupa maarifa
 
Sijakejeli popote pale labda wewe ndie unataka kujiaminisha hivyo ninaposema wapigania uhuru wako namaanisha ni babu zako ambao wewe ni ndugu zako,tukija hili swala la makamanda waliopigana vita vya majimaji kuwa wote ni waislamu hapo unapotosha wazi kabisa kwasababu kijijini kwetu likokona sisi tulisimuliwa kuwa mzee mandota na ndugu zake wawili walipigana hivyo vita na walinyongwa na huyo mjerumani na hao hawakuwa waislamu na hawajatajwa popote pale je hili nalo lilifichwa? Na unadai kuwa aliletwa padre ili awabatize ili iweje wakishabatizwa?
 
Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
18,953
27,100
Mzee Mohammed samahani kama nitakuwa nimetoka nje ya mada ila ninahitaji kitabu au vitabu vyenye historia ya pwani ya Afrika ya Mashariki kabla ya ukoloni iwe kwa mji mmoja mmoja au yote kwa ujumla.
Mwenyezi Mungu akuzidishie uzidi kutupa maarifa
Awa...
Siwezi kukusaidia kwenye hili.
Jaribu maduka ya vitabu.
 
Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
18,953
27,100
Sijakejeli popote pale labda wewe ndie unataka kujiaminisha hivyo ninaposema wapigania uhuru wako namaanisha ni babu zako ambao wewe ni ndugu zako,tukija hili swala la makamanda waliopigana vita vya majimaji kuwa wote ni waislamu hapo unapotosha wazi kabisa kwasababu kijijini kwetu likokona sisi tulisimuliwa kuwa mzee mandota na ndugu zake wawili walipigana hivyo vita na walinyongwa na huyo mjerumani na hao hawakuwa waislamu na hawajatajwa popote pale je hili nalo lilifichwa? Na unadai kuwa aliletwa padre ili awabatize ili iweje wakishabatizwa?
Mnachihangu,
Inaelekea huijui vizuri historia ya Maji Maji.

Unazungumzia Mzee Mandota na ndugu zake wawili jumla watatu walionyongwa na Wajeruamani.

Mimi nimekupa historia ya majemadari 67 na nimekuwekea na majina yao ambao walinyongwa na kuzikwa katika kaburi moja Mahenge, Songea.

Hilo jina mji ''Songea'' linatoka kwa Abdulrauf Songea Mbano.
Yeye kazikwa kaburi la peke yake pembeni kwa kaburi hilo la halaiki.

Sasa angalia uwiano wa watu watatu na majemadari 67 walionyongwa na Wajerumani.

Hawa kwa khiyana na kutaka kufuta historia Wamishionari walikwenda Songea kuwabatiza ili kufuta Uislam wao.

Watu 3 huwezi kulinganisha na watu 67.

Nakuongeza kitu kiingine angalia picha hizo hapo chini minara ya kumbukumbu ya wazalendo walikonyongwa na angalia wametoka sehemu zipi:

1668684025078.jpeg

Mnara wa Kumbukumbu ya Maji Maji Songea
1668684079558.png

Majina katika mnara kwa Kumbukumbu ya Maji Maji Kilwa katika majina hayo Hassan Omar Makunganya peke yake ndiye ambae hakunyongwa kwa sababu ya vita.

1668684336255.jpeg

Abdulrauf Songea Mbano
 
umucyo

JF-Expert Member
Aug 12, 2020
849
697
Mohamed saidi huku kusini wengi sana walishiriki kuupigania huo uhuru kwa namna tofauti tofauti kuanzia vita kama majimaji na babu zangu mimi walipigana hivyo hatari ambavyo walikuwa wanacheza na risasi na japo wengi wao walìshatangulia mbele za haki ila hautakuta sisi wajukuu zao tunaanza kudai majina yaandikwe kwenye vitabu tupo cool kabisa,sembuse hao wadai uhuru wako waliokuwa wanadai huku wanacheza bao na kuuza kahawa sokoni uhuru uliodaiwa kilaini sana
Haya nayo ni maajabu ya Dunia. Kwakua nyinyi wajukuu waflani mmeamua kukaa kimya nababu zenu hawatajwi kwenye vitabu nawengine hawana haki ya kuandika? kukaa kwako kimya ,kusiwe sababu ya kuwafunga wengine midomo.

Kama hamjawapa thamani wanayo stahil acha wegine waandike Yale walio pitia wapendwa wao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mnachihangu

JF-Expert Member
Oct 22, 2022
890
971
Mnachihangu,
Inaelekea huijui vizuri historia ya Maji Maji.

Unazungumzia Mzee Mandota na ndugu zake wawili jumla watatu walionyongwa na Wajeruamani.

Mimi nimekupa historia ya majemadari 67 na nimekuwekea na majina yao ambao walinyongwa na kuzikwa katika kaburi moja Mahenge, Songea.

Hilo jina mji ''Songea'' linatoka kwa Abdulrauf Songea Mbano.
Yeye kazikwa kaburi la peke yake pembeni kwa kaburi hilo la halaiki.

Sasa angalia uwiano wa watu watatu na majemadari 67 walionyongwa na Wajerumani.

Hawa kwa khiyana na kutaka kufuta historia Wamishionari walikwenda Songea kuwabatiza ili kufuta Uislam wao.

Watu 3 huwezi kulinganisha na watu 67.

Nakuongeza kitu kiingine angalia picha hizo hapo chini minara ya kumbukumbu ya wazalendo walikonyongwa na angalia wametoka sehemu zipi:

View attachment 2419493
Mnara wa Kumbukumbu ya Maji Maji Songea
View attachment 2419494
Majina katika mnara kwa Kumbukumbu ya Maji Maji Kilwa katika majina hayo Hassan Omar Makunganya peke yake ndiye ambae hakunyongwa kwa sababu ya vita.

View attachment 2419496
Abdulrauf Songea Mbano
Bado hoja yako haina mashiko kuufuta uislamu wao kwa watu ambao ni mateka?
 
ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
17,013
35,615
Ooh long time not heard blessings comrade Said, inshallah heri ikawe juu ya shehe wetu. Jiji la maraha la Lindi I miss Lindi ni patamu sana, Uwanja wa Fisi samaki kama wote
Nimekuja lindi kikazi of course kumetulia flan napapenda now nina muda hapa naimani zamani ilikuwa ni bonge la paris kwerikweri
 
wadiz

JF-Expert Member
Nov 10, 2022
2,478
4,359

Hakika it was for east Africa, sehemu ya starehe imetengwa kabisa na wana kanuni zao, hata mademu hupatikananga hizo sehemu inakuwanga poa sana
 
ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
17,013
35,615
Hakika it was for east Africa, sehemu ya starehe imetengwa kabisa na wana kanuni zao, hata mademu hupatikananga hizo sehemu inakuwanga poa sana
Of course yes kuanzia santorin mpk makuti bay kwa brother ray sijui unamjua alifariki...njoo mpk chamikumbi
 
wadiz

JF-Expert Member
Nov 10, 2022
2,478
4,359
Of course yes kuanzia santorin mpk makuti bay kwa brother ray sijui unamjua alifariki...njoo mpk chamikumbi
I will be there soon bro, nikija nakula kwenye mgahawa wenu maarufu jirani na hizo bar karibu na shirton Lodge. Nina eneo juu kule mbele ya central police 1/2 eka
 
Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
18,953
27,100
Nani amekuambia sikuwa nayajua?na ni nani kakuambia nina shida ya kuyajua?
Mnachihangu,
Ulikuwa unajua kuwa kadi ya TANU No. 2 ilikuwa ya Ally Sykes na ya kaka yake Abdul No. 3?

Dossa Aziz kadi yake no. 4.

Ulikuwa unajua kuwa kadi No. 5 ilikuwa ya Denis Phombeah Mnyasa kutoka Nyasaland?

Kadi No. 6 Dome Okochi Budohi Mluya kutok Kenya.

Ulikuwa unajua kuwa kadi ya TANU no. 1 ilikuwa ya Territorial President, Julius Kambarage Nyerere na aliandikiwa na Ally Sykes?

Hakuna mtu aliyekuwa anajua hadi mimi nilipoeleza katika kitabu cha Abdul Sykes.

Mimi siko hapo kubishana au kufanya mzaha.

Kwa nini unajibu fedhuli.
kwa lipi?

Lipi baya ndugu yangu ambalo mimi nimelisema kukughadhibisha?

Au umekasirika kwa kusoma historia ya wazee wangu?

Historia ambayo kwa miaka mingi haikuwapo?
 
Marashi

JF-Expert Member
Apr 14, 2018
2,744
4,115
Hata wazazi wangu walikuwepo kipindi cha harakati za uhuru lakini baada ya hapo wakaendelea na maisha mengine bila kujipendekeza.
Anachotaka kutudanganya Mzee Said ni kusema uhuru wa Taifa letu ulipiganiwa na viongozi

Hakuna raifa ambalo uhuru unapiganiwa na viongozi, ni wananchi wenyewe!
 
3 Reactions
Reply
Top Bottom