Lindi: Watumia mafuta ya Mil 7 kwa siku 4 na kununua pikipiki 2 kwa mil 11

May 4, 2020
32
37
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi Hashim Komba ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU wilayani humo kufanya uchunguzi wa matumizi mabaya ya fedha kiasi cha shilingi milioni 18 zilizotumika kwenye mradi wa Usafi na Mazingira (WASH) wilayani humo ambapo ni Ununuzi wa pikipiki 2 kwa shilingi milioni 11 na Ununuzi wa Mafuta ya Milioni 7 yaliyotumika ndani ya siku 4

Komba ametoa agizo hilo baada ya ziara yake katika Zahanati ya Mkotokuyana, Ikungu, Tunduru ya Leo na hospitali ya wilaya ya Nachingwea ambapo pia amewataka watumishi wote waliochukua fedha kwa ajili ya kufuatilia utekelezaji wa mradi huo kuzirejesha mara moja sababu ikiwa ni kutoifanya kazi na kupelekea mradi kutokamilika kwa wakati.

65d70f62-aa91-4a30-9fb0-1ca669d02701.jpg
 
Waongezeni mishahara..mana hawafanyi hivyo bure wanajua na wakubwa wao wanapiga na wenyewe wameona wapige tu..kwa mshahara gani wanao pata wasipige nao wanafamilia za kuhudumia...TAkukuru wafanye kazi zao ili na wao ni wapigaji pia..kesi kama hizi ni dili kwao..

Cha mwishoni Mitano tena.

#MaendeleoHayanaChama

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Kuna watu masteringi kweli kweli..
pamona na mikwara ya awamu ya 5 bado kuna mtu anapiga parefu,

Hapo kwenye pikipiki 2 kwa milioni 11 sitaki kubisha saana, hali ya kuwa sijajua aina ya pikipiki zilizonunuliwa kama ni hivi vi haojue, boxer, tvs, sijui fekon na wenzie kifupi chini ya cc 200, haiwezekani ikafika huko.

Kichekesho zaidi ni kusikia watu wamenunua mafuta ya pikipiki ya milion 7 kwa matumizi ya siku 4
 
CCM yajenga nchi!!. CCM HOyeeeeeeeeeeeeeeeeee!. Haya ndiyo yalikuwa yanatafutwa katika utashi wa kufuta upinzani.
 
Waongezeni mishahara..mana hawafanyi hivyo bure wanajua na wakubwa wao wanapiga na wenyewe wameona wapige tu..kwa mshahara gani wanao pata wasipige nao wanafamilia za kuhudumia...TAkukuru wafanye kazi zao ili na wao ni wapigaji pia..kesi kama hizi ni dili kwao..

Cha mwishoni Mitano tena.

#MaendeleoHayanaChama

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Unaiba harafu unasingizia mshahara, kama nawewe ni kambale kama wakubwa wengine subiri kuoshewa kama hivi.
 
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi Hashim Komba ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU wilayani humo kufanya uchunguzi wa matumizi mabaya ya fedha kiasi cha shilingi milioni 18 zilizotumika kwenye mradi wa Usafi na Mazingira (WASH) wilayani humo ambapo ni Ununuzi wa pikipiki 2 kwa shilingi milioni 11 na Ununuzi wa Mafuta ya Milioni 7 yaliyotumika ndani ya siku 4

Komba ametoa agizo hilo baada ya ziara yake katika Zahanati ya Mkotokuyana, Ikungu, Tunduru ya Leo na hospitali ya wilaya ya Nachingwea ambapo pia amewataka watumishi wote waliochukua fedha kwa ajili ya kufuatilia utekelezaji wa mradi huo kuzirejesha mara moja sababu ikiwa ni kutoifanya kazi na kupelekea mradi kutokamilika kwa wakati
View attachment 1703477
🤣🤣🤣Kumbe watu bado wana ujasiri wa kumega cake ya Magu
 
Unaiba harafu unasingizia mshahara, kama nawewe ni kambale kama wakubwa wengine subiri kuoshewa kama hivi.
Matatizo tunayatengeneza sisi..ajiri mfanyakazi mpe access ya kushika mauzo ya zaidi ya milioni kwa siku halafu mlipe mshahara wa elfu 50 kwa siku..ndipo utajua hujui.

#MaendeleoHayanaChama

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Matatizo tunayatengeneza sisi..ajiri mfanyakazi mpe access ya kushika mauzo ya zaidi ya milioni kwa siku halafu mlipe mshahara wa elfu 50 kwa siku..ndipo utajua hujui.

#MaendeleoHayanaChama

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
unadahani kwa cashier anayeshika milioni hata 500 kwa siku ni halali kumlipa laki 9!!!!

mtu kama mwizi ataiba tu hata umlipeje.
 
Na serikali ichunguzwe kwa kutokuwaongezea mishahara watumishi wa umma kwa miaka zaidi ya 5.
Pia ichunguzwe kwa kutokuwapandishia madaraja watumishi waliostahili madaraja.
Yaani mnataka msumeno ukate upande mmoja tu?
 
unadahani kwa cashier anayeshika milioni hata 500 kwa siku ni halali kumlipa laki 9!!!!

mtu kama mwizi ataiba tu hata umlipeje.
Sometimes pia mshahara unashawishi mtu kua mwizi ama asiwe mwizi..iwapo kama mshahara wake unakidhi au haukidhi mahitaji.

#MaendeleoHayanaChama

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi Hashim Komba ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU wilayani humo kufanya uchunguzi wa matumizi mabaya ya fedha kiasi cha shilingi milioni 18 zilizotumika kwenye mradi wa Usafi na Mazingira (WASH) wilayani humo ambapo ni Ununuzi wa pikipiki 2 kwa shilingi milioni 11 na Ununuzi wa Mafuta ya Milioni 7 yaliyotumika ndani ya siku 4

Komba ametoa agizo hilo baada ya ziara yake katika Zahanati ya Mkotokuyana, Ikungu, Tunduru ya Leo na hospitali ya wilaya ya Nachingwea ambapo pia amewataka watumishi wote waliochukua fedha kwa ajili ya kufuatilia utekelezaji wa mradi huo kuzirejesha mara moja sababu ikiwa ni kutoifanya kazi na kupelekea mradi kutokamilika kwa wakati
View attachment 1703477
Ni mwendo wa kutapishana tu siku hizi mpaka tunyooke...
 
Back
Top Bottom