Lindi: Watu wasiojulikana wamechoma moto nyumba ya Msimamizi wa Uchaguzi na nyumba ya Mbunge

mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
12,358
2,000
Habari ya lini Hii?

Ni ngumu sana kwa wananchi waliogoma kushiriki maandamano kufanya matukio ya hivi, ila ni rahisi sana kwa wale waliokua wakihamasisha maandamano kutekeleza haya.

Serikali ifanye uchunguzi wahusika washughulikiwe
 
Ciril

JF-Expert Member
Jan 10, 2011
8,562
2,000
Ndio ndugu yangu, unasema na bado! Kwa nini tupe faida tafadhali.

Ndipo tulipo fikishwa na Watawala kila kukikuchwa tuna hubiriwa ubaya wa kuwa na Wapinzani mpaka mwenye Nchi kujiapiza kutopeleka Maendeleo ktk Majimbo ambayo yata waunga Upinzani mkono, msumari wa Moto ukagongwa ktk Uchaguzi Mkuu.Wasio na Dola wakapoteza/wenye Nchi waka dharauliwa baadhi waka uwawa na wengine kubaki na vilema huku wengine wakiwa korokoroni kwa Kesi za kutunga.

Wanaitafutia wapi Haki yao ilhali wanao takiwa kusimamia Sheria wamelala Kitanda kimoja na Chama tawala !?.
 
Ciril

JF-Expert Member
Jan 10, 2011
8,562
2,000
Habari ya lini Hii?

Ni ngumu sana kwa wananchi waliogoma kushiriki maandamano kufanya matukio ya hivi, ila ni rahisi sana kwa wale waliokua wakihamasisha maandamano kutekeleza haya.

Serikali ifanye uchunguzi wahusika washughulikiwe

Una jitahidi sana kuuchora Mshale kuelekea unapo palenga ,Kesi ya Ugaidi mliyo sema mtamfungulia Mh Mbowe imeishia wapi !?..
 
magu2016

JF-Expert Member
Oct 8, 2017
6,225
2,000
Ni ngumu sana kwa wananchi waliogoma kushiriki maandamano kufanya matukio ya hivi, ila ni rahisi sana kwa wale waliokua wakihamasisha maandamano kutekeleza haya.

Serikali ifanye uchunguzi wahusika washughulikiwe
Mkuu hayo ni matukio ya tarehe 29/10/2020 na RC alishayatolea Press Conference na wahusika walishakamatwa. Mleta thread hii analake jambo! Anataka kuhamasisha kitu fulani katika jamii kwa sababu anaonyesha kama haya matukio yametokea hivi sasa wakati yalisharipotiwa hata kwenye vyombo vya habari vya nchini na nje!
 
REALNEGRONEVABROKE

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
3,254
2,000
Mkuu hayo ni matukio ya tarehe 29/10/2020 na RC alishayatolea Press Conference na wahusika walishakamatwa. Mleta thread hii analake jambo! Anataka kuhamasisha kitu fulani katika jamii kwa sababu anaonyesha kama haya matukio yametokea hivi sasa wakati yalisharipotiwa hata kwenye vyombo vya habari vya nchini na nje!
Kwa hiyo?
 
big IQ

JF-Expert Member
Dec 16, 2012
445
1,000
Kumbe hawa watu wasiojulikana wapo upande huo,Basi hata kwa Tundu lissu itakua ni watu hawahawa wasiojulikana
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom