Lindi: Wanachama watano wa CUF wadaiwa kutekwa na watu wenye silaha usiku wa manane

Hivi unafikiri CUF ina madhara gani kisiasa Tanzania mpaka wanachama wake kutekwa?..

Tujaribu kutoliweka kila jambo kwenye mlengo wa kisiasa, ili fikra zetu ziende mbali kidogo..
Unataka liwekwe kwenye mlengo gani? ni wakina nani wenye tabia ya kuteka watu? ni mashekhe, mapadri au wachungaji? na hao watekaji hufanya hivyo kwa manufaa ya nani?

Ukipata jibu sahihi la hayo maswali ukae chini utulie.
 
Msiwe mnakimbilia upotoshaji wa habari muwe wakweli hao watakuwa na makosa yao husika na wamekamatwa kwa jinai.
CUF haina impact yoyote hadi kupelekea kutekwa wafuasi wake.

Usikute ndio baadhi ya watanzania waliokuwa msumbiji na wamechukuliwa na kikosi kazi.
 
Niliona kwenye taarifa ya habari. Nikajisemea moyoni kuwa bado wasijulikana wapoo eeennhhh.
 
Wananchi watano usiku wa saa saba wanachama wa CUF walikuwa wamekusanyika sehemu moja??
 
Sidhani kama hiyo 'threat' yao ina uzito zama hizi, JPM kutokwenda Mtwara na Lindi huku wakati mwingine akijipa mapumziko ya wiki moja huenda ilikuwa sababu ya kiafya tu.
But nikiwaza nguvu iliyotumika kuzuia Lissu kufanya kampeni za lala salama huko Lindi na Mtwara (Ilipangwa mikutano sio chini ya 15) huku JPM hakufika ilihali kuna maeneo alirudi mara mbili ilitia shaka kidogo.

Of course inawezekana sio threat tena lakini ufahamu CCM ni unpopular huko tokea issue za gesi na sasa korosho!! So kuna kura nyingi sana za hasira huko na hyo ndio inakua threat kwa viongozi waliopo hasa waliorudi bila kura za wananchi.
 
But nikiwaza nguvu iliyotumika kuzuia Lissu kufanya kampeni za lala salama huko Lindi na Mtwara (Ilipangwa mikutano sio chini ya 15) huku JPM hakufika ilihali kuna maeneo alirudi mara mbili ilitia shaka kidogo...
Ni kweli Ccm sio unpopular kumbuka hata mikoa ya Kaskazini nako ilitumika nguvu kubwa kuipa Ccm ushindi hivyo huenda nayo pia bado ni threat vile vile kama huko tu japo hakuna tukio hilo lilotokea siku za karibuni, kama hilo tukio ni la kisiasa huenda ni siasa za ndani ya mkoa za uhasama tu.

Lakini bado miaka mingi kuelekea uchaguzi mkuu sidhani kama kuna kitisho Ccm inaweza kupata kipindi hiki kutoka huko mpaka iwatie kashkash hao Cuf.

Kumzuia Lissu kufanya mikutano kipindi kile huko kusini ndio ilikuwa njia pekee ya kupunguza kasi yake.

Hata mgombea wa Ccm alipopumzika kufanya kampeni kwa wiki moja ilibidi Lissu afungiwe kwa wiki hiyo hiyo ili kupunguza 'kasi na ushawishi wake.
 
Hivi unafikiri CUF ina madhara gani kisiasa Tanzania mpaka wanachama wake kutekwa?..

Tujaribu kutoliweka kila jambo kwenye mlengo wa kisiasa, ili fikra zetu ziende mbali kidogo..
Nilisita kidogo kutaka kukubaliana nawe; lakini "fikra" hizo hizo unazozisema hapa zinaweza kabisa kukufikisha sehemu ambayo wewe umeidharau, yaani ya "CUF kutokuwa na madhara".

Hivi haiwezi kutumiwa kama kichagizo cha mambo mengine hata kama siyo ya kisiasa?

Hilo ni swali linalohitaji jibu.
 
Niliona kwenye taarifa ya habari. Nikajisemea moyoni kuwa bado wasijulikana wapoo eeennhhh.
Usalama wa taifa ni top priority nchi yeyote ile... mbinu zote legal na illegal zinatumika ili muwe na Amani na muda wa kupost humu na kupiga soga vijiwe vya kahawa.
 
Hapo kuna jambo polisi wanalijua na ndio watakuwa wanahusika. Sema hiyo ni hatari sana kama bado haya mambo yanaendelea.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom