Lindi: Wanachama watano wa CUF wadaiwa kutekwa na watu wenye silaha usiku wa manane

Kamugumya

JF-Expert Member
Aug 18, 2021
925
1,000
Hapo kuna jambo polisi wanalijua na ndio watakuwa wanahusika. Sema hiyo ni hatari sana kama bado haya mambo yanaendelea.
 

Frustration

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
1,269
2,000
Mtekaji anatafuta watekaji wenzake, kwani wamepoteana? Waache uzembe wa kijinga. Haya wapelekwe wakatoe ushuhuda kwa kayafa kuwa yesu ni muhalifu na yafaa ahukumiwe na ikibidi anyongwe.
 

Frustration

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
1,269
2,000
Msiwe mnakimbilia upotoshaji wa habari muwe wakweli hao watakuwa na makosa yao husika na wamekamatwa kwa jinai.
CUF haina impact yoyote hadi kupelekea kutekwa wafuasi wake.

Usikute ndio baadhi ya watanzania waliokuwa msumbiji na wamechukuliwa na kikosi kazi.
Usiku saa 7. Mbona hawapo kituo chochote cha polisi? Jambo gani lingine unalolijua polisi wakafanikisha tofauti na kusimamia mwenge?
 

Terrible Teen

JF-Expert Member
May 1, 2017
807
1,000
Muendelezo wa awamu iliyopita, halafu yule jamaa mwingine anasema sasa hivi hatapinga kama mwanzo, siasa ikitumika kama kitega uchumi ni hatari sana kwa usalama wa taifa na watu wake.

Baada ya siku kadhaa kelele zikizidi utasikia wamefikishwa mahakamani, kama shida yao ni kuwapeleka mahakamani kwanini kutekana usiku na silaha nzito? naona hawa askari wetu wanatamani vita, vyema wapelekwe Msumbiji wakasaidie huko.
umechanganya mambo mengi kwenye uzi mmoja
 

Kilwa94

JF-Expert Member
Aug 21, 2016
2,302
2,000
'Masisiemu' yameanza kutuchokoza wanakusini.Tutawashusha mishipa!
 

zitto junior

JF-Expert Member
Oct 7, 2013
14,014
2,000
Bro...asikudanganye mtu, hakuna CUF kusini labda kidogo ungesema ACT. Watu wa kusini na siasa zao ni tofauti na tunavyofikiri... hakuna kitisho cha CUF kusini labda asikudanganye mtu.
Wewe ndio hufuatilii, kama kuna eneo CUF ilibaki intact basi ni kusini. Hakuna defection za maana Lindi,Mtwara na Ruvuma kwenda ACT ukiachana na Mhe.Bwege tu. Wabunge ama wagombea wengi wa 2015 Wengi walibaki CUF ama kurejea CCM so ACT bado kupata numbers za CUF kule kusini.

Anyway uchaguzi uliopita sio kipimo but had it been ungeona ambavyo ACT ingegawana sana kura na CUF. Mfano yule Baruan, Bobali, Ngombale, Nachuma Maftah n.k waliopata kuwa wabunge walibaki CUF hawakumfuata Maalim ACT!! So usije ukadhani ACT ilibeba CUF wote kule.
 

VAPS

JF-Expert Member
Jul 10, 2012
5,356
2,000
Haya Mambo yanaudhi na kusikitisha. Kisa cheo na kujipendeleza!?
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
16,449
2,000
kesi ya mbowe 2020 amekuja kukamatwa 2021, labda hili litapata suluhu 2022.

Kwetu kila kitu ni cha ajabu, hewa au dhwaifu.

Kwetu maridhiano hapana hayo yana maana Zanzibar tu.

Picha mbaya kabisa kwa rais mzanzibari anayevutia ya maana kwao.
 

Faana

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
18,487
2,000
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Foka Dinya amekiri kutokea kwa tukio hilo akisema kwamba Jeshi la Polisi linaendelea na uchaguzi.

"Jeshi la polisi linaendelea na uchaguzi ili kubaini chanzo cha tukio na kujua wapi waliko" amesema Kamanda Dinya

Chanzo: Mwananchi
Ugonjwa wa magazeti ya siku hizi
 

SAGAI GALGANO

JF-Expert Member
Nov 13, 2009
33,435
2,000
Ni huko mkoani Lindi inasemekana wanaCuf hao walivamiwa makwao na watu waliokuwa wamejihami kwa siraha nzito na kutokomea nao kusikojulikana.

---
Watu watano wakazi wa Kijiji cha Rutamba Halmashauri ya Mtama wanadaiwa kuwa ni wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF), wamepotea tangu Oktoba 30, 2021.

Katibu wa CUF Wilaya ya Lindi, Shadhil Bosha amesema kuwa watu hao waliopotea ni wanachama wa chama hicho akidai kuwa walichukuliwa na watu wasiojulikana nyumbani kwao Oktoba 30, 2021 saa saba usiku.

"Tunaliomba Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa haraka ili familia na jamii iondolewe hofu," amesema Bosha.

Bosha aliwataja watu hao wanaodaiwa kupotea kuwa ni pamoja na Musa Fukutu, Hamisi Liendeka, Shaziri Chileu, Baraka Ali na Isumail Yahaya.

Mke wa Ismail Yahaya, Husna Litapwachi amesema Oktoba30, 2021 saa saba usiku walisikia mlango uikgongwa na watu watano huku akidai kuwa wawili wakiwa na silaha waliingia chumbani na kuwakuta wamelala kitandani na kuwaamuru washuke chini .

Litapwachi anasema baada ya hapo walikusanya simu na wakaondoka na mumewe.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Foka Dinya amekiri kutokea kwa tukio hilo akisema kwamba Jeshi la Polisi linaendelea na uchaguzi.

"Jeshi la polisi linaendelea na uchaguzi ili kubaini chanzo cha tukio na kujua wapi waliko" amesema Kamanda Dinya

Chanzo: Mwananchi
Hivi hawa majambazi wanaovaa uniform wanataka kulipeleka wapi Taifa hili? Division 4 point 32 ndiyo tabu yake
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom