Lindi: Ustadhi ahukumiwa miaka 20 na fidia ya laki 6 kwa kumtomasa mtoto wa miaka 12

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,499
9,279
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Lindi, imemuhukumu mkazi wa Kata ya RahaLeo, Ustaadhi Selemani Ally (58) kutumikia kifungo cha miaka (20) baada ya kupatikana na hatia ya udhalilishaji wa kingono kwa mtoto mwenye umri wa miaka {12}, jina limehifadhiwa.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu wa mahakama hiyo,Muyonga Makala baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa Mashitaka.

Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, mshitakiwa aliulizwa kama anazo sababu zitakazoishawishi mahakama isimpe adhabu kali kwa kosa linalomkabili, ambapo aliiomba asipewe adhabu kali na hatarudia tena kutenda kosa la aina hiyo.

Baada ya utetezi huo, Hakimu Makala alimuuliza mwanasheria wa Serikali, Yahaya Gumbo kama anazo kumbukumbu kwa makosa ya zamani na kujibu hana, lakini akaiomba mahakama kumpa mshitakiwa adhabu kali ili kukomesha vitendo vya udhalilishaji.

Hakimu Makala akitoa hukumu katika kesi hiyo namba 88/2020, kupitia kifungu 138 C (1) (a) (b) cha sheria kanuni ya adhabu sura ya 16 rejeo la 2002, akamhukumu mwalimu huyo wa madrasa, Selemani Ally kutumikia kifungo cha miaka 20 jela na atakapomaliza amlipe mlalamikaji fidia ya Sh,600,000/-.

Awali ilidaiwa mahakamani hapo na mwendesha mashitaka wa Serikali Gumbo, kuwa mshitakiwa ni mwalimu wa madrasa na amekabidhiwa watoto kuwafundisha elimu ya dini lakini amekiuka maadili na kumdhalilisha kingono mtoto huyo mwenye umri wa miaka (12).

Gumbo alidai kuwa mshitakiwa licha ya kuwa na umri mkubwa, amekuwa na tabia ya kumtomasa mtoto huyo bila ya ridhaa yake na baadae akalalamika kwa kutoa taarifa kwa wazazi wake, ambao nao walichukua hatua ya kulifikisha suala hilo Polisi, ambao walimfikisha mahakamani.

Mwananchi
 
Nazani hiyo stori hata humu jamii forumn ipo,ilitokea kama sikosei moshi,Binti ni Mwanafunzi,Mama yake ndiye aliyemshitaki Padiri.Ingawa naona na wewe unaonekana unamtetea Padiri
Hajatetewa, inatafutwa taarifa kamili before judging...
 
Mimi huwa naduatilia mahubiri ya hawa watu ninakuwa na hofu kuhusu malezi ya watoto wao

1. Hawana ibada tofauti kulingana na umri wa watoto

2. Ibada ni mchanganyiko wa watoto na watu wazima na mawahdha yanatolewa humohumo

3.Asilimia kubwa ya mawahdha niliyowahi kuyasikia sana yanalenga ndoa, talaka, Mambo ya mahusiano

4.Sasa watu kama akina kipoozeo na mafundisho ya ki comedy na watoto wapo humohumo utatarajia mtoto akitoka ibadani asiende kufanya practical?
 
Back
Top Bottom