lindi umasiki waathiri maendeleo ya shule

lifeofmshaba

JF-Expert Member
Feb 19, 2011
867
219
WANAFUNZI wa shule za msingi mkoani Lindi wamedaiwa wameacha masomo na kuamua kuwalea wazazi wao walioathirika na maambukizi ya magonjwa.

Mratibu wa Mradi wa Pasha mkoani Lindi, Sarah Mraponi alitoa taarifa hiyo wakati akizungumza na walimu wanasihi wa shule za msingi kutoka wilaya za Kilwa, Ruangwa, Nachingwea, Lindi Mjini na Vijijini.

Alisema, hali kwa wanafunzi hao si nzuri kwa kuwa wanabaki nyumbani badala ya kwenda shuleni.

Alisema, wamekata tamaa ya maisha kutokana na kukabiliwa na majukumu kabla ya wakati huku wakiyakosa masomo.

Wakati huo huo alisema, mfumo wa utandawazi unazidi kuangamiza wanafunzi kutokana na kufanya mapenzi kabla ya wakati na kuwa katika hatari ya kuambukizwa maradhi.

Alisema mitandao na picha za video hasa zinaoneshwa nyakati za usiku hasa vijijini, huwaathiri watoto kimaadili.

Alisema hali hiyo yote inasababisha wanafunzi wengi kufuata tamaduni za nje na kuacha za Kitanzania .
 
samahani hii post hiko hapa kwa makosa
hpe wataihamisha
pole kwa usumbufu
 
Back
Top Bottom