Lindi: RC Zainabu Telack ameagiza kuteketezwa kwa tani 24 za Korosho zilizopo Mtama

Wa
NImeziona hapo mtama nyuma ya ATM ya nmb Kuna mpaka mbao kibao sijui zilikamatwa lini zikatelekezwa pale..me nashauri serikali Bora igawe kwa wananchi vitu vyinavyokamatwa
Wangeziuza katika mfumo wa mnada. Hivi mkuu hiyo ofisi ya mbunge wa mtama hapo ina kazi gani? Maana sijawahi kumuona Nape akifika maeneo hayo badala yake anataka aharibu pesa ajenge ofisi nyingine pale kiwalala
 
Kwenye suala la korosho,
Serikali yetu ilishafeli na inaendelea kufeli.

Hii biashara walitakiwa waiche ijiendeshe yenyewe Kama yalivyo mazao mengine ya chakula.
Yule mchunga ng'ombe alivuruga kila kitu,alikufa tunanywesha soda mbuzi kwa pesa za korosho,akavuruga,rejea kunde nk
 
M
Hadi sasa korosho imeshashindikana kwa serikali

Mkuu wa mkoa wa Lindi Zainabu Telack akiwa kwenye kikao cha utekelezaji wa mpango wa kuboresha usimamizi wa huduma za ugani kwa wakulima wa korosho katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma na Pwani, ameagiza kuteketezwa kwa korosho tani 24 zilizopo ghala kuu la Mtama, lililopo halmashauri ya Mtama wilayani Lindi.

Hayo yamejiri baada ya Korosho hizo kupelekwa kwenye ghala kuu la hazina zikiwa na Grade One na Grade Two na baadae zikapoteza ubora na kushindwa kuuzika kwenye minada.

Sambamba na hilo Telack amewataka wakurugenzi wa halmashauri zote mkoa wa Lindi kuwawezesha maafisa ugani ili weweze kuwasaidia wakulima kwenye zao la korosho.

Chanzo cha habari Mashujaa FM
Mlikuwa mnatukana na kumsingizia Magufuri kuwa ndie anaua zao la korosho, Sasahivi hayupo huo mzigo mnantwisha yupi? maana mbebeshwa mabaya hayupo 🤣🤣mbona sijamwona waziri wa kilimo hakijinasibu mafanikio ya Samia ya utawala wa mwaka mmoja,ila watanganyika kwa unafiki utajambo.
 
Kwani
Meko ndio ameua zao la korosho na watu wanamsifia tu
Kwani Sasahivi yupo mbona hamfunyi? mbona mnasifia Samia kuwa amefungua mchi,mazao yote yamepata masoko ikiwemo mbaazi na maindi, Sasa Nini kimemshinda Samia kwa korosho, mpaka bado mnamuwaza Magufuri?
 
Wasiziteketeze wapeleke kwa wale wanaoandaa vyakula vya mifugo.
Tani 24 sio kdg. Halafu mbona hajataja thamani yake?! Zaidi ya kusema zilikua grade one!

Nani anajua? Lazima kuna mazingira ya uwizi wizi'

Hawa wanatoaga mzigo mzuri usiku usiku wanaingiza korosho zisizofaa. Ndio maana wanaona suluisho ni kuziteketeza ( kupiteza ushaidi)

Kwa nn wasichunguzwe!?
 
Dah kuteketeza? Kisa zimekosa wateja? Hilo nalo ni kosa kubwa sana. Kwani vile viwanda vya kubangua korosho vimekwenda wapi? Si waziprocess wenyewe ziuzwe zilizobanguliwa na kama zitakosa mteja tena hata mashuleni na majeshini zinaweza kugawiwa watu wakazila wakapata afya. Agizo la mh mkuu wa mkoa sio la kiungwana kwani korosho ni chakula nahaijasemwa kuwa zimeharibika au hazifai kwa matumizi ya binadamu.

Ukiprocess korosho unapata korosho yenyewe na mafuta pia ambayo ni material.nzuri kwa viwanda vya plastic kwani ndio hupolish vyombo vya plastic sasa ukiteketeza unapata nini?
Sababu si kukosa wateja, ila ni kutokuwa na ubora unaotakiwa kwa korosho kuingia sokoni(mnadani). Hapo kuna mchanganiko wa koroshi grade 1 na grade 2 ambazo hazifai.
 
Zao linaloingiza pesa nyingi za kigeni linachezewa kama kichwa cha hayawani kisa siasa za kijinga. Hii nchi inafelishwa sana na uongozi usio na maono zaidi ya kula kwa urefu wa kamba.
 
Back
Top Bottom