Lindi: Nyumba saba zachomwa moto kwa imani za kishirikina, ni baada ya mwanakijiji kupotea ghafla

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
nyumba.jpg

Wananchi wa Kijiji cha Nahukahuka A, Wilaya na Mkoa wa Lindi, wamechoma nyumba saba moto kwa kile kinachodaiwa kuwa imani za kishirikina.

Imedaiwa kuwa, tukio la kuchomwa kwa nyumba hizo saba lilitokea jana asubuhi ambapo wananchi hao wenye hasira waliamua kuchoma moto nyumba hizo zote za wanakijiji wenzao kutokana na kuamini kwamba mwenzao mmoja aliyepotea kijijini hapo katika mazingira ya kutatanisha siku tatu zilizopita na kuonekana ghafla juzi saa sita usiku alichukuliwa kichawi na wananchi waliowachomea moto nyumba zao.

“Kuna mtu alipotea katika mazingira ya kutatanisha siku tatu zilizopita, jana majira ya saa sita usiku alionekana akiwa katika hali mbaya nahajitambui. Wananchi wenye hasira kali walichukizwa na kitendo hicho, mapambazuko (alfajiri) wakachoma nyumba hizo moto, “alisema mmoja wa mashuhuda ambae hakutaka kutaja jina lake.

Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Mussa Bakari Namwanga bila kutaja jina wala umri wa aliyepotea na kuonekana katika mazingira ya kutatanisha alikiri kuwa tukio hilo limetokea katika kijiji chake. Ambapo hadi alipozungumza na Muungwana kutoka katika kijiji hicho hakukuwa na mtu aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo.

“Nikweli tukio hilo limetokea, wananchi wamechoma moto nyumba za wananchi wenzao kwa imani za kishirikina. Tukio hilo lilitokea alfajiri ya leo (jana) hivi navyozungumza nawewe, mheshimiwa diwani amekwenda Mtama kuripoti tukio hilo. Hakuna aliyejeruhiwa katika tukio hilo. Kwasasa bado hatujua kiasi cha mali ziliteketea na moto huo ,” alisema Namwanga.

Maelezo ya mwenyekiti huyo juu ya mazingira ya tukio hilo na sababu za wananchi hao kufanya ukatili huo dhidi ya wananchi wenzao, hayakutofautiana na maelezo yaliyotolewa na shuhuda ambae alikataa jina lake liandikwe kwenye habari hii.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga alisema ofisi yake ilikuwa haijapata taarifa yoyote kuhusiana na tukio hilo na kuahidi kufuatilia ili kupata ukweli.

“Mimi sina taarifa, ngoja nifuatilie kwawasaidizi wangu. Maana tumeamka kukiwa shwari, kwakifupi tumeamka kukiwa shwari, sasa kama kuna hilo acha nifuatilie, “alisema Kamanda Mzinga.

Serikali imekuwa ikikemea wananchi kujichukulia sheria mkononi kwa kuwauwa wenzao kwa tuhuma za kishirikina lakini bado jamii haina elimu ya kutosha kuhusiana na suala hilo.

Chanzo: Darmpya
 
Bongoland showoff haziish, rukwa nako watu wamekimbia maiti makaburini kisa mvua ya radi et marehemu hakua tayar kuzikwa. I think marehemu aliiwa Razaro
 
Back
Top Bottom