LINDI: M/kiti wa CHADEMA na Katibu wa tawi la Nyangamara wahukumiwa miezi 8 bila faini

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Lindi Suleiman Mathew Luwongo na Katibu wa CHADEMA tawi la Nyangamara wamehukumiwa kifungo cha miezi nane jela (bila faini).

Kosa walilokuwa wanatuhumiwa nalo ni kufanya mkutano bila kibali. Hukumu imetolewa leo 18.01.2017 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi. Walioshitakiwa walikuwa sita lakini wanne wameachiwa huru.

Ngatunga - Katibu Chadema Nyanda ya Kusini.

======

UPDATES:

Kwa mujibu wa Afisa Habari wa CHADEMA, Tumaini Makene amedai kuwa hukumu hii inaonekana ni ya kimkakati kwakuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Lindi alikuwa ni mmoja ya wagombea wa Ubunge katika jimbo la Mtama jimbo aliloshinda Nape Nnauye (Ambaye ni Waziri wa Habari).

Pia Mwenyekiti huyo alikamatwa siku ambayo Mbunge wa Kawe na Mwenyekiti wa Baraza ya wanawake CHADEMA(BAWACHA), Halima Mdee lakini hakukuwa na mkutano wa siasa.

Aidha wanasheria wa CHADEMA wanaangalia uwezekano wa kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.
 
Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Lindi Suleiman Mathew Luwongo na Katibu wa CHADEMA tawi la Nyangamara wamehukumiwa kifungo cha miezi nane jela (bila faini).

Kosa walilokuwa wanatuhumiwa nalo ni kufanya mkutano bila kibali. Hukumu imetolewa leo 18.01.2017 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi. Walioshitakiwa walikuwa sita lakini wanne wameachiwa huru.

Ngatunga - Katibu Chadema Nyanda ya Kusini
Haki imetendeka kabisa.............
 
Kwa wasioojua sheria, adhabu kama hizi hutumiwa pale inapotakiwa adhabu "iwe fundisho kwa wengine". Umezuka mtindo miongoni mwa jamii kwa watu kurudia makosa yale yale, wakipewa dhamana wanarudia makosa yale yale. Nadhani njia hii itasaidia kupunguza utitiri wa kesi kama hizi kwenye mambo yale yale sehemeu zile zile watu wale wale.

Trump alipendekeza adhabu hizi hizi kwa watu wanashitakwa kwa makosa ya law and order.

WM
 
Now this is too much........

Ina maana kwenye nchi hii wenye haki ya kufanya mikutano ya siasa ni CCM pekee?

Kwa kuwa kila kukicha tunawaona wao wakiongozwa na Mwenyekiti wao wakiendelea kufanya siasa bila kubughuziwa na Jeshi la Polisi.

Ina maana sheria za kuzuia mikutano ya kisiasa inawahusu vyama vya upinzani peke yao?

Demokrasia ya dizaini hiyo katika dunia nzima inapatikana only in TZ
 
Back
Top Bottom