Philipo Khan
Member
- May 14, 2016
- 37
- 44
Ni jambo la furaha sana kwa mkoa wa Lindi moja ya mikoa ya zamani iliyobakia nyuma kimaendeleo huenda kuliko mikoa yote iliyoanzishwa zamani.
Uwepo wa mradi huu mkubwa ambao utakua ni kivutio kikubwa cha viwanda mkoani Lindi ambavyo vitakua chachu ya maendeleo mkoani Lindi.
Hoja kubwa kwa wananchi wa Lindi je, wamejiandaa kuupokea mradi huu kinguvu kazi na uwekezaji wa kijasiliamali?
Ujio wa mradi huu utaenda sambamba na mahitaji makubwa ya nyumba za kupanga, vyakula kama nyanya, kuku, viazi, matikiti nk
Maana kutofanya hivyo kutasababisha watu wa mikoa mingine kuja kuchukua hizo fursa nanyi muendelee kubakia watazamaji wa maendeleo ya wenzenu
Kwa upande wa serikali imeanza kuandaa muindombinu ya nishati itakayohakikisha uhai wa viwanda hivyo?
Je wameandaa miradi ya maji toka kwenye vyanzo vya maji vya kudumu na uhakika? Maana viwanda bila maji ni kazi bure, hali ya upatikanaji wa maji mjini Lindi bado siyo nzuri, kuna mitaa ina miaka miwili mabomba yao hayajawahi kutoa maji.
Naunga mkono jitihada za serikali kuuweka mradi huo mkoani Lindi, eneo la likong'o ili kupunguza tofauti za kimaendeleo kati ya mikoa yake au ukanda na ukanda
Hongera Rais Kikwete, muasisi wa mradi huu.
Hongera Rais Magufuli mtekelezaji mkuu wa mradi huu