Lindelof ndani ya Maguire,na Maguire ndani ya lindelof

Matanga

JF-Expert Member
Nov 13, 2019
2,281
3,973
KAZI ya kwanza ya beki anapokua uwanjani ni kuzuia mashambulizi. Anafanya hivyo akihakikisha mipira hatari inayoweza kusababisha bao haimfikii golikipa. Kwa kufanya hivi, beki anawazuia wachezaji wa timu pinzani wasipate bao.

Achana na mabeki wa pembeni, kuna aina mbili za mabeki wa kati. Kwa lugha ya Kiingereza aina ya kwanza wanafahamika kama 'center-backs' huku aina ya pili wakifahamika kama 'sweepers'. Majukumu yao ni tofauti ingawa kazi yao inabaki kuwa sawa. Kuzuia mashambulizi.

'Sweepers' hawachezi kwa kukaba na kuwazuia washambuliaji wa timu pinzani kwa nguvu muda wote. Kazi yao ni kuondoa mpira kwenye eneo la hatari.

Kwenye mfumo wa 5-3-2, 'sweepers' hucheza kama beki wa kati kwenye msitari wa mabeki watano. Akicheza katikati ya mabeki wawili kulia kwake na mabeki wawili kushoto kwake.

Majukumu yake ni kuzunguka eneo la ulinzi, katikati akizuia mashambulizi. Anafanya majukumu haya akiwa huru. Hachezi kwa kumuangalia mchezaji mmoja. Hii inamrahisishia kukaba, kuponya mipira na kuindoa kwenye eneo la hatari.

Ukiachana na jukumu hili, 'sweeper' hutumika kama beki anayeanzisha mashambulizi kwa kupiga mipira mirefu kwenda mbele. Anatakiwa awe na uwezo mzuri wa kupiga pasi hizi kwa usahihi. Wakati mwingine husogea mbele kidogo ya eneo lake la ulinzi na kucheza kama kiungo mkabaji.

Wachezaji wa zamani kama Franz Beckenbauer, Gaetano Scirea, Bobby Moore, Franco Baresi, Ronald Koeman, Fernando Hierro na Matthias Sammer walikua na majukumu haya wakati wanacheza.

Si rahisi kuwapata wachezaji wa aina hii kwenye mifumo ya sasa ingawa wachezaji kama Daniele De Rossi, David Luiz, Leonardo Bonucci na Javi Martínez wanaweza kutumika kama 'sweepers'.

Tukirudi kwa 'center-backs', hawa ni mabeki halisi wa kati na wamegawanyika kwenye makundi mawili. Kuna wale wanaotengeneza 'base' yao upande wa kulia na wale wanatengeneza 'base' yao upande wa kushoto.

Mfumo wowote unaotumia mabeki wanne nyuma wanaomlinda golikipa huwa na mabeki wawili wa kati na mabeki wawili wa pembeni. Beki mmoja wa kati anacheza zaidi upande wa kulia karibu na beki wa kulia huku mwingine anacheza kushoto karibu na beki wa kushoto.

Mmoja kati ya mabeki hawa hucheza nyuma kidogo ya beki mwingine. Yaani hawatengenezi msitari mmoja. Wanafanya hivi kwa sababu, mpira unapompita mmoja kati yao kunakua na beki mwingine nyuma yake anyehakikisha anaouondoa kabla haujamfikia golikipa.

Mara nyingi beki wa mwisho kukutana na mpira huwa ni mrefu, mwenye nguvu, anayeweza kucheza vizuri mipira ya kichwa na ni mzuri kwenye kucheza 'tackling' na kufanya 'clearance' kwa haraka. Hii ni kwa sababu yeye ni mtu wa mwisho kabla ya kumfikia golikipa. Hivyo ni hatari kama mpira utampita.

Chaguo la beki gani wa kati anastahili kucheza nyuma ya mwenzake huwa ni chaguo muhimu sana. Kinachotakiwa kuangaliwa ni urefu, kasi, uharaka wa kufanya maamuzi hasa kwa kucheza 'tackling', 'clearance' na jinsi anaweza kuwapanga vizuri mabeki wenzake.

Baadhi ya mabeki hawa wa kati wanaweza kutumika kwenye eneo la kulia au kushoto. Inategemea anacheza na beki wa aina gani. Mabeki wengi hutumika kwenye eneo moja tu. Kama ni eneo la kulia, atacheza eneo hilo tu, kama ni eneo la kushoto basi atacheza eneo hilo tu.

Hii inasababishwa na mambo mengi. Mojawapo ni mguu anaotumia kupigia mpira mara nyingi. Mfano, mabeki wanaotumia mguu wa kushoto daima hucheza upande wa kushoto. Ni vigumu kwa mabeki hawa kucheza upande wa kulia kwa sababu upande huu unahitaji beki anayetumia mguu wa kulia.

Wale wanaotumia mguu wa kulia ndio hao wanaokuwa 'comfortable' kucheza upande wowote. Anaweza akacheza kushoto au kulia.

Harry Maguire. Tangu amesajiliwa Manchester United, amekua akitumika kama beki wa kati anayecheza upande wa kushoto. Alikua akicheza hivi tangu alipokua Leicester City. Hata kwenye timu ya taifa ya England amekua akicheza kwenye upande huu.

Victor Lindelof amekua akicheza pamoja na Maguire kama beki wa kati. Yeye 'base' yake ni upande wa kulia. Uwepo wao kama mabeki wa kati bado haujaiimarisha Manchester United kwenye eneo la ulinzi. Bado wanaruhusu mabao ya kufungwa. Hii imesababishwa na mambo matatu.

Kwanza ni Victor Lindelof. Kwa jinsi wanavyocheza, Maguire na Lindelof mara nyingi, Maguire amekua anacheza nyuma ya Lindelof. Yaani Lindelof anakua mtu wa mwisho.

Imekua hivi kwa sababu, Maguire ni beki anayejaribu kwenda mbele kutengeneza mashambulizi. Hivyo 'option' ya kumuacha yeye kama beki wa mwisho si nzuri. Ndio maana Lindelof hubaki kama beki wa mwisho.

Hii huleta matatizo. Lindelof anakosa sifa za beki wa mwisho. Moja si mrefu, hii ina maana anaporuka juu kujaribu kuucheza mpira wa kichwa, uhakika wa kuucheza mpira huo ni mdogo. Pili, si mzuri kwenye kufanya 'clearance'.

Unapokua na beki wa aina hii, kama beki wa mwisho ni hatari kwa sababu, mipira mingi ya hatari inaweza kumfikia golikipa na kusababisha bao.

Pili, si busara kumtumia Maguire kama beki wa mwisho kwa sababu, hana kasi na si mzuri kwenye kufanya 'tackling'. Ana uzito wa kilo 100. Hivyo anapokutana na mchezaji mwenye kasi inakua rahisi kuachwa.

Silaha yake kubwa ni kwenye kucheza mipira ya kichwa na kwenye makutano ya ana kwa ana. Udhaifu wake hasa kwenye kasi ndio uliomfanya Kocha Pep Guardiola apunguze matamanio ya kutaka kumsajili.

Tatu, Lindelof ni beki aliyekua akicheza upande wa kushoto. Tangu akiwa Benfica na hata timu ya taifa. Si beki wa mwisho.

Alipokua Benfica alicheza mechi nyingi pamoja na Luisao. Akiwa Manchester United kabla ya kuja kwa Maguire, alikua akicheza upande wa kushoto na alionekana kufanya vizuri.

Kwa maana hiyo, Lindelof na Maguire ni mabeki wa aina moja. Wote ni wazuri wakicheza upande wa kushoto huku wakiwa mbele ya beki mmoja anayecheza nyuma yao kama beki wa mwisho.

Ubora wao unategemea na aina ya mabeki anaocheza nao. Yaani kama atacheza na beki mwingine wa kati anayeweza kuficha madhaifu yao kwa kuwa na kasi, kufanya 'tackling' na 'clearance' nyingi.
 
Kuna mabeki wazuri kama Gabriel Megalhaes na Kieran Tierney pale Arsenal, wako akina Van Dijk, TAA, Robertson..... Bora tukawajadili hao sio hizo takataka za Pundamilia Fc.............

#COYG
#ARSENAL MABINGWA EPL 2020/2021
Hongera kwa ubingwa wa kwenye makaratasi mkuu
 
Man Utd wanapitia kipindi kigumu sana,fukuza huyu Kocha analeta utoto mwingi.
Tutafukuza makocha wangapi mkuu?? Au unataka tuwe ka MLIPUKO FC ambao Wana idadi kubwa ya makocha kuliko makombe waliyoyachukua
 
Sawa Edo 2.
 
Maguire ndo kavunja rekodi ya VVD ..
Na Kepa ndo kavunja rekodi ya Alison..

Aibu Sana Kwa kweli
 
Umechambua vizuri sana ..
Tunahitaji articles kama hizi hapajf.
Sio.ushabiki maandazi
 
Man United ni mbovu na itachukua mda kukaa sawa huyo Maguire ni bonge la beki ngoja atoke hapo aende timu nyingine utaona Moto wake .

Mwisho mtoa mada nitajie wachezaji walitoka man u wakashindwa ku perfome nje ya man United kuanzia Memphis depay lukaku Sanchez all are doing good na hata Sancho ambaye man u wanamtaka akija man u anakuwa yikpe tu
 
Unajua maana ya neno SWEEPER kwenye soka SWEEPER ni beki wa kat ambae yupo free kwenda upande wowote kusaidia ukabaji kwa beki mfano halisi ni Van di jk pale livepool au km uliwah kumuona puyol pale barcelona nadhan utaelewa maana ya neno sweeper sweeper ni km captain wa mabeki ana uwezo wa kumwambia full back aje kati km central back na yy acheze pemben km full back hawa akina maguire cjui lindef mm huwa siwaelew kabisa yaan Man U kwa sasa ni mbovu kabisa hawana sweeper hawana full back hawana player maker hawana false 9 hawana free kick specialist hawana winga za maana hawana crosser hawana box to box wala engine yoyote pale kati hawana clinical finisher yaan ukiangalia wanavyocheza unaona kabisa wanakimbiakimbia na hawajui wanachokitaka man city na liverpool hawa wapo vzr zaid kila mchezaji ana majukumu japokuwa liverpool ni bora kwa upande wa mabek
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom