lindege la jeshi la uwa mtu moja na kuzimisha tv mtaani kwangu.

Fede Masolwa

JF-Expert Member
Oct 26, 2013
528
123
wakuu kuna lindege la jeshi limepita muda simrefu nadhani kuelekea taifa sasa, limeua mtu moja aliyekuwa mgonjwa kiasi na tv zote mtaani kwangu kukata kabisa ata channel moja hakuna, limepita kwa mshituko mkubwa sanaaaa kwani yasipite baharini huko.
 
Wapi yametokea hayo? Visigwa,msolwa,chalinze au?

ni dar tena sijui lilikuwa linatokea lugalo, ilipita ya kwanza vizur tu, iliyofata sasa imepita kwa mshituko na mtetemo mkubwa sanaanadhan wagonjwa weng wa moyo watakuwa wameshituka... Sijui kwanini.
 
Litakua limesababisha Electromagnetic pulse(EMP)hadi kuweza kuzima tv.
 
wakuu kuna lindege la jeshi limepita muda simrefu nadhani kuelekea taifa sasa, limeua mtu moja aliyekuwa mgonjwa kiasi na tv zote mtaani kwangu kukata kabisa ata channel moja hakuna, limepita kwa mshituko mkubwa sanaaaa kwani yasipite baharini huko.

Poleni sana na msiba huo, hizo ndo shmra shamra za kusherehekea Uhuru.
 
ni dar tena sijui lilikuwa linatokea lugalo, ilipita ya kwanza vizur tu, iliyofata sasa imepita kwa mshituko na mtetemo mkubwa sanaanadhan wagonjwa weng wa moyo watakuwa wameshituka... Sijui kwanini.

Dar ni kubwa. Weka wazi specifically ni g/mboto, tabata, lugalo, masaki au wapi. By the way poleni sana
 
na mlivyokuwa mnashabikia vita na Rwanda..kumbe zikipita tu mnakufa kwa presha..
 
Ndio kishaungua hivyo... Uyo mgonjwa alikua anaumwa nini? Kafa siku ya uhuru.. RIP mzalendo
 
Hapa tabata ya kwanza vizuri ila ya pili kingamuzi changu cha startimes kimesema no signal mpaka naondoka saa sita ,sijui alitumia supersonic sound maana kuna mwendo wa sauti miongoni mwa ndege za kivita

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 
Kumbe kagame angetumaliza asubuhi na mapema, kama li ndege limoja tuu lililochoka choka linapita angani TV zinazimika zenyewe na watu wanajifia kwa kihoro, jee linge rusha bomu, si mtaa mzima ungezima!
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom