Limekaaje suala la madalali kulipwa kodi ya mwezi mmoja?

Madalali ni muhimu sana maana huwezi kutembea mtaa kwa mtaa kutafuta nyumba...utachukua miezi kuipata. Madalali ukitaka uone umuhimu wao uwe na bidhaa unauza au unataka kumunua hasa nyumba au kiwanja. Nadhani tuendelee kuwaheshimu hawa watu
ishu sio umuhimu wao ishu ni hiyo kodi ya mwezi walipe kodi kama ni halali wao kupewa wawe kisheria na watambulike ili kusiwe na migongano.
 
udalali ni wizi na utapeli wa kisasa ambao hautumii nguvu,saiv adi watoto wadogo ni madalali ,
 
Kwahiyo mnataka mtulipe sh ngapi? Kama vipi tafuteni wenyewe nyumba za kupanga. Niwaambie tu hiyo ni kanuni kama ilivyokanuni nyingine..

Kwa aliekaribu na sinza aje muda huu nimetoka kukunja laki 2 ya mpangaji ,njoo tupige gambe
 
Akitokea mwekezaji akaanzisha mfumo mzuri wa kimtandao wa kupangisha nyumba, vyumba, warehouses nk.

Kuwe na vigezo vya kuwabaini wenye nyumba kama takwa la kujisajili.

Huu mfumo utatengenezwa kimaeneo, kwamba nikiwa singida na ninahitaji chumba arusha niwe na uwezo wa kuangalia nyumba ama vyumba vinavyopatikana katika wilaya, kata, na mitaa husika na occupancy status.

Mfumo uwe na database ya wateja wote, waliokwisha pangisha nyumba vyumba, na wale wakorofi, wenye kadhia mbalimbali wawe reported na kuwe na list ya wapangaji wakorofi wote wasiolipa na matukio mengine yasiyofaa, hii itawapa fursa wapangishaji kujua tabia ya mpangaji wake mpya kwasababu kutakuwa na records za nyumba zote alizopanga, na wenye nyumba lazima waache reviews za wapangaji wao pale wanapo hama. Unaweza kuhisi itakuwaje kama mwenye nyumba kamchafua mpangaji wake kwa maksudi ili asipokelewe sehemu zingine atakazo kwenda kuomba kupanga, jibu ni kesi yoyote ya mpangaji na mpangishaji lazima iwe reported na inapothibitika mwenye nia ovu ni mpangaji basi profile yake inaweza kuwekewa nyota ndogo kuonesha yeye ni mpangaji msumbufu au asielipa kwa wakati.

Hili project inaweza kusimamiwa na serikali na itapata makusanyo mengi sana ya kodi.

Hapa madalali (kamfukoo jitegemeee)
Not easy km unavyoongea ongea apo hamilet tu bado hazijapimwa mfumo wa address bado bomu mtu kufika eneo husika tu shida ndio ije iyo haiwezekan kwa sasa
 
Kwahiyo mnataka mtulipe sh ngapi? Kama vipi tafuteni wenyewe nyumba za kupanga. Niwaambie tu hiyo ni kanuni kama ilivyokanuni nyingine..

Kwa aliekaribu na sinza aje muda huu nimetoka kukunja laki 2 ya mpangaji ,njoo tupige gambe

Mkuu unalipa kodi serikalini?
 
Hii ni huduma tu, anaelipa ni mwenye nyumba
Kumbe unafanya kazi ya u-agent lakini hujui hata maana yake? Hospitali zinatoa huduma, shule zinatoa huduma, vipi wao wasilipe kodi. Hiyo huduma unayotoa ni chanzo chako cha kipato. Ndio maana tunasema iwepo regulatory board kwa ajili ya real estate agents, mlipwe stahiki zenu, mlipe kodi stahiki, mlipwe kwa viwango vinavyoeleweka. Kama ni 10% basi ijulikane hivyo.
 
- Na wenye nyumba wanavyopendana na madali sasa.

- Kuna nyumba ukienda hupewi chumba/nyumba mpaka uje na dalali.

- Mwenye nyumba unakuta kashaset anapangisha chumba 70000 dalali anakuja anamwambia mzee usitoe chumba hichi nakuletea kichwa cha laki moja, mwenye nyumba hapo ni full shangwe na kumwona dalali ndio mtu.
Kweli hapo meno nje!
 
Serikali iliangalie hili la madalali,mbaya zaidi wanapandisha bei kubwa Sana Zaid ya muuzaji bidhaa au mwenye nyumba.

Walau Sasa wajisajili na wawe na kiwango fixed Cha service yao
 
Back
Top Bottom