Manton
JF-Expert Member
- Mar 27, 2012
- 1,164
- 1,520
Nakusalimu katika lugha ya kiungwana sana,lugha asilia isiyo na chembe chembe za utumwa wala ubaguzi.
'Abawe naiwe mugumile?' maana yake 'wote hamjambo?' Jibu hivi; 'tugumile chwena!' yaani umejibu "sote hatujambo!"
Baada ya salamu tuelekeze fikra zetu katika kichwa cha uzi huu, kisemacho, jina mwaka wa 2020 katika lugha asilia ya kihaya ni LIMA EMILALA yaani likimaanisha 'lima matuta.' Bila kuweka kando mwaka 2019 uliopata jina la 'Birug'omumpita' likimaanisha "Upatikana kwa jasho."
Imekuwa ni desturi kwa Wahaya kila mwaka kuupatia jina lake tofauti na mwaka mwingine kama tulivyoona.
Tangu mwaka 1954 utaratibu huu umekuwa rasmi kwani kila mtu uwa na shauku ya kujua mwaka unaofuata utaitwaje! Na mimi nikaona vema nisiwe mchoyo wa habari, maarifa na taarifa kwako msomaji nikitarajia nawe utakuwa tayari kutushirikisha jina la mwaka 2020 katika lugha yako asilia ni lipi bila kusahau, kutuelezea maana yake kwa lugha ya Kiswahili, Kifaransa, Kichina (Kimandarini) Kiarabu, Kihindi ama Kiingereza.