Lile shamba nililokuwa nauza hatimaye nimefikia hapa

igihumbi

JF-Expert Member
Feb 20, 2017
441
350
Habari wapendwa,

Poleni na majukumu kunakipindi nilikutana na changamoto flani nikataman niuze baadhi ya vitu kimoja wapo lilikuwa ni shamba langu lile la Kilosa. Nashukuru Mungu sikupata mteja maana bei nilio kuwa nauza na ninacho kiona sasa nilikuwa nauza bei sawa na bure.

1. Zao la ufuta linakubali vizuri
2. Mahindi yanakubali vizuri pia
3. Mihogo inakubali vizuri sana
4. Kuna kunde
5. Maboga

Kiukweli aridhi ya KILOSA iko vizur sijawahi ona pia hakuna wanyama wala mifugo wenyeji wa huku kwa hekari moja huwa wanatoa hadi gunia 35 za mahindi na kukiwa kuna hali mbaya ya hewa wanapata gunia had 25 za mahindi kwa heka.

Kilimo cha huku KILOSA mara mbili kwa mwaka kuna mvua za vuri na masika.

Ni heka 3 yani (70×70) (70×70) (70×70) najiona mbali sana nikijitazama wenyeji wamenihakikishia sikosi chini ya gunia 80 kwa heka zote tatu na bado nimepanda na kunde ndani yake.

Mfano. bei ya chini ya mahindi iwe 30000
30000×80 idadi ya gunia
Gharama zote kama kulima na palizi na kuangalia shamba zinalipwa kwa kupitia kunde.

Nilitaka kuuza shamba kwa 350000 kila heka ambayo jumla ningepata 1,100,000 ila leo nakuja kupata sio chini ya 2,000,000 na bado aridhi ni naendelea kuimiliki.

Ushauri kwa Watanzania wote.

Aridhi inalipa jamani kupitia shamba naweza nunua kiwanja ila kupitia kiwanja kwasababu shamba linazalisha kiukweli fanya yote ila aridhi inalipa sio lazima ulime unaweza ukakodisha au ukafanya ufugaji.

IMG-20191117-WA0000.jpeg
IMG-20191117-WA0001.jpeg
IMG-20191117-WA0002.jpeg
 
Jembe Halimtupi Mtu
Wakulima Wa Mahindi, Asipangiwe Bei, Bei Itajipanga Yenyewe
Huko Kuna Rutuba Sana
Nilipita Njia Ya Kutokea Mikumi Hadi Kilosa, Dumila
Ardhi Nzuri Sana Watu Wengi Sana Wanalima
Nimekumbuka Kuna Kijiji Kimoja Kinaitwa ULAYA
 
Hongera

ila naona kama ni shamba LA jirani yangu vile..

Shamba lako nilitarajia nione mihogo,ufuta,kunde na maboga..

umeotesha na baiskeli?
 
Hongera

ila naona kama ni shamba LA jirani yangu vile..

Shamba lako nilitarajia nione mihogo,ufuta,kunde na maboga..

umeotesha na baiskeli?
Hapana hiyo baiskeli ni ya kijana wangu wa shamba . Ila ngoja nifabye parizi kunde utaziona vizur mkuu
 
Jembe Halimtupi Mtu
Wakulima Wa Mahindi, Asipangiwe Bei, Bei Itajipanga Yenyewe
Huko Kuna Rutuba Sana
Nilipita Njia Ya Kutokea Mikumi Hadi Kilosa, Dumila
Ardhi Nzuri Sana Watu Wengi Sana Wanalima
Nimekumbuka Kuna Kijiji Kimoja Kinaitwa ULAYA
mkuu Kilosa iko vizuri kuukweli kiujumla mkoa wa Morogoro umebarikiwa sijawahi ona
 
mkuu Kilosa iko vizuri kuukweli kiujumla mkoa wa Morogoro umebarikiwa sijawahi ona
Maeneo Mengi Sana Mazuri Ardhi Yenye Rutuba Sana
Nilikwenda Mkuyuni Njia Ya Kwenda Matombo Yaani Matunda Na Vyakula Tele, Maeneo Ya Kisaki Hatari
 
Maeneo Mengi Sana Mazuri Ardhi Yenye Rutuba Sana
Nilikwenda Mkuyuni Njia Ya Kwenda Matombo Yaani Matunda Na Vyakula Tele, Maeneo Ya Kisaki Hatari
mkuu ulipo sema Kisaki umenikumbusa mbali sana kule kuna kuku wengi sana yani mtu kula nyama ya kuku tena wakienyeji ni kitu cha kawaida ila wale wa dar inabaki historia
 
mkuu ulipo sema Kisaki umenikumbusa mbali sana kule kuna kuku wengi sana yani mtu kula nyama ya kuku tena wakienyeji ni kitu cha kawaida ila wale wa dar inabaki historia
Dar es salaam Hakuna Kuku, Haa😁😀😂😃😄😅😅
Watu Wanalishwa Chemical, Yaani Mtu Anayetoka Mikoani
Mfano Akafika Soko Lolote Akaonyeshwa Machinjio Ya Kuku

Hatakula Kuku Tena, Kwanza Atashangaa Vifaranga Ndiyo Wanaochinjwa

Mikoani Huko Kuku Anajitafutia Chakula
 
Mkuu unalimia kilosa sehemu gani?
mkuu ulipo sema Kisaki umenikumbusa mbali sana kule kuna kuku wengi sana yani mtu kula nyama ya kuku tena wakienyeji ni kitu cha kawaida ila wale wa dar inabaki historia
 
NAUZA KIWANJA KILOSA NA BABATI.

Morogoro wilaya ya kilosa Eneo la Miyombo lina ukubwa wa Ekari tatu na Nusu bei ni milion 25 tu. Karibu sana.

Kiwanja cha Babati kipo kata ya Singe kijiji cha Maitsa. Ukubwa wa Ekari moja bei ni million 4.5.
Karibuni wadau. Viwanja hivi vipo maeneo yenye rutuba hivyo unaweza kulima chochote au kujenga.

Kwa mawasiliano piga: +255621856340

CCA41BFD-A72F-4316-8D17-9C85FAAEE78E.jpeg

C9F4D2F2-FED1-4B69-939F-770B8CEE5C8F.jpeg

A73D3EAA-9FE8-4F79-9665-C9F3DE3477BB.jpeg

E3B708C6-2ADF-4CDF-BEE1-CECD2D38C0DF.jpeg
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom