Lijue kundi la kiharifu la PCC la nchini Brazil

elmagnifico

JF-Expert Member
Jul 7, 2011
8,260
9,704
Premier Commando de le Capitale (PCC)

Rio De Jeneiro

Tarehe 2, mwezi wa 10 mwaka 1992, ndani ya gereza kubwa linalo hifadhi wahalifu sugu katika nchi ya brazil, lijulikanalo kama gereza la Carandiru, kulizuka mapigano baina ya makundi mawili hasimu katika gereza hilo.
Chanzo cha ugomvi huo yalikuwa mabishano baina ya wafungwa wawili ambao kila mmoja alikuwa kundi pinzani na mwenzake.
Mabishano hayo yalipelekea kuzuka mapigano baina yao, ambapo mapigano yalienea na kupelekea kuwa ugomvi mkubwa baina ya wanachama wa kundi moja dhidi ya kundi pinzani.
Wafungwa waliuana kwa kukatana vichwa, kula nyama na kunywa damu ya wapinzani wao kama mazombie.
Chanzo cha ugomvi ni mabishano ambayo yalianza wakati wa mechi ya mpira mida ya saa nne asubuhi. Ugomvi huo ulikuwa na kugeuka kuwa ugomvi mkubwa kwenye gereza lote ambalo lilikuwa na zaidi ya wafungwa zaidi ya wafungwa 7000, huku uwezo wake ukiwa kuhifadhi wafungwa 3,500 tu.
Ilipofuka saa nane mchana, wafungwa walikuwa wanachoma magodoro na kuyaweka kwenye njia ya kuingilia gerezani ili kuwazuia polisi wasiweze kuingia ndani ya gereza hilo.
Polisi walijaribu kuzungumza na wafungwa ili kufikia makubariano wamalize ugomvi na kurudisha utulivu katika gereza hilo, lakini juhudi zao hazikuzaa matunda ndipo polisi wakutulizia ghasia walivamia gereza hilo na kuwapiga risasi wafungwa 111 wakauawa na wengine wengi wakajeruhiwa.
4e2f0104fbd1a3466a5d00a14e340973.jpg

Wafungwa waliobaki, walilazimishwa kuvua nguo na kulala chini.
Habari za mauaji hayo zilisambaa kwa kasi nchini Brazil, ndugu na jamaa za wafungwa wakajazana nje ya gereza kila mmoja aliwa ana hofu juu ya uhai wa ndugu yake lakini polisi walizuia watu kusogelea hilo gereza kwa siku mbili bila hata kuwaruhusu kutambua miili ya ndugu zao.
2c61ed51b19527ab9c40c9e15209e65e.jpg

5a5284b3d861c8739bb5db98afaaa589.jpg

a745efda6af7731038107599e62f78cd.jpg

Kuzaliwa kwa kundi la kihalifu la Premier Commando de le Capitale (The First Command of the Capital)

Kutokana na mauaji hayo yaliyotokea gerezani hasa kwa polisi kuua zaidi ya wafungwa 111, kulizuka hisia mbaya juu ya jeshi la polisi kuwa wamefanya mauaji makusudi kwa wafungwa hao hasa baada ya miili ya wafungwa wengi waliouwa kukutwa ina risasi zaidi ya tano.
Premier Commando De le Capitale (PCC), ilianzishwa mwezi wa nane mwaka 1993, katika gereza lijulikanalo kama Big Paranha lilipo katika mji wa Taubate, 130 nje ya mji wa Sao Paul.
Wakiwa katika mechi ya mpira, marafiki nane waliamua kuanzisha kundi ambalo litakuwa na lengo la kulinda wafungwa dhidi ya unyanyasaji wa polisi kwa wafungwa katika magereza, wazo hilo lilitokana na tukio la mwaka 1992 nililoeleza hapo juu.
Waanzilishi wa PCC wanajulikana kwa majina yafuatayo: Misael "Misa" Aparecido da Silva, Wander Eduardo "Cara Gorda" (Big face) Ferreira, Antônio Carlos Roberto da Paixão, Isaías "Esquisito" (Bizarre) Moreira do Nascimento, Ademar "Dafé" dos Santos, Antônio "Bicho Feio" (ugly beast) Carlos dos Santos, Caesar "Césinha" (Little Caesar) Augusto Roris da Silva and José "Geleião" (Big jelly) Márcio Felício.
Na kundi hilo lilianza kama timu ya mpira wa miguu katika gereza hilo, na waliamua kuliita PCC likiwa na maana Premier Commando de la Capitale au Party of Crime.
177a9e844a2776a64c8af57269260b97.jpg

Pia linajulikana kama 15:3:3, yani ukitazama mpangilio wa herufi za alfabeti "P" ni wa 15 wakati "C" iko namba 3 hivyo PCC ni 15:3:3.
Kundi hili lilikuwa na kusambaa magereza mengine ndani ya mji wa Sao Paul, ambapo kwa sasa inakadiliwa kuwa lina wanachama zaidi ya 13,000, na ni kati ya makundi ya kihalifu na yanayo ogopwa sana nchini Brazil.
Kundi hili linajihusisha na biashara za madawa ya kulevya, utekaji wa kudai malipo, mauaji ya kulipwa, kukusanya ushuru kutoka kwa makundi madogo yanayofanya biashara ya madawa ya kulevya Sao Paul ili wapate ulinzi kutoka kwa kundi hili dhidi ya wapinzani wao na mgao kutoka shughuli yoyote haramu itakayofanyika ndani ya Brazil.
Inasadikiwa kwamba, hakuna shughuli yoyote haramu iwe wizi, ujambazi, utekaji n.k inayoweza kufanyika bila PCC kuwa na taarifa ya shughuli hiyo na ni lazima wapate mgao hata kama hawakushiriki kwenye kutekeleza shughuli hiyo.

Mwaka 2006, mwezi wa saba, mamia ya wafungwa ambao walikuwa ni viongozi wa makundi ya kihalifu walikuwa wahamishwe kwa siri kutoka magereza mbalimbali ili wakawekwe kwenye gereza moja lijulikanalo kama Presidente Venceslau ambalo lina ulinzi mkali liliwa umbali wa kilometa 500 kutoka Sao Paul.
Kutokana na polisi wala rushwa, habari hiyo ilivujishwa kwa viongozi wa PCC.
PCC ilianzisha mapambano pamoja na mgomo kwenye magereza yote ya Sao Paul yaliyokuwa na wafungwa zaidi 150,000, pia walianzisha mashambulizi dhidi ya vituo vya polisi, uvamizi wa mabank, mahakama, maduka vituo vya mabasi kwa kutumia wanachama wake walioko nje ya magereza ambapo zaidi ya watu 150 waliuawa.
7459dfafb869e6c37fec34cb325ad5ae.jpg

Hii ilizidi kuishtua serikali ya Brazil juu ya nguvu na mtandao mkali ambao PCC imejijengea ndani ya jimbo la Sao Paul.
Kutokana na matukio haya polisi walishindwa kuwahamisha hap viongozi wa magenge na kauli mbiu ya PCC ya "One for all, all for one" ilizidi kupata umaarufu na vijana wengi wakapenda kujiunga na kundi hili la kiharifu linalojinasibu kuwa limeanzishwa kupinga uonevu wa mfumo wa polisi dhidi ya wafungwa.
Wanachama wa PCC upatikana kwa kupewa jukumu la kutimiza kazi flani hasa kuua, kuteka n.k na mwanachama mpya uwa anazidi panda ngazi za uongozi kutokana na kukamilisha majukumu anayopewa kwa weledi.
Mpaka sasa serikali ya Brazil inawatambua na kuwafahamu viongozi 1,500 wa PCC huku ilidai kundi hili lina zaidi ya wanachama 20,000
Ili mfungwa aweze kulindwa na hili kundi akiwa gerezani inabidi kulipia kiasi cha pesa ya Kitanzania 38,000 kwa mwezi huku wale waliomaliza muda wao, huutajika kulipia mchango wa kiasi cha pesa ya Kitanzania 1,334,000.
PCC uendesha pia uuzaji wa dawa za kulevya magerezani, mauaji ndani na nje ya magereza kwa malipo maalumu, pia ina miliki maafisa wengi wa polisi hasa polisi magereza ambao uwa inawalipa kwa ajili ya kutoa taarifa.
Kwa madai ya viongozi wa PCC uwa wao hawamuui mtu bila sababu, wanasema ni damu kwa damu ukiuawa basi umefanya kosa dhidi yao au dhidi ya mtu aliyewatuma wakuue.

**** Tukutane hapo baadae kwenye thread yangu itakayohusu tukio moja hatari lililokuwa na mkono wa PCC***
 
Hao wafungwa 'wanadekezwa' na sheria zao..

Africa wafungwa hao wote 'wangelazwa salama' na NDUGU zao wangepewa kesi ya kuvamia gereza
Ni kweli kabisa...hapo ni mkono wa rushwa..tangu lini wafungwa wakatunishiana misuli na serikali....usikute mabosi wa hilo kundi ni viongozi wakubwa serikali...nchi za bara la America kusini zinamatatizo makubwa sana hasahasa sababu ya kushamir kwa biashara ya madawa ya kulevya...
 
Aiseeeee,, hyo local mafia iko powa saaana,,, japokua hapo inaonesha serikali hyo imekithiri rushwa kubwa,,,
Hapo ndo utajua Dunia n uwanja fujo
 
Sijaisoma.

Vp imeisha au unaendeleza maana upo vzr kwa kutuachia alosto..
Wanaua hadi polisi mtaani ukiua mmoja wanaua familia nzima, usidhani ni panya road na linawanachama wengi wanaojulikana na wasiojulikana
 
Premier Commando de le Capitale (PCC)

Rio De Jeneiro

Tarehe 2, mwezi wa 10 mwaka 1992, ndani ya gereza kubwa linalo hifadhi wahalifu sugu katika nchi ya brazil, lijulikanalo kama gereza la Carandiru, kulizuka mapigano baina ya makundi mawili hasimu katika gereza hilo.
Chanzo cha ugomvi huo yalikuwa mabishano baina ya wafungwa wawili ambao kila mmoja alikuwa kundi pinzani na mwenzake.
Mabishano hayo yalipelekea kuzuka mapigano baina yao, ambapo mapigano yalienea na kupelekea kuwa ugomvi mkubwa baina ya wanachama wa kundi moja dhidi ya kundi pinzani.
Wafungwa waliuana kwa kukatana vichwa, kula nyama na kunywa damu ya wapinzani wao kama mazombie.
Chanzo cha ugomvi ni mabishano ambayo yalianza wakati wa mechi ya mpira mida ya saa nne asubuhi. Ugomvi huo ulikuwa na kugeuka kuwa ugomvi mkubwa kwenye gereza lote ambalo lilikuwa na zaidi ya wafungwa zaidi ya wafungwa 7000, huku uwezo wake ukiwa kuhifadhi wafungwa 3,500 tu.
Ilipofuka saa nane mchana, wafungwa walikuwa wanachoma magodoro na kuyaweka kwenye njia ya kuingilia gerezani ili kuwazuia polisi wasiweze kuingia ndani ya gereza hilo.
Polisi walijaribu kuzungumza na wafungwa ili kufikia makubariano wamalize ugomvi na kurudisha utulivu katika gereza hilo, lakini juhudi zao hazikuzaa matunda ndipo polisi wakutulizia ghasia walivamia gereza hilo na kuwapiga risasi wafungwa 111 wakauawa na wengine wengi wakajeruhiwa.
4e2f0104fbd1a3466a5d00a14e340973.jpg

Wafungwa waliobaki, walilazimishwa kuvua nguo na kulala chini.
Habari za mauaji hayo zilisambaa kwa kasi nchini Brazil, ndugu na jamaa za wafungwa wakajazana nje ya gereza kila mmoja aliwa ana hofu juu ya uhai wa ndugu yake lakini polisi walizuia watu kusogelea hilo gereza kwa siku mbili bila hata kuwaruhusu kutambua miili ya ndugu zao.
2c61ed51b19527ab9c40c9e15209e65e.jpg

5a5284b3d861c8739bb5db98afaaa589.jpg

a745efda6af7731038107599e62f78cd.jpg

Kuzaliwa kwa kundi la kihalifu la Premier Commando de le Capitale (The First Command of the Capital)

Kutokana na mauaji hayo yaliyotokea gerezani hasa kwa polisi kuua zaidi ya wafungwa 111, kulizuka hisia mbaya juu ya jeshi la polisi kuwa wamefanya mauaji makusudi kwa wafungwa hao hasa baada ya miili ya wafungwa wengi waliouwa kukutwa ina risasi zaidi ya tano.
Premier Commando De le Capitale (PCC), ilianzishwa mwezi wa nane mwaka 1993, katika gereza lijulikanalo kama Big Paranha lilipo katika mji wa Taubate, 130 nje ya mji wa Sao Paul.
Wakiwa katika mechi ya mpira, marafiki nane waliamua kuanzisha kundi ambalo litakuwa na lengo la kulinda wafungwa dhidi ya unyanyasaji wa polisi kwa wafungwa katika magereza, wazo hilo lilitokana na tukio la mwaka 1992 nililoeleza hapo juu.
Waanzilishi wa PCC wanajulikana kwa majina yafuatayo: Misael "Misa" Aparecido da Silva, Wander Eduardo "Cara Gorda" (Big face) Ferreira, Antônio Carlos Roberto da Paixão, Isaías "Esquisito" (Bizarre) Moreira do Nascimento, Ademar "Dafé" dos Santos, Antônio "Bicho Feio" (ugly beast) Carlos dos Santos, Caesar "Césinha" (Little Caesar) Augusto Roris da Silva and José "Geleião" (Big jelly) Márcio Felício.
Na kundi hilo lilianza kama timu ya mpira wa miguu katika gereza hilo, na waliamua kuliita PCC likiwa na maana Premier Commando de la Capitale au Party of Crime.
177a9e844a2776a64c8af57269260b97.jpg

Pia linajulikana kama 15:3:3, yani ukitazama mpangilio wa herufi za alfabeti "P" ni wa 15 wakati "C" iko namba 3 hivyo PCC ni 15:3:3.
Kundi hili lilikuwa na kusambaa magereza mengine ndani ya mji wa Sao Paul, ambapo kwa sasa inakadiliwa kuwa lina wanachama zaidi ya 13,000, na ni kati ya makundi ya kihalifu na yanayo ogopwa sana nchini Brazil.
Kundi hili linajihusisha na biashara za madawa ya kulevya, utekaji wa kudai malipo, mauaji ya kulipwa, kukusanya ushuru kutoka kwa makundi madogo yanayofanya biashara ya madawa ya kulevya Sao Paul ili wapate ulinzi kutoka kwa kundi hili dhidi ya wapinzani wao na mgao kutoka shughuli yoyote haramu itakayofanyika ndani ya Brazil.
Inasadikiwa kwamba, hakuna shughuli yoyote haramu iwe wizi, ujambazi, utekaji n.k inayoweza kufanyika bila PCC kuwa na taarifa ya shughuli hiyo na ni lazima wapate mgao hata kama hawakushiriki kwenye kutekeleza shughuli hiyo.

Mwaka 2006, mwezi wa saba, mamia ya wafungwa ambao walikuwa ni viongozi wa makundi ya kihalifu walikuwa wahamishwe kwa siri kutoka magereza mbalimbali ili wakawekwe kwenye gereza moja lijulikanalo kama Presidente Venceslau ambalo lina ulinzi mkali liliwa umbali wa kilometa 500 kutoka Sao Paul.
Kutokana na polisi wala rushwa, habari hiyo ilivujishwa kwa viongozi wa PCC.
PCC ilianzisha mapambano pamoja na mgomo kwenye magereza yote ya Sao Paul yaliyokuwa na wafungwa zaidi 150,000, pia walianzisha mashambulizi dhidi ya vituo vya polisi, uvamizi wa mabank, mahakama, maduka vituo vya mabasi kwa kutumia wanachama wake walioko nje ya magereza ambapo zaidi ya watu 150 waliuawa.
7459dfafb869e6c37fec34cb325ad5ae.jpg

Hii ilizidi kuishtua serikali ya Brazil juu ya nguvu na mtandao mkali ambao PCC imejijengea ndani ya jimbo la Sao Paul.
Kutokana na matukio haya polisi walishindwa kuwahamisha hap viongozi wa magenge na kauli mbiu ya PCC ya "One for all, all for one" ilizidi kupata umaarufu na vijana wengi wakapenda kujiunga na kundi hili la kiharifu linalojinasibu kuwa limeanzishwa kupinga uonevu wa mfumo wa polisi dhidi ya wafungwa.
Wanachama wa PCC upatikana kwa kupewa jukumu la kutimiza kazi flani hasa kuua, kuteka n.k na mwanachama mpya uwa anazidi panda ngazi za uongozi kutokana na kukamilisha majukumu anayopewa kwa weledi.
Mpaka sasa serikali ya Brazil inawatambua na kuwafahamu viongozi 1,500 wa PCC huku ilidai kundi hili lina zaidi ya wanachama 20,000
Ili mfungwa aweze kulindwa na hili kundi akiwa gerezani inabidi kulipia kiasi cha pesa ya Kitanzania 38,000 kwa mwezi huku wale waliomaliza muda wao, huutajika kulipia mchango wa kiasi cha pesa ya Kitanzania 1,334,000.
PCC uendesha pia uuzaji wa dawa za kulevya magerezani, mauaji ndani na nje ya magereza kwa malipo maalumu, pia ina miliki maafisa wengi wa polisi hasa polisi magereza ambao uwa inawalipa kwa ajili ya kutoa taarifa.
Kwa madai ya viongozi wa PCC uwa wao hawamuui mtu bila sababu, wanasema ni damu kwa damu ukiuawa basi umefanya kosa dhidi yao au dhidi ya mtu aliyewatuma wakuue.

**** Tukutane hapo baadae kwenye thread yangu itakayohusu tukio moja hatari lililokuwa na mkono wa PCC***
Aiseee!! Hatari sana tunashukuru kwa kutujuza! Mkuu.
 
Sijaisoma.

Vp imeisha au unaendeleza maana upo vzr kwa kutuachia alosto..
Hii imeisha hapo nilikuwa nawajuza ili nipate kuandika story flani inayolihusisha hili kundi nimeshaipost nasubiri moderator aiachie
 
Back
Top Bottom