Lijue kabila la "Karamojong" - Uganda

CHIWAMBO

Member
Jun 4, 2012
59
18
Historia
Karamojong ni miongoni mwa Makala yanayopatikana kusini mwa mkoa wa Karamoja nchini Uganda katika ukanda wa kaskazini mashariki karibu na Mrima Moroto, Kidepo valley national park na Manyatta. Ni kabila lililojaa utamaduni wa kila aina na ni kivutio kikubwa kwa wageni. Katika Makala mbalimbali za wataalamu wa mambo ya kale, Karamojong ni miongoni mwa makundi ya watu yenye asili ya Ethiopia na walikuja Afrika ya mashariki miaka ya 1600BK. Baada ya ujio wa kabila hili maarufu Afirka ya mashariki, waligawanyika katika makundi makubwa mawili yaani lile la Uganda liliitwa Karamojong na kundi lingine lilielekea Kenya ambao walijulikana kama Kelenjin na nguzo ya Maasai.

Waateker waligawanyika zaidi katika makundi kadhaa, wakiwa ni pamoja na Waturkana katika nchi ya Kenya, Wateso, Wadodoth au Wadodos, Wajie, Wakaramojong na Wakumam nchini Uganda, pia Wajiye na Watoposa kusini mwa Sudan: wote hawa wakijulikana kama "Kundi la Kiteso" au "Kundi la Karamojong".

Wakaramojong walikuwa wanajulikana awali kama Wajie. Jina Karamojong lilitokana na kauli "Ekar ngimojong", linamaanisha "watu wakongwe hawaweza kutembea zaidi". Kwa miaka mingi Wakaramojong au Wakarimojong ni kabila la watu wanaojihusisha na kilimo na ufugaji ambao ndiyo sehemu kuu ya utamaduni wao.

Lugha yao inajulikana kama Kikaramojong au Kikarimojong, na ni sehemu ya kundi la lugha za Kinilo-Sahara. Kabila hili kwa sasa lina watu wapatao 960,000 ambao nusu yao wana umri wa chini ya miaka 18. Kabila hili lina sifa ya kuhama hama kulingana na upatikanaji wa chakula cha mifugo. Hii ni kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa ya mara kwa mara au ukame.

Lugha
Katika lugha ya Kikaramojong, watu wa lugha hii hutumia viambishi awali ŋi- na na- mtawalia, ukosefu wa kiambishi awali huonyesha nchi au sehemu wanamoishi. Matawi yaliyotajwa hapo awali kutoka lugha zinazozungumza Kiateker yanaweza kuelewana kwa kiasi kikubwa au kidogo. Lugha ya Kilango nchini Uganda pia ina uhusiano wa kiasi fulani na lugha ya ŋiKarimojong, na hii inathibitishwa na majina yanayofanana miongoni mwa mambo mengine, ingawa wana njia fulani ya kuzungumza ambayo walikopa kutoka lugha ya Kiluo.

Utamaduni
Jambo usilolijua katika kabila Karamojong ni kwamba kabla kijana wa kiume hajapewa mke wa kuoa, anapaswa kupigana mieleka (Wrestle) na mwanamke anaye hitaji kumuoa. Endapo mwanaume huyo ataibuka kuwa mshindi katika pambano hilo, basi mwanaume huyo atatambulika kuwa ni mwanaume na atakabidhiwa mke huyo na kumuoa. Hii inamaanisha kuwa ana nguvu za kutosha kumlinda mke wake. Mwisho wa pambano la mieleka atapangiwa mahali ya kulipa na kukabidhiwa mke.

Na pale itapotokea mwanaume ameshindwa katika pambano hilo la mieleka, jamii hiyo itachukulia kuwa sio mwanaume mkamilifu na badala yake hatoruhusiwa kuoa katika kabila lake na hivyo kwenda kuoa makabila mengine ambako hawana mapambano ya mieleka kama yao ili kuoa.

Pia, hata kwa jamii ya makabira mengine yalipohitaji kuoa mwanamke wa kabila la Karamajong ilikuwa lazima apangiwe shindano la mieleka na mwanamke anayependa kumuoa.

Karamojong wanaamini kuwa ng’ombe ni utukufu na ni kipimo cha kuwa mwanaume. Wanaume wa kabila hili wanathaminika kwa idadi kubwa ya ng’ombe walio nao. Pia wapo tayari kufanya lolote ili mradi wapate marisho ya ngombe wao na maji.
Upatikanaji wa chakula na maji daima ni wa wasiwasi na ina athari kwenye mwingiliano wa kundi la Wakaramojong na makundi mengine ya kikabila.

Shughuli za uzalishaji
Shughuli kuu ya maisha ya Wakaramojong ni ufugaji, ambao una umuhimu wa kijamii na kitamaduni. Kulima mazao ni shughuli ya pili na huratibiwa tu katika maeneo ambayo yanaweza kulimwa.

Kutokana na hali ya hewa ya jangwa katika eneo hilo, Wakaramojong walikuwa daima wanajaribu njia tofauti za ufugaji kama vile kuwahamisha wanyama katika maeneo tofauti ambazo zina nyasi kwa ajili ya malisho, ambapo kwa muda wa miezi 3-4 kwa mwaka, wao walihamisha mifugo yao katika wilaya jirani kutafuta maji na malisho ya wanyama wao.

Dini
Watu wa kabila la Karamojong wana dini zao kama ilivyo kwa makabila mengine. Dini zao kuu ni dini ya kikristo au Kiislam na wanaendelea kutukuza mungu wa kale ajulikanaye kwa jina “Akuj”. Hivyo wanaamini kuwa “ng’ombe wote waliopo duniani na maeneo yao wamepewa na mungu wao AKUJ”. Hata hivyo, Imani hiyo inawezekana imepelekea migogoro na vita ya kimakabira na majirani zao ambao wanaimani kama yao. Aidha, katika kipindi cha utawala wa Idi Amin kabila hili lilijitwalia silaha nyingi sana hasa bunduki na kuongeza kasi ya mapigano dhidi ya makabira mengine katika eneo hilo. Hata hivyo, serikali ya Uganda kwa sasa imefanikiwa kuzipokonya silaha hizo ili kulinda Amani na utulivu wa eneo hilo.

Mgawanyo wa majukumu
Mgawanyo wa kazi katika kabila la Karamojong umegawanyika katika mfumo wa umri na upo katika makundi mawili yaani wanaume na wanawake. Wanaume utafuta marisho na maji ya ng’ombe, na kwa upande wa wanawake ujishughulisha na kazi za nyumbani ikiwemo malezi ya watoto pamoja na shughuli za kutafuta chakula. Maisha ya ufugaji kwao si ya kibiashara bali ni kujizolea umaarufu na sifa kemkem.

Maisha katika kabila hili ni ya kijamaa, wanashirikiana kwa pamoja katika matukio ya kijamii na kifamilia. Pia mwanaume wa kabira hili anaweza kumiliki wake wengi apendavyo kulingana na uwezo wake wa kulipa mahali. Kwa maana hiyo, suala la malipo ya mahali kwao ni kitu muhimu sana kabla ya kuodheshwa mke. Na malipo ya mahali hayo ulipwa kwa kutumia mifugo ya ng’ombe.

Migogoro
Wakaramojong wamekuwa wakihusika katika migogoro mbalimbali unaozingatia mazoezi ya wizi wa wanyama.

Wakaramojong daima wanahusika katika vita na majirani wao nchini Uganda, Sudan na Kenya kutokana na wizi wa mifugo wa mara kwa mara. Hii inaweza kutokana na imani za mila kuwa Wakaramojong wanamiliki wanyama wote kwa haki ya Mungu, lakini pia kwa sababu mifugo, hasa ng'ombe, ni muhimu katika mazungumzo ya kutoa mahari kwa ajili ya bibiharusi. Wanaume hutumia wizi wa mifugo kama haki ya kifungu na njia ya kuongeza mifugo yao ili kupata heshima.

Kwanini utembelee Karamojong?
Kutembelea kabila la Karamojong ni darasa tosha. Ni kabira lenye utajiri mkubwa wa kiutamaduni katika vijiji vyao wa enzi na enzi. Ukarimu wa watu wake, mpangilio wa makazi, michezo ya asili (kuimba na kuruka), lugha inayotamkwa vyote vinaashiria ni kwa namna gani jamii hiyo inaishi kwa kutegemeana na umoja wa hali ya juu.

Imeandikwa na
Ausi Chiwambo
chiwambo@hotmail.com
 
Picha za watu (wanawake, wanaume, vijana like,kiume, nyumba) nk hauna?
 
Back
Top Bottom