Lijue Kabila halisi la Edward Lowassa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lijue Kabila halisi la Edward Lowassa

Discussion in 'Celebrities Forum' started by mmaroroi, Mar 18, 2009.

 1. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #1
  Mar 18, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  WAZEE WA KIMASAI WAMJADILI LOWASSA risasi mchanganyiko


  Aidha, wazee hao wapatao 90 wamejadili pia kuhusu mkanganyiko uliopo ambao baadhi ya watu humchukulia waziri mkuu huyo aliyejiuzulu kuwa ni kutoka kabila la Kimasai wakati wao wanamfahamu kuwa ni Mmeru.Akizungumza na mwandishi wetu kwa simu kutoka kijiji cha Luburuko, Arumeru Mashariki mkoani Arusha mwanzoni mwa wiki hii, Katibu wa Mila za Kimasai, Amos Mollel alisema kuwa kikao hicho kilikaa Machi 8, mwaka huu.Mollel alisema kuwa, walilazimika kuitisha kikao cha wazee kutoka maeneo mbalimbali mkoani humo kufuatia watu wengi kusema kuwa tuhuma zilizomfanya Lowassa ajiuzulu uwaziri mkuu ni kubwa na ni kitendo cha aibu ambacho Mmasai hawezi kufanya.Aliendelea kusema kuwa kikao chao kilifikia uamuzi wa kuwaomba wananchi waelewe kuwa Lowassa si Mmasai, kwani kufanya hivyo ni kuwachokoza watu wa kabila hilo.“Unajua mwandishi, madai yanayoelekezwa kwa Lowassa kuhusu ufisadi uliofanywa kupitia kampuni hewa ya kuzalisha umeme ya Richmond ni kitendo cha aibu kubwa kwa jamii.“Hivyo, tulikaa ili kujisafisha kwakuwa wengi wanajua kuwa ni Mmasai mwenzetu kumbe ni Mmeru,” alisema Mollel.Lowassa alijiuzulu hivi karibuni kwa kuhusishwa na sakata la Kampuni hewa ya Richmond ambayo hadi sasa inalipwa shilingi milioni 152 kwa mwezi.Mawaziri wengine waliojiuzulu kufuatia kashfa hiyo ni pamoja na waliowahi kuwa mawaziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi na Ibrahim Msabaha.
   
 2. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #2
  Mar 18, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ...Thanx for this...Tatizo sio kabila, tatizo wizi alofanya huyo bwana.Kwani akiwa Mmeru maana yake wameru ndio watu wa kupakwa matope kuwa ni majambawazi???
   
 3. B

  BeNoir Member

  #3
  Mar 18, 2009
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Walikuwa wapi kutoa tamko hilo siku zote hizi au ni kwa vile madaraka yamemtoka?
   
 4. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #4
  Mar 18, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Aliwagilibu tuu kwa utajiri wake lakini ukweli ni huo,pia usisahau usemi wa Baba wa taifa kwamba mwanasiasa akifilisika kisiasa hutafuta namna yoyote ya kutafuta umaarufu.
   
 5. Gelange Vidunda

  Gelange Vidunda JF-Expert Member

  #5
  Mar 19, 2009
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 312
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  So what if he is originally a Meru? Some pipo bwana!!!!
   
 6. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #6
  Mar 19, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Ni vyema ukaandika na tarehe ya habari hii kwani nachelea kusema Lowasa alijiuzulu hivi karibuni. Halafu swali la kizushi HADITHI YAKO INATUFUNDISHA NINI?
   
 7. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #7
  Mar 19, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Either - Mmeru or Mmasai - the difference is very same!
   
 8. Lusajo

  Lusajo JF-Expert Member

  #8
  Mar 19, 2009
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 451
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mhmm!! karibu na 2010 people kampeni karibu zitaanza. labda wanamuandaa Mmasai mwenzao huwezi kujua. Anyways ni mawazo yangu tuu.
   
 9. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #9
  Mar 19, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Washaanza kubaguana kikabila? Mbona tunaelekea kubaya
   
 10. kimatire

  kimatire JF-Expert Member

  #10
  Mar 19, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 365
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Huo ndio ukweli kabisa kwani Lowasa alitumia umaarufu wa kabila la kimasai kuingia madarakani,Pia mtakumbuka siku ile aliporejea nyumbani baada ya kashfa hiyo zilitumika mbinu hizo hizo kuwahadaa wamasai kumpokea kwa kuchinjiwa ng'ombe kibao.Kwani nani asiyejua wamasai kwa kitoweo cha beef utawatega hata kuwamaliza??
  Wazazi wake wote Edward Ngoyaiya Lowasaa wanatoka Arumeru (Ni WAMERU na asili yao ni wachagga wamachame huko mkoani Kilimanjaro-Japo yeye mwenyewe EL alikuwa na chuki kali sana na wachagga kwa kinywa chake alitamka hadharani) na kwamba wanapakana na wamasai,Ndiyo maana Lowasaa aliweza kuongea kimasai cha kubabaisha.Hata alipoona apate political influence ya record nzuri aliyoweka marehemu Edward Moringe Sokoine ndipo alipojitosa kuhamia na kuishi Monduli kuusaka umahiri wa marehemu kwa kujitia yeye ndiye atawakomboa wamasai.Kuna tofauti kubwa sana kati ya Wameru na Wamasai.Sikuwa na nia ya kujadili ukabila kwa siasa za Tanzania lakini ukweli ndiyo huo.Ukiitwa mmasai una sifa zaidi za ushujaa na uadilifu.Hizo ndizo alitumia EL kujipatia umaarufu wa kisiasa.Sasa walichokifanya hao wazee wa kimasai ni sahihi kabisa kudumisha mila na desturi zao,pia kujisafisha na ufisadi wa EL.Kisha kumuuondoa kabisa katika uwanja wa sia sa kwani ni mbabaishaji na fisadi mwenye uchu na hila za kuingia ikulu hata kwa mlango wa baharini.LOWASAA KWELI SIYO MMASAI
   
 11. Makaayamawe

  Makaayamawe JF-Expert Member

  #11
  Mar 19, 2009
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hivi kwani kuwa Mmasai ni sifa? Wilaya ya Meru ina Wameru na Wamasai pia (Waarusha). Kwa hiyo yeye kutokea Meru kijiografia hakumfanyi asiwe Mmasai kwani hata Chalinze kuna Wamasai wake.

  Huyu EL ana dhambi nyingi sana za kumhukumu nazo, lakini haya ya ukabila ni muelekeo mbaya maana wapo Wabunge wengi wanaowakilisha majimbo waliyohamia tu na kuishi kwa muda. Tuachane na mambo ya ukabila.
   
 12. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #12
  Mar 19, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Sawa tumekuelewa kwamba si mmasai sasa tufanye nini?
   
 13. Kandambilimbili

  Kandambilimbili R I P

  #13
  Mar 19, 2009
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 782
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  SIPATI picha hapa Lowassa alienda Monduli kama Massai au alienda kwenye jimbo analoliwakilisha Bungeni? tukipata jibu hilo twaweza kulonga vizuri,
  ukiachilia kuwa wakati akiwa PM hao hao walimkumbatia kama NEMBO YAO.
   
 14. kimatire

  kimatire JF-Expert Member

  #14
  Mar 19, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 365
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Kwamba ameporomoka kisiasa hata kule alikokuwa akiungwa mkono wamemstukia ndiyo maana wanahoji kuingia kwake katika Jimbo la Monduli kama mzawa ili apate kura za wananchi.Si hilo tuu kwamba muda wote ameuhadaa umma wa Watanzania kwamba yeye ni mmasai ili tuone kwamba anafuata nyayo za marehemu Sokoine kumbe sivyo!!Yeye ni fisadi aliyejivisha ngozi ya watawala wengine.Ndo maana dhana ya ukabila ikawa imeingia na si vinginevyo,Kwani wapiga kura wake ndiyo wanahoji kabila lake na wala siyo Wana JF.
   
 15. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #15
  Mar 19, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Si ubaguzi wa kikabila bali ni kuweka sawa historia iliyowekwa na Sokoine kuwa Wamasai ni waadilifu hala Lowassa ajilimbikizie mali kwa kujiita masai mchunga ng'ombe ni wizi mtupu.Ninavyowafahamu wamasai hawana tamaa ya mali na ni waadilifu katika utendaji.
   
 16. ibrasule

  ibrasule Member

  #16
  Mar 19, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo ni patamu sana, sizani kama EL angekuwepo madarakani issue hii ingerise up? Ukweli unabakia palepale kuwa EL ni mmeru lakini kwakuwa alikuwa anawasidia wamasai insingekuwa rahisi issue hiyo kuwa discussed. lakini wanatakiwa kuwa waangalifu sana na mazungumzo yao maana si mtu wa mchezo anaweza kurudi madarakani tena ikwa shida.
   
 17. A

  Audax JF-Expert Member

  #17
  Mar 19, 2009
  Joined: Mar 4, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ni mwizi tu!!!
   
 18. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #18
  Mar 19, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Wakina OLE ------- mliopewa vyeo na Lowassa mpo hapo?
   
 19. M

  Mkora JF-Expert Member

  #19
  Mar 19, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 360
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mkuu nadhani itabidi arudishwe kwao Kenya kama walivyomfanya Jenerali Ulimwengu
  Itabidi aishi kwa kibali Umasaini
   
 20. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #20
  Mar 19, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,562
  Likes Received: 18,294
  Trophy Points: 280
  Ni kweli Lowasa ni Mmeru, ila mnamsingizia hayo mengine yote. Ukweli ni kuwa Baba yake Lowasa alikuwa Akida utawala wa Mwingereza kazi yake ikiwa ni kukusanya kodi ya kichwa na kuwapa waingereza.
  Wameru walifika mahali wakagoma kuilipa kodi hiyo, Baba Lowasa akawaripoti kwa Bwana DC wakapata kibano, ndipo wakatishia maisha yake na familia yake, ili kuisalimisha familia, Baba mtu ndio akauza shamba na kuhamia Monduli kimoja.
  Eduwadi amezaliwa Monduli, amekulia Monduli na amefanyiwa mila za Kimasai.

  Hii ni kampeni chafu dhidi yake kuelekea 2010. Tena kosa lake sio Richimondi, kosa lake ni kuwadharau Maleigwanan walipotaka kusuluhisa mgogoro wa Ole Sendeka na yule dogo wa UVCCM. Maleigwanan walishauri maadam wote ni Wamasai, watayamaliza kimila.
  lowasa akamshinikiza dogo asikubali bali aende mahakamani-ili ammalize Ole Sendeka.
  Bahati mbaya sasa huo ndio mwanzo wa mwisho wa Lowasa, hswa ukizingatia Ole Mangi amemwaga faranga na kuwachinjia ng'ombe mpaka Malaibon wamepagawa na kumtosa Lowasa.
   
Loading...