Lijuakali: Ndege moja tayari hairuki ni mbovu sababu ya one man show

  • Akihojiwa na blog ya muuñgwana kuhusu hali nzima ya makinikia na hatua alizochukua rais kuongea na wezi ikiwa ni tofauti na wezi wengine wanaopigwa mawe na kufungwa.
Azidi kushangaa kumpongeza rais kwa kazi aliyoanza badala ya kusubili amalize kazi na kusema alitarajia aseme flani na flani wahojiwe juu ya mikataba huu ni kudhihirisha hii muvi ndo efika mwisho.

Na kaenda mbali zaidi na kusema rais alipata wapi mamlaka ya kuchukua fedha na kununua ndege kinyume na sheria? Je ccm walio wengi wana haki ya kuhoji matumizi hayo yalio nje na mpango wa bunge?

Je unajua moja ya ndege hizo ni mbovu na imepaki haifanyi kazi? Na tulisema kanunua mitumba?
Hivi kila akigusa huwa ni kibovu ana nini?
 
lol aende nigeria akasafishwe nyota maana hamna hata moja anafanya linaeleweka, kadanganya wananchi bei halali za ndege kumbe ma ndege yenyewe mabovu
NB: Na hata ikitokea siku zikafanikiwa kuruka yani mtu atakayeipanda atakuwa kachoka kuishi kwa kweli
 
Huyo Mbunge pumbavu sana, hata binadamu akizaliwa leo anaweza kuugua baada ya siku kadhaa sembuse ndege?

Hivi hawa wapinzani wa Tanzania wana matatizo gani kwenye ubongo?

kwani tangazo la ATCL kuhusu hii ndege hawakulisoma au? Mbona gari yake huwa anaipeleka service kila wakati why ndege?

Mkuu;
Ukipunguza hasira itakusaidia. Angalia, wataalam wanasema atii, hasira hufanya damu ikapotesa mwendo au mtiririko wake. Hoja ya huyu mbunge ni kuwa; Hata USA nchi tunayoona kuwa ni tajiri sana, HUKOPA ndege. Hawalipi Cash.

Sio kwamba hawana pesa bali ili yakitokea ya kutokea, usilie kilio cha mbwa kidomo juu. Kwa hela tuliyotoa, ingelikuwa malipo kidogo na mkopo tungeliweza nunua zile ndege zao zote zilizokuwa kule stoo yao. Sasa leo, tumechukua hapo baadhi tu, nazo kumbe mbovu! Sijui zilikaa mno bila hata kuwasha injini zake.

Anaenda mbali na kusema; Hata miezi 8 tangu ianze kazi bado, tiyari isha wekwa kando. Wadhani ni hasara kidogo hiyo?? Sio kwamba anadharau hiyo ndege.

Swali tu la kizushi. Je hawakupewa gerentiii?? Jamani, nilinunua jenereta Tshs 780.000/= nikapewa gerentii mwaka mmoja sembuse ndege? Tujichunguze, ni nani ametuloga?? Tunashabikia hata sumu!!
 
Wewe ndo mpumbavu hujui usemalo! Kimsingi manunuzi yanatakiwa yawe wazi kwa bunge na si rais kujichukulia maamuzi bila kushirikisha bunge wewe huoni kama kuna maamuzi Rais hufanya kibabe bila ushauri wa wote!! TAKE TIME TO THINK IT IS A SOURCE OF POWER!.

Huna akili wewe Kaa KIMYA Kabisa, kasome sheria ya za fedha vizuri punguani wewe ndo uje na hayo maneno ya kushikishwa na vibunge vyenu uchwara hivo.

Kwa kukusaidia, Rais anayo mamlaka ya kuamrisha fedha fulani iende ikafanye kazi fulani sehemu fulani ila kuna sharti kwamba, katika mkutano wa bunge unaofuata au utakaokaa Serikali ilijulishe Bunge kwa maandishi kuhusu hatua hiyo...

Jamani, muwe mnasoma, msikubali kubeba maneno ya wanasiasa wenu wa vyama vyenu na kuyashikia bango, hao wanasiasa wenu huwa wanaongea maneno machache sana ambayo wanajua kuw mkiyasikia watawachanganya sana na mtaendelea kuwazungumza, huwa hawanukuu taarifa yote.

so, dawa hapa ni ninyi kuingia chimbo, upo hapo?
 
Acha kupotosha umma
Si vyema kusema mambo usiyekuwa na uhakika nayo
Air Tanzania kwa sasa wana ndege 3
Iliyoaribika kwa sasa ni ile ndege ya zamani
Sio zile Bombidier 2 zilizo nunuliwa na serikali ya mh Magufuli
Unajua njia ya muongo huwa ni 'PUFI'

Juzi juzi tu humu humu jukwaani mada hii imezungumwa, na kuna mtu akajitia mkurugenzi kutolea ufafanuzi. Naweka hapa chini kipande cha maelezo yake kwa italics:

(Kwa wale waliofuatilia ujio wa ndege hizi wakati zinaletwa Tanzania,watakumbuka kuwa ndege moja ilitangulia kabla ya nyingine,iliyotangulia ni ile iliyokuja na namba za usajili za Canada za C-FHNF ambapo ilipofika Tanzania ikapewa namba ya 5H-TCB.

Hii 5H-TCB ndio ilianza kufanya kazi mbele ya ile ya pili yenye usajili wa 5H-TCD.Kwa hiyo hata kwa masaa ya kukaa hewani,hii iliyotangulia ya 5H-TCB ndiyo yenye masaa mengi hewani kuliko 5H-TCD iliyokuja baadae na kuanza kufanya kazi.

Ndege iliyoegeshwa kwa muda kwa ajili ya matengenezo madogo ni 5H-TCB,na hii si Tanzania tu,bali dunia nzima.Ndege inapofikisha masaa kadhaa kuwa hewani,let say masaa 12000 hewani,inatakiwa kuwa grounded ili kuweza kubadilishiwa vifaa kadhaa ambavyo masaa yake yanakuwa yamekwisha kwa vyenyewe kutimika.)

Rejea hii thread: Ukweli kuhusu Ndege ya Air Tanzania "kuegeshwa" bila kuruka
https://www.jamiiforums.com/threads...hwa-bila-kuruka.1266560/page-14#post-21617655
Hii inadhihirisha kuwa kuna kamati za kusema uongo zisizo na weledi na kumbukumbu. Sijui sasa tuelewe nini!
 
ifikie wakati wapinzani wetu wafanye mambo kwa kutumia ufahamu wao si kila jambo ni kuropoka tu.....ye aende atcl aulize atapewa jibu...ina maana ndege zisifanyiwe service kweli........mbona wamepigwa billion 7 na mwenyekiti hawalalamiki au ndo hasira wanazihamishia serikalini
 
Acha kupotosha umma
Si vyema kusema mambo usiyekuwa na uhakika nayo
Air Tanzania kwa sasa wana ndege 3
Iliyoaribika kwa sasa ni ile ndege ya zamani
Sio zile Bombidier 2 zilizo nunuliwa na serikali ya mh Magufuli
Mkuu una uhakika na unacho kisema? Kabla ya kutuhumu watu wanapotosha hakikisha uko sahihi.. bombardier ndio ipo kwenye matengenezo
 
Atafukuzwa Bungeni ili ashughulikiewe!. Yeye anahoji kama nani? Kazi yake ni kutombea tu na kuonyesha uzalendo wakati tunatafuta fwedhaaaa!. Habari za fwedhaaa hizo zinafanya nini kwa ajili ya anani sijui nani kashiriki kununua nini HAYAMUSU. Kutuhoji ni kutujaribu!. Akifukuzwa bungeni sisi huku tutamshughulikia bila huruma kabisa!. Hatuajiribiwi sisi!.

Na kaiendeleea tutawaambia wajumbe wetu kule wamfukuze akione cha moto!. Hawa watu hawaaminiki. Wanaaminika tu katika kutuombea, lakini masuala mengine ya maendeleo ni "ADUI".!. Siyo wenzetu hwa wanaohojoi hoji mitindo yetu!
Duh! hata kama maana na muktadha si kama ulivyoandika hapo kwenye red, ni vizuri uhariri tu hilo neno likae vizuri!
 
, hata binadamu akizaliwa leo anaweza kuugua baada ya siku kadhaa sembuse ndege?

kwani tangazo la ATCL kuhusu hii ndege hawakulisoma au? Mbona gari yake huwa anaipeleka service kila wakati why ndege?


Ukimya wako ungekusaidia kuficha upumbavu wako, unatoa tu maneno ya kanga sababu imetajwa CCM?

Ungekuwa Mtanzania kwanza ungejaribu kufikiri kabla ya kuongea lakini ushabiki wa siasa za CCM umekufanya kuwa punguwani.

Ni afadhali nchi ingekuwa na sungura wengi tungekula nyama na kufanya biashara ya ngozi kuliko kuwa na mizoga ya watu wasio wataifa na uwezo mdogo wa kufikiri.
 
Mbona Kawaida chombo cha moto Kupata technical/mechanical problem

Yeye amejuaje kuwa ni Mbovu!
Mali mpya huwa inapewa guaranteee ya kufidiwa au kutengeneza,sasa hii mpya ya mabilioni mbona walioitengeneza hawaji kuikarabati?
 
Kwanini upinzani mnaona kila jambo ni kupinga tu? Why harbor such vitriol and negativity? Kwani ndege kuharibika ni kitu cha ajabu? Chombo chochote huharibika na kutengenezwa. Mnapopinga kila kitu ili mradi tu mmepinga mnatusikitisha hata sie ambao huwa kuna wakati tuna-support hoja zenu. Wekeni u-Taifa mbele na sio kupinga kila kitu Mheshimiwa Rais anachofanya. Kuna mambo ambayo wengi hatumuungi mkono lakini kumtafuta uchawi kwa kila jambo si busara. Hii nchi ni yetu wote. Let us all play our parts to be proactive and constructive even in our criticism. Badilikeni.
Cha kushangaza na kusikitisha zaidi mkuu, ni kwamba iliyoharibika sio kati ya zile Bombadia za JPM....ni ndege ya zamani. Na jana imetolewa ufafanuzi vizuri sana na Mkurugenzi wa ATCL.
Najiuliza hawa watu akiwemo huyu Lijualikali wanapata faida gani kumwaga sumu na chuki aina hii kwa Watanzania!?
 
kwani wapinzani kuna kitu gani washawahi kuisifia serikali....wao sababu ni wapinzani wanajua kila kitu ni kupinga tu...anyway hatukatai kuikosoa serikali pale inapobidi....

Mkuu kwani ccm huwa wanakubali kipi cha wapinzani? Mambo mengi ya wapinzani waliyosema kuhusu raslimali za nchi, ccm walipinga kwa nguvu zote leo hii wanaumbuka. Elimu bure walipinga leo hii wanatekeleza kwa tai shingoni. Ni hivi katika nchi hii mambo yote yanaamuliwa kwa mtazamo wa kisiasa. Wazo kabla ya kufanyiwa kazi linaangaliwa linatoka wapi. Baada ya hapo huungwa ama kupingwa kiitikadi bila kujali faida au hasara katika nchi.
 
naona ikipona route yake iwe ni dar to chato! Tuwaone Hao wafitini watakuja na nini tena
 
toka ile juzi magu awakingie wastaafu kifua sina imani naye kamwe. iko mikataba inafanywa sasa kimyakimya huko mbele atageukwa na wanaccm wenzake na kusemwa vibaya. muda utasemwa.
 
Back
Top Bottom