Ligi zimesimama, vipi bei ya vifurushi zinaweza kushushwa?

nyumbamungu

JF-Expert Member
Mar 3, 2017
996
826
Kwasasa ligi karibu zote zimesimama nauliza upo uwezekano wa kushushwa bei ya vifurushi vya ving'amuzi? Tukumbuke kampuni (DStv, StarTimes na Azam Tv) zimeshalipa haki za matangazo "TV Rights "?
 
Kama mafuta yameshuka bei kwenye soko la dunia, na bado bei ya mafuta iko juu nchini, kwanini vifurushi vishushe?
Ukijua sababu ya mafuta kutoshuka bei, utajua kwanini vifurushi pia haviwezi kushuka bei.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwasasa ligi karibu zote zimesimama nauliza upo uwezekano wa kushushwa bei ya vifurushi vya ving'amuzi? Tukumbuke kampuni (DStv, StarTimes na Azam Tv) zimeshalipa haki za matangazo "TV Rights "?
Tegemea kupanda, si kushuka. Mapato yao yatashuka kwani tupo ambao hatulipii vifurushi baada ya ligi kusimama, japo sikubaliani nao kwani wanatuibia sana. Ukiwa peke yako na ukaangalia tv siku 2 kisha ukasafiri mwezi, ukirudi utakutana na tangazo la kifurushi chako kwisha. Tulipie mb na siku. TCRA wasaidie kwa hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama mafuta yameshuka bei kwenye soko la dunia, na bado bei ya mafuta iko juu nchini, kwanini vifurushi vishushe?
Ukijua sababu ya mafuta kutoshuka bei, utajua kwanini vifurushi pia haviwezi kushuka bei.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna mapato serikali inajikosesha kwa kupandisha kodi bila mahesabu. Nina shindwa kujua kama wapanga Kodi Wana abc za uchumi. Bei kubwa ya mafuta inawafanya watu wa kipato kidogo kutelekeza magari majumbani. Matokeo ni battery za magari kwisha nguvu kwa kusimama muda mrefu, na usiku wezi na vibaka kuyanyemelea kwani wanajua tayari alarm hazifayikazi. Kodi nchi hii ziko juu na ndio chanzo cha rushwa TRA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom