Manji Phinias
Member
- Oct 13, 2019
- 21
- 15
Andaeni Panya wenuDROO ya mashindano ya kimataifa, kombe la shirikisho na Ligi ya mabingwa Afrika imefanyika mchana wa leo huko nchini Misri na wawakilishi wawili wa Tanzania katika mashindano hayo wametambua wapinzani wao.
Simba ambao wapo katika Ligi ya mabingwa Afrika wamepangwa kundi (A), tena na Waarabu wa Misri Al Ahly ambao walikuwa nao katika kundi misimu miwili iliyopita katika mashindano hayo na wote wakasonga katika katua ya robo fainali.
View attachment 1671905
Kundi hilo la A, ukiachana na Al Ahly wawakilishi hao wa Tanzania wamepangwa na nyingine mbili, AS Vita ambao nao walikuwa kundi moja misimu miwili iliyopita na Simba walifuzu hatua ya makundi baada ya kuwafunga mchezo wa mwisho mabao 2-1, katika uwanja wa Benjamin Mkapa (Taifa).
Timu nyingine ambayo ipo katika kundi hilo la Simba ni miamba ya soka la Sudan El Marreikh.
View attachment 1671909
Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi Simba, Mulamu Ng'ambi amesema si kundi lao bali mengine yote ni magumu lakini kwa namna ambavyo anauzoefu wa mashindano hayo anaona wananafasi kubwa ya kwenda katika hatua ya robo fainali pamoja na Al Ahly kama ilivyokuwa mwaka juzi.
"Kundi ni gumu lakini kuwepo na Al Ahly pamoja na AS Vital ambao tunawafahamu naona nafasi kubwa ya kusonga mbele tunayo kuhusu EL Marreikh si timu ya kuibeza lakini rekodi zinaonyesha hatujawahi kupoteza mchezo wowote nchini kwao," amesema Ng'ambi.
Ukiachana na mchezo huo wawakilishi wengine kutoka Tanzania katika kombe la Shirikisho Afrika Namungo katika hatua ya tatu wamepangwa kucheza na DE Agosto kutokea Angola.
Katika hatua hiyo Namungo wataanzia ugenini kabla ya kuja kukamilisha hatua hiyo kwa kucheza mechi ya marudiano nyumbani hapa Tanzania na kufahamu kuwa watakuwa wamesonga mbele hatua ya makundi au wameishia hapo.