Ligi ya Europa: Manchester United uso kwa uso na Real sociedad, Arsenal kumenyana na Benfica

Shadida Salum

Journalist at JamiiForums
Sep 11, 2020
69
104
20210225_181226.jpg
Takwimu zinaonesha Manchester United imeshinda mechi moja tu kati ya tisa za nyumbani walizocheza dhidi ya timu za Uhispania, wakishindwa kufunga katika mechi mbili.

Mechi moja waliyoshinda ilikuwa dhidi ya Real Sociedad katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa ya Ulaya msimu wa 2013-14

Kwa upande wa Real sociedad haijawahi kupata ushindi katika mechi zao tatu dhidi ya Manchester United kwenye mashindano yote.

Aidha, Manchester United haijafungwa katika michezo 14 ya UEFA Europa ikiwa Old Trafford tangu ilipopoteza 3-2 dhidi ya Athletic Bilbao msimu wa 2011-12.

Kwingineko Arsenal itakuwa nyumbani kukipiga dhidi ya Benfica. Mchezo wa mwisho wa Benfica wa ugenini dhidi ya Arsenal katika mashindano ya Ulaya ilishinda na ilikuwa msimu wa 1991-92.

Michezo mingine itakayopigwa hii leo ni kati ya Ajax dhidi ya Lille, Napoli dhidi ya Granada huku Leicester city ikikipiga dhidi ya Slavia Praha, Hoffenheim dhidi ya Molde, Rangers itaumana na Antwerp, Shakhtar Donetsk ataumana na M. Tel-Aviv , Villarreal dhidi ya RB Salzburg, Milan dhidi ya Crvena zvezda na Clab Brugge dhidi ya Dynamo kyiv.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom