Ligi Kuu Tanzania Bara: Wachezaji 5 kubadilishwa katika mchezo mmoja. Usajili kuanza Agosti Mosi

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Shirikisho la Soka Nchini (TFF) limezingatia maelekezo ya FIFA katika kukabiliana na changamoto za #COVID19 ambapo katika mchezo mmoja timu itaruhusiwa kubadili hadi Wachezaji watano badala ya watatu

Limesema marekebisho hayo yamefanyika katika Kanuni ya 14 (25) ya Ligi Kuu, Kanuni ya 14 (25) ya Ligi Daraja la Kwanza, Kanuni ya 14 (24) ya Ligi Daraja la Pili, Kanuni ya 17 (24) ya Ligi Kuu ya Wanawake na Kanuni ya 13 (24) ya Ligi ya Mabingwa ya Mikoa

Aidha, TFF imefanya marekebisho ya Kanuni kuhusu usajili, hivyo msimu wa mashindano wa TFF wa 2019/20 sasa utamalizika Julai 31, 2020 badala ya Mei 31, 2020 kama ilivyokuwa awali

Kutokana na mabadiliko hayo, TFF imewataka Wachezaji waliokuwa wamalize mikataba yao Mei 31, 2020 waendelee kuzitumikia klabu zao mpaka Julai 31, 2020 ambapo ndio itakuwa mwisho wa msimu

Dirisha la usajili kwa msimu wa 2020/21 litafunguliwa Agosti 1, 2020 na kufungwa Agosti 30, 2020

EaUERrZWkAAkw-z.png
 
Back
Top Bottom