Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) | Mzunguko wa 8: Young Africans SC Vs Simba SC, Washindwa kutambiana. 28 Oktoba 2017


Kunguru Mjanja

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2012
Messages
1,972
Likes
3,214
Points
280
Kunguru Mjanja

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Joined Aug 22, 2012
1,972 3,214 280
Habari Wakuu!

Leo ndio ile siku ambapo watani wa jadi wa muda mrefu wa ligi kuu ya Tanzania bara (Vodacom Primier League), Simba SC na Yanga SC wanakutana.

simba-yanga-jpg.619038

Tiketi za mchezo wa Yanga SC na Simba SC Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara zinaendelea kuuzwa Uwanjani.
  • VIP - Tsh. 20,000/=
  • Mzunguko - Tsh. 10,000/=

UPDATES
Vikosi vya leo;

Kikosi cha Yanga;
1. Rostand 2. Abdul 3. G Michael 4. Vicent 5. Yondani 6. Tshishimbi 7. Buswita 8. Loth 9. Mwashiuya 10. Chirwa 11. Ajibu

Sub za Yanga SC: Benno Kakolanya, Hassan Kessy, Mwinyi, Nadir, Pato, Mhilu, Emanuel Martine.

Kikosi cha Simba;
1. Manula 2. Nyoni 3. Mo Hussein 4. Murushid 5. Mwanjale 6. Kotei 7. Yassin 8. Niyonzima 9. Kichuya 10. Mavugo 11. Okwi

Sub za Simba SC; Emmanuel Mseja, Ally Shomary, Ndemla, Bocco, Mkude, Kazimoto, Nicholas Gyan.
===============================================

Yanayojiri;

>Ripoti zinasema Kiungo wa Yanga Thabaan Kamusoko hatokuwepo kwenye mchezo wa leo Yanga vs Simba akiendelea kutibiwa majeraha

>Vikosi vipo uwanjani vinapasha misuli kabla ya kuanza kwa mtanange kuanza pale majira ya saa kumi za jioni

> Vikosi vimeingia kwenye vyumba vya kubadili nguo kujiandaa na mechi ya leo

> Mashabiki bado wana moto uwanjani hapa, si wa Simba si wa Yanga wote wanaimba na kucheza

> Vikosi ndio ndo zinaingia uwanjani hapa

> Yanga SC wapo na jezi zao za kijani huku Simba wakiwa na Jezi zao za rangi nyeupe kwa mashati na Kaptura nyekundu
=================================================

full-png.619275

01' Simba ndio wameanza mpira kati hapa,
01' Kichuya anampa mpira Mavugo , Mavugo anapiga shuti mtoto na linatoka nje

02' Mpira bado unazunguka katikati ya uwanja hapa naona, Simba wanapiga pasi fupi fupi

05' Nyoni kafanya kazi nzuri pembeni huku upande wa kulia amemfinya beki wa Yanga (juma Abdul) lakini anaikiza kross sio nzuri ya kimo cha mbuzi na kipa anaudaka mpira

06' Yanga nao wanajibu, lakini pasi nzuri ya mwisho, Ajibu anakuwa ameotea ikiwa ni offside ya kwanza ya mchezo

10' Nyoni na Kichuya wanawekuana vizuri huku chini kulia mwa lango la Yanga, Nyoni napiga krosi lakini inakuwa kubwa na kumkuta Okwi upande wa pili hakuna maradha yoyote

12' Ajubu na Juma Addul wanpiga faulo nje kidogo ya box la 18 la Simba upande wa kulia wa goli, wanapiga faoulo mbaya na kumbabatiza kwenye ukuta mdogo

14' Kichuya anaachwa mwenyewe sana anamtengea Nyoni anaingiza kross na wanapata kona

15' Kona fupi inapigwa pale ambapo Nyoni na Kichuya wanapadilishana pasi mbili tatu na Nyoni kuingiza kross kubwa ambayo ni goal kick kwa Yanga

18' Okwi na Niyonzima wanagongeana vizuri lakini Yanga wako makini wanatoa na kuwa kona ya pili ya Simba, inachongwa lakini ni goal kick

21' Kichuya anachezewa faulo katokati ya uwanja hapa

22' Nyoni leo naona anapata wakati mzuri upande wa kulia huku anageuza tu. ALienda na kumgongea Okwi aliyemtafuta Kichuya, Kichuya kamtengea Nyonin na akaingiza kross nzuri kumtafuta Okwi aliyepiga kichwa sio cha juu sana ila ni goal kick

23' Yanga wamejibu mashambulizi, shambulizi kali wanafanya Yanga, shuti kali Mwashiuya, Manula anautema, Tshishimbi naye anaachia mkwaju mali hapa, goal kick

24' Yanga wanafanya shambulizi jingine zuri, Manula anaokoa inakuwa kona ya kwanza ya Yanga. Inachongwa na Mwashiuya na kuokolewa na Niyonzima kuchezewa faulo

27' Mavugo anajaribu shuti la chinichini pale ila ni goal kick kwa Yanga

29' Kila mmoja hapa anacheza kwa tahadhari sana kuogopa kuanza kufungwa wao.

30' wanapata Faulo Yanga, Shishhimbi anatengewa anachia mkwaju wa hatari ila manula anacheza na kuwa kona. Mkwaju hatari sana ule

31' Chirwa alikata upepo upande wa juu wa uwanja kule na kuingia ndani ya box la Simba, apiga krossi nzuri lakini hakuna mtu wa kujaza kimiani pale

33' Ajibu anampiga mtu chenga ya mwili ila beki mwingine anakuja kunyang'anya Ajibu mpira katika harakati za kuwania mpira Ajibu anafanya faulo

37' Ajibu anamtengea Raphael na kugongeana vizuri, Ajibu anageuka vizuri lakini anatoa pasi mkaa nje ya 18 ya Simba

41' Bado mpira unachezwa sana maeneo ya katikati ya uwanja hapa

42' Aliondoka vizuri Niyonzima akamimiza krosi iliyomkuta Mavugo akamtengea Okwi nadani ya 18 ya Yanga ila Okwi anashindwa kumiliki mpira iue. Yanga wanaondosha

45' Dakika moja ya nyongeza inaonyeshwa na muamuzi hapa

45+1' Half Time
Si Yanga wala Simba walioweza kuona lango la mwenzake. Timu zinarudi kwenye vyumba vya kubadili nguo

MPIRA NI MAPUMZUKO


> Timu ndio zinarudi uwanjani hapa kuendelea na mtangane. Kipindi cha kwanza timu zilicheza sana maeneo ya katikati na kufanya mashambulizi ya hapa na pale. tuone sasa kipindi hiki cha lala salama kitatupa magoli yoyote

45' Mpira umekwisha anza hapa. Yanga wameanza mpira katikati pale

47' Japo Yanga wameanza wao mpira kipindi hiki lakini Simba ndio ana umiliki mkubwa.

49' Simba wanapata faulo hatua chache nje ya box la 18 la Yanga Niyonzima amechezewa faulo na Abdul. Okwi yupo maeneo ya Kupiga faulo ile

50' Okwi anapiga faulo ile, anapiga mpira kwa nguvu na kugonga ukuta mdogo wa Yanga

51' Simba wanafata faulo nyingine safari hii Okwi ndio kachezewa rafu na Vicent

51' Anaingiza faulo ile Nyoni, Mavugo anakutana nayo anapiga kichwa. Ni goal kick

55' Simba alipata kona hapa, Kichuya akapiga ya chinichini wakaokoa yanga. Yanga wakaanza safari kwa kufanya kaunta ataki, lakini manula naokoa na kuwapa Yanga kona

56' Sub; Simba wanafanya mabadiliko, anatoka Mavugo nafasi yake inachukuliwa na John Bocco

57'
Goooooooooooooooooooooooaallllllllllll. Kichuya anaweka kamba
Kichuya aliingia na mpira ule taratibu akapika krosi kwa 'outer' ikamkuta Okwi upande wapili wa 18 ya Yanga akamimina kipa wa yanga akacheza lakini ukamkuta mchezaji wa Simba (Nyoni) ambapo alimuwekea vizuri Kichuya

58' Kadi ya njano; Kichuya analambwa kadi ya njano kwa kukimbia nje ya uwanja na kupoteza muda

60' Gooooooooooooooooooooaaaaallllll. Chirwa anaweka kimiani

Yanga wanasawazisha kupitia Chirwa baada ya pasi ya Ajibu kumfikia Gadiel ambaye kapiga krosi dongo na Chirwa anaunganisha mbele ya Juuko

62' Mwashiuya anakwenda nje na nafasi yake inachukuliwa na Emmanuel Martin

65' Sub;
Yanga wamatoa Raphael Daud na nafasi yake ianchukuliwa na mkabaji Pato Ngonyan

66' Simba wanafanya shambulizi jingine, Yanga wanaokoa,inakuwa kona. Inachongwa vizuri hapa, kichwa cha Bocco, goal kick

67' Simba wanapata kona nyingine baada ya Okwi kuingia vizuri, inachongwa na Niyonzima, Rostande anaokoa vizuri kabisa

69' Kadi ya njano; Ajibu analambwa kadi ya njano baada ya kuonyesha jazba baada ya mwamuzi kupuliza filimbi

70' Kadi ya njano; Juma Abdul analambwa kadi ya njano baada ya kumuangusha Okwi

70' Krossi nzuri ya Tshishimbi, Ajibu anaunganisha vizuri kifundi kabisa lakini mpira unatoka juu kidogo tu

72' Simba wanajisahau, Yanga wanafanya shambulizi la kushitukiza, Emmanuel Martin yeye na kipa, anaachia mkwaju hapa, Manula anapangua na kwua kona

73' Kona nzuri sana hii, kichwa kinapigwa safi, Simba wanaokoa katika msitari kabisa

> Mpira umechangamka sasa na ile ladha ya Kariakoo derby sasa inaonekana dhahiri shahiri. Timu zinashambulia kwa zamu vizuri sana

81' Mwanjale alimtafuta Bocco kwa mpira mrefu pale, Bocco akageuka lakini angle ilikuwa ngumu ile. Ni goal kick

82' Mzamiru Yassin anapiga shuti fulanin la kitoto kabisa pale ila linatoka nje mbali na goal na kuwa goal kick

84' Sub; Simba wanamtoa Muzamiru na nafasi yake inachukuliwa na Said Ndemla, maana yake Simba wamemaliza Sub

87' Yondani yuko chini baada ya kuminya na kiatu cha Bocco, anatolewa kwenda kutibiwa nje. Mpira wasiamam kwa muda

91' Yanga wanapata kona baada ya Martin kujaribu kumuingiza Nyoni, na Nyoni kusimama imara. kona inapigwa ila Manula anadaka

92' Mpira Umekwisha.
Pambano hili la leo hakuna Mbabe. Si Simba wa Yanga anayeweza kutoka kifua mbele

stat-png.619277
 
Iyegu

Iyegu

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2014
Messages
6,301
Likes
12,202
Points
280
Iyegu

Iyegu

JF-Expert Member
Joined Jun 16, 2014
6,301 12,202 280
Uzi maalum wa mechi ya Leo.
Karibuni....
 
Wonderful

Wonderful

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2015
Messages
7,476
Likes
5,224
Points
280
Wonderful

Wonderful

JF-Expert Member
Joined Apr 8, 2015
7,476 5,224 280
KIKOSI CHA YANGA:
1. Youthe Rostand
2. Juma Abdul
3. Gadiel Michael
4. Andrew Vicent
5. Kelvin Yondani
6. Papy Tshitshimbi
7. Pius Buswita
8. Raphael Daud
9. Obrey Chirwa
10. Ibrahim Ajibu
11. Geofrey Mwashiuya
 
Wonderful

Wonderful

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2015
Messages
7,476
Likes
5,224
Points
280
Wonderful

Wonderful

JF-Expert Member
Joined Apr 8, 2015
7,476 5,224 280
KIKOSI CHA SIMBA:
1. Aishi Manula
2. Erasto Nyoni
3. Mohamed Zimbwe (C)
4. Juuko Murshid
5. Method Mwanjale
6. Jonas Mkude
7. Shiza Kichuya
8. Muzamiru Yassin
9. John Bocco
10. Emmanuel Okwi
11. Haruna Niyonzima
 
3llyEmma

3llyEmma

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2017
Messages
1,422
Likes
1,430
Points
280
3llyEmma

3llyEmma

JF-Expert Member
Joined Oct 23, 2017
1,422 1,430 280
Bocco amepona?..
weka mavugo hapo
 
radicals

radicals

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2016
Messages
2,352
Likes
2,597
Points
280
Age
38
radicals

radicals

JF-Expert Member
Joined Nov 7, 2016
2,352 2,597 280
kwani mechi ni saa ngapi,?
 
tramadol

tramadol

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2015
Messages
5,173
Likes
4,002
Points
280
tramadol

tramadol

JF-Expert Member
Joined Oct 10, 2015
5,173 4,002 280
Wengi wameogopa kuja na tiketi zilizouzwa na kwa wenye kadi tu hivyo nafasi bado zipo mpaka muda huu na tiketi zipo uwanjani zinauzwa... Njooni Please.

Muda huu ni saa saba na dakika 44 mchana tiketi zipo kibao tu za bila kadi.
 
chilumendo

chilumendo

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2013
Messages
2,318
Likes
1,792
Points
280
chilumendo

chilumendo

JF-Expert Member
Joined Oct 26, 2013
2,318 1,792 280
KIKOSI CHA SIMBA:
1. Aishi Manula
2. Erasto Nyoni
3. Mohamed Zimbwe (C)
4. Juuko Murshid
5. Method Mwanjale
6. Jonas Mkude
7. Shiza Kichuya
8. Muzamiru Yassin
9. John Bocco
10. Emmanuel Okwi
11. Haruna Niyonzima
mavugo alitakiwa aanze
 

Forum statistics

Threads 1,235,749
Members 474,742
Posts 29,233,845