Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) - Mkapa Stadium | Yanga SC v Simba SC

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Hello Tanzania na Ulimwengu kwa Ujumla...

Karibu katika Patashika ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL ) Jumamosi ya leo November 7, 2020 kunako Uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo Yanga SC kutoka mitaa ya Jangwani wanakwaruzana na Mabingwa wa Nchi Simba SC, kutoka mitaa ya Msimbazi.

Ni mchezo ambao utarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua kwa muda wote wa dakika 90 za mchezo, huku Yanga ikijivunia rekodi ya kutopoteza mchezo wowote hadi sasa huku ikiwa imeshinda saba na imetoka sare mara mbili kwa michezo tisa, ambapo Simba SC imepoteza michezo miwili na kutoka sare mchezo mmoja huku ikiwa imeshinda mchezo sita.

Kocha wa Yanga SC, Cedric Kaze amesema "Tunajua tutakabiliana na hali ngumu kesho (leo), lakini tumejiandaa kukabiliana na hali hiyo ngumu, pia mechi dhidi ya Simba SC ni kipimo kikubwa cha kwanza cha ubora wa kikosi cha Yanga SC" amesema Kaze.

Na upande wake Kocha wa Simba SC Sven Vanderbroeck amesema " Ni mchezo wa watani wa Jadi, lakini pia ni mchezo ambao tunapaswa kuwa makini zaidi ili kushinda na hatimaye kukusanya alama tatu muhimu" amesema Sven.

Nani kuibuka na alama tatu muhimu leo? timu kutoka JF sambamba nami nahodha Ghazwat ipo nawe mpaka mwisho... Usikose Ukaambiwa!

Kumbuka mtanange huu wa VPL ni kuanzia saa 11:00 jioni.

DA958623-6B27-4F18-9CAA-8E21673D058A.jpeg
 
Mashabiki wa Yanga na Simba uwanja wa Benjamin Mkapa wakiwa wengine tayari wamechukua nafasi zao kuweza kushuhudia mchezo huu wa VPL
Screenshot_20201107-141336.jpg
Screenshot_20201107-141321.jpg
 
Hii game ni ngumu upande wa UTO na huenda akapoteza au wakafungwa na Simba SC
 
Wananchi kama Wananchi, hatuna pressure, tuko makini kuhakikisha mnyama haleti matatizo mjini.

Lazima azibitiwe arudi porini ama akibidi tumgawane aishie jikoni.

Kila la kheri wananchi wenzangu ktk kazi hii nyepesi.
 
Simba dawa yake ni ndogo tu, mkamate muinue mkia wake.
Ukishaiona ile tundu yakutolea chakula kisicho na kazi tumboni, basi Simba hana maneno tena.
Leo wananchi tunaenda kuifanya hiyo kazi, amini.
 
Back
Top Bottom