Ligi Kuu Tanzania Bara kuanza kutimua vumbi Septemba 6

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Bodi ya ligi nchini TPLB leo imetangaza ratiba ya michezo ya ligi kuu Tanzania bara msimu wa mwaka 2020/2021 utakaoshirikisha jumla ya timu 18 huku Raundi ya saba vilabu vya Simba na Yanga vikitarajia kukutana October 18 mwaka huu katika dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam

Akitangaza ratiba hiyo mtendaji mkuu wa bodi ya ligi Almas Kasongo amesema ligi hiyo itaanza kutimua vimbi September 6 mwaka huu baada ya mchezo wa ufunguzi wa ligi wa ngao ya jamii Kati ya Simba SC dhidi ya Namungo utakaopigwa August 29 mwaka huu katika dimba la sheikh Amri Abeid jinini Arusha.

Kwa upande mwingine Kasongo amesisistiza kuwa katika upangwaji wa ratiba wamezingatia sana kuendana na Kalenda ya CAF pamoja na FIFA.

VPL itaanza August 6 kwa Namungo Fc Kucheza na Coastal Union katika dimba la Majaliwa huku Biashara United wakiwaalika Gwambina Fc katika dimba la Karume mjini Musoma nayo timu iliyopanda ligi kuu ya Dodoma Jiji watacheza na Mwadui Fc katika dimba la Jamhuri Jijini Dodoma.

Mabingwa watetezi Simba sc wao wataanza kuutetea ubingwa wao dhidi ya wageni wa ligi hiyo Ihefu FC ya Jijini Mbeya,Mtibwa Sugar watawaalika Ruvu Shooting na Yanga Sc wakicheza na Tanzania Prizons .

Ratiba inaonyesha kuwa raundi ya kwanza itakamilika agosti 7 ambapo KMC wataalika Mbeya City na mwisho Azam FC watacheza na Polisi Tanzania.

Jumla ya michezo 306 itapigwa kwenye raundi 34 ambapo ligi hiyo inatarajiwa kumalizika mei 5 mwakani

TAREHE 6 SEPTEMBA

Namungo FCV Coastal Union (Saa 8 Mchana)

Biashara V Gwambina FC (Saa 10 Jioni)

Dodoma FC V Mwadui FC (Saa 10 Jioni)

Ihefu Fc V Simba (Saa 10 Jioni)

Mtibwa Sugar V Ruvu Shooting (Saa 10 Jioni)

Young Africans V Tanzania Prisons (Saa 1 Usiku)

TAREHE 7 SEPTEMBA.

KMC V Mbeya City (Saa 8 Mchana)

Kagera Sugar V JKT Tanzania (Saa 10 Jioni)

Azam Fc V Polisi Tanzania (Saa 1 Usiku)
 
Raundi ya kwanza itamalizika August 7 mwaka upi?
Nafikir alimaanisha Sept 7 2020(siku ya pili yake) na c August means mechi za raundi ya kwanza kati ya raundi 34 na c mzunguko wa kwanza japo ktk lugha maneno yote yana maana moja lkn kimpira yana maana tofauti
 
Ila Tff nimewashanga hata ratiba kupanga inawasumbua hivi inakuwaje bingwa anaanzia ugenini halafu manyani yanaanzia nyumbani au hayana pesa za kusafiria
 
Simba kuanza na Ihefu haukuwa uamuzi wa msingi.
Simba ilipaswa ianze na Masao bwile au JKT Tanzania.
Ihefu wangeanza na japo KMC ili wapate uzoefu.
Maana wanaweza chezea 10:0 wakaishia kupata mfadhaiko wa mapema.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom