Ligi Kuu Tanzania Bara, Februari 16, 2019: Kariakoo Derby, Yanga SC 0 - 1 Simba SC

MSAGA SUMU

JF-Expert Member
May 25, 2015
6,478
20,390
Leo ndio leo, Watani wa jadi wanakutana katika mechi ya ligi kuu mzunguko wa pili, Yanga akiwa mwenyeji wa mchezo huu.

Yanga rekodi inambeba na wachambuzi wengi wanampa uwezekano mkubwa wa kushinda katika mchezo wa leo huku ikizingatiwa tangu kocha Mwinyi Zahera aje Yanga haijawahi kupoteza mchezo wowote kwa idadi kubwa ya magoli.

Kocha Patricks Aussem amekuwa na wakati mgumu na timu ya Simba baada ya kupata vipigo kadhaa mfululizo huku akipigwa goli 10 katika mechi 2 klabu bingwa.

UPDATE
MIDA YA SAA 4 ASUBUHI JESHI LA POLISI NA VYOMBO VYA USALAMA wanawakatalia wazee watatu wa Simba kuingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo vya wachezaji hasa baada ya kushindwa kutoa maelezo wanaenda kufanya nini vyumbani humo.

UPDATES: VIKOSI RASMI.

SIMBA: Aishi Manula, Zana Coulibaly, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Juuko Murshid, Serge Wawa, James Kotei, Clatous Chama, Jonas Mkude, John Bocco, Meddie Kagere na Emmanuel Okwi.

Benchi: Deo Munishi ‘Dida’, Nicholas Gyan, Yussuf Mlipili, Muzamil Yassin, Haruna Niyonzima, Hassan Dilunga na Rashid Juma.

Bechi la Ufundi; Kocha Mkuu, Patrick Aussems; Msaidizi Dennis Kitambi; Kocha wa mazoezi ya viungo, Mtunisia Adel Zrane; Kocha wa Makipa, Muharami Mohammed; Meneja Patrick Rweyemamu; Mtunza Vifaa, Hamisi Mtambo na Daktari Yassin Gembe.


YOUNG AFRICANS: Ramadhani Kabwili, Paulo Godfrey ‘Boxer’, Gardiel Michael, Andrew Vincent ‘Dante’, Kelvin Yondan, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Feisal Salum ‘Fei Toto’, Papy Kabamba Tshishimbi, Heritier Makambo, Amissi Tambwe na Ibrahim Ajibu.

Benchi: Klaus Kindoki, Juma Abdul, Said Juma ‘Makapu’, Haruna Moshi ‘Boban’, Mohammed Issa ‘Banka’, Mrisho Ngassa na Matheo Anthony.

Benchi la Ufundi: Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera; Msaidizi Noel Mwandila; Kocha wa Makipa Juma Pondamali; Meneja Nadir Haroub ‘Cannavaro’; Mratibu Hafidh Saleh; Daktari Edward Bavu na Mtunza Vifaa, Mohammed Omar ‘Mpogolo’.


MAPUMZIKO
Takwimu za kipindi cha kwanza zinaonesha hakuna shuti lolote lililolenga lango kwa timu zote mbili.

1.png

Dakika ya 71: Gooooooallllllllll ni Meddie Kagere
Yuleyule aliyeimaliza Al Ahly Meddie Kagere ameitanguliza Simba kwa bao la kuongoza alilofunga kwa kichwa akimaliza kazi nzuri ya John Bocco.

MPIRA UMEISHA
1.png
 
Umeandika kishabiki sana, hata updates zako umeweka za Yanga tu.
Simba wamefungwa kwenye CAF tournament, lakini kwa hapa nyumbani rekodi zinambeba zaidi Simba.

Mechi za hivi karibuni Yanga amefanya vibaya. Katika mechi kama tano hivi yanga ameshapoteza Points 7.

Hii ndo kama ile ya awali ambako walipotoka droo, Yanga alishangilia wakati Simba alisikitika.
 
Hatimaye ile siku ya kukata mzizi wa fitina baina ya miamba ya soka nchini Simba na Yanga imewadia. Tambwe, majigambo na majivuno kutoka pande zote kuna kila dalili yatabaki upande mmoja tu- utakaoibuka kidedea. Haitarajiwi kuwa mechi itakayoisha kwa sare leo

Pamoja na ukweli kuwa kuna imani kuwa mchezo wa Simba na Yanga huwa hautabiriki, lakini kwa mtu makini atagundua kuwa kuna kipindi timu zinapokuwa zimepishana sana ubora, matokeo hufuata uwezo ulikolalia.

Sote tunakumbuka jinsi Yanga iliyokuwa bora msimu wa 2014/2015, na 2015/2016, ilivyoipiga Simba ndani nje bila kujali imani zilizopo kuwa yule aliye dhaifu ndiye hushinda. Ndivyo pia ilivyotokea katika muongo wa kwanza wa karne hii miaka ya 2000 - 2010 jinsi Simba ilivyokuwa na ubora kuliko Yanga na kuipiga mfululizo kwa takribani miaka 8 ambapo mafanikio ya Yanga yalikuwa ni sare.

Ni kwa muktadha huu, siku ya leo inaonekana itakuwa mbaya kwa Wanajangwani a.k.a wananchi kwa kuwa kuna ufa mpana sana wa ubora baina yao na Simba. Simba bila ubishi wowote inapokuwa katika ubora wao, ni ngumu kuizuia isifunge goli kwenye uwanja mzuri kama wa Taifa. Kila unapoangalia vikosi vya timu hizi, inabaki ni miujiza pekee ya kuikoa Yanga. Eneo litakaloiathiri zaidi Yanga ni eneo la golikipa. Ramadhani Kabwili ni kijana mdogo anayekuja vizuri lakini ni wazi mechi hii ni kubwa mno kwake. Anahitaji ulinzi mzuri zaidi utakaompa kujiamini, kitu ambacho bado huwezi kujiaminisha kwa kiasi kikubwa kwa aina ya beki line ya Yanga. Ili kuwazuia Bocco, Kagere na Okwi wasifunge katika Uwanja wa Taifa, hasa wanapokuwa wamepania, unapaswa kuwa 'on the top of your game' kwa muda wote wa mchezo. Hii ni pacha bora zaidi ya ushambuliaji nchini huku pia ikitisa katika anga za kimataifa.

Kuna mabadiliko makubwa ya kiufundi ya timu hizi tangu mtanange wao wa mwisho Septemba 30 mwaka jana. Benno Kakolanya hayupo aliyetajwa kuokoa zaidi ya magoli 7 ya wazi kwa Simba iliyokuwa bado inatengeza pacha ya ushambuliaji! Leo hii Simba inaonekana kuunga karibu kila sehemu ya uwanja kwa hiyo vijana wa Mwinyi Zahera kazi wanayo.

Aidha, habari mbaya zaidi kwa Yanga ni uwepo wa John Bocco ambaye hakucheza mechi ya mkondo wa kwanza kwa tatizo la kadi 3 za njano. Huyu ana ufunguo usionekana wa kuiyumbusha beki yoyote na ndiyo maana hakosi kupangwa kila anapokuwa fit. Japo washabiki wengi wa Simba wanamchukilia poa, lakini John Bocco anatoa utulivu mkubwa katika timu hasa eneo la ushambuliaji hivyo kuwaacha wachezaji wengine Okwi na Kagere wakifaidi mianya anayoisababishia defence ya timu pinzani.

Kuteseka kwa Yanga leo hakutatokana na matokeo ya mechi pekee, lakini faida watakayoipata Simba kuelekea mbio za kuchukua ubingwa. Simba ikishinda, itaifanya Yanga iwe na pressure kubwa zaidi na hivyo uwezekano wa kudondosha pointi nyingi zaidi. Lakini pia Yanga ikishinda itaivuruga Simba kisaikolojia na inawezekana ikashinda ubingwa mwisho wa msimu.

Vyovyote iwavyo mshindi wa leo ndiye ambaye kwa kiwango kikuu atainua kwapa kupokea taji la Ligi Kuu Bara hapo mwezi Mei.

Naitakia timu bora ushindi ili heshima katika mpira iwepo
 
Back
Top Bottom