LIGI KUU BARA: Timu za Simba na Yanga haziruhusiwi kucheza mechi zake usiku?

Jacobus

JF-Expert Member
Mar 29, 2011
4,700
1,721
Wakuu,

Imebidi kutafuta msaada wenu kufahamu ni vigezo gani vinatumiwa na TFF (shirikisho la soka) kupanga mechi za timu za Simba na Yanga kuchezwa mchana tu. Mpaka sasa timu takribani zote zinacheza mechi zake usiku pale uwanja wa Azam uliopo Chamazi ila kwa timu hizo mbili tu zimekataliwa kucheza hapo na TFF japo zenyewe zimesema sio tatizo. Kama hakuna basi TFF itende haki kwa timu zote.
 
Pita usiku wakukabe.. Karibu mtaani kwetu, japo alikabwa mtu juzi.

#TMK_MASKANI
 
Sababu za kiusalama

Zilichezwa mchana viti viling'olewa sasa zikichezwa usiku si watang'oa hadi yale machuma golini na nyasi zote za uwanjani
 
Sababu za kiusalama

Zilichezwa mchana viti viling'olewa sasa zikichezwa usiku si watang'oa hadi yale machuma golini na nyasi zote za uwanjani
Mimi Nilikua Sijui kama Uwanja Wa Taifa una Taa za Kuchezea Mpira Mpaka AZAM ilipocheza na Mamelod Usiku.... Ishu ya Usalama ni ya Jeshi la Polisi Mbona Fiesta zinafanyika Usiku na ndio tukio linalokusanya Wahuni Kibao?
 
Sababu za kiusalama

Zilichezwa mchana viti viling'olewa sasa zikichezwa usiku si watang'oa hadi yale machuma golini na nyasi zote za uwanjani
Oh kweli ni hatari sana ila mkuu mie nilimaanisha mechi za timu hizi na timu nyengine kama Azam FC anavocheza na timu nyengine pale Chamazi.
 
Back
Top Bottom