Life is not fair: Niliamini uwezekano wa kupata pesa kwa njia halali ni mkubwa sana...

Mshika Tester

Member
May 3, 2020
38
35
Sijui ndiyo nimeanza kukata tamaa kwa kweli sijielewi! Zamani niliamini uwezekano wa kupata pesa kwa njia halali ni mkubwa sana, niliamini uchawi si chochote lakini sasa naanza kuingiwa na kaimani, watu tunataabika miaka mingi kutafuta mali kwa njia halali tunawahi kuamka daily, tunapiga kazi bila kuchagua, tunajibana kula na kuvaa, hatuna mademu wakali, hatuni nyumba, magari, tumechelewa kuzaa na kuoa.

Lakini tunaowaona wazembe kila siku wanapiga hatua tu wanaenjoy maisha vyote tunavyojizuia kufanya ili tufanikiwe wao wanafanya tena kwa speed kama yote hata hivyo mafanikio yanaendelea kuwafuata (sina maana sipendi wengine wafanikiwe ila ni mfano wa kulinganisha na sisi tunao hastle).

Naanza kuamini upepo wa pesa, nuksi, mikosi na chuma ulete nk, tunapata pesa haikai na ukiangalia hatuna majukumu mengi kama kusomesha, kutunza wazazi, kutunza familia cha ajabu zaidi hatuna matumizi ya anasa, lakini bado hela haikai kila siku umaskini unaongezeka makali.

Niliamini nitakuja kuwa tajiri siku moja lakini kadiri siku zinavyosonga mbele mambo yanachange, naamini pia vijana wengi wa kati ya 18-27 wanaamini watakuja kuwa matajiri pia.

Angalizo! Usiamini kama mimi inawezekana mimi nimenza kukata tamaa au kuna maarifa fulani sahihi nimekosa katika harakati zangu, hebu na wewe jipe muda kufanya utafiti kabla hujaanza kuwaza kama mimi.

Yesu mwokozi naomba nisaidie nisiingie kwenye ushirikina angalau nipe ishara za kwenda peponi niridhike kuwa sitakuwa tajiri lakini nitaenda peponi kuliko hivi sasa. Sijui nikifa nitaenda kuteseka katika moto wa milele au nitaenda peponi. Naogopa nisije nikawa nimeteseka duniani na mbinguni nikateseka pia nikiwa moja ya viumbe vilivyoumbwa kwa ajili ya kuteseka.
 
Mkuu kwa kuwa hapo mwisho umemtaja Yesu mwokozi, basi na Mimi nitakujibu kiyesu Yesu. NI hivi, Mungu humkirimia mtu kadili impendezavyo Wala huwezi kumpangia.

Kama fungu lako lilikuwa ni kupata utapata tu, ila Kama fungu lako ni kuwa mtumwa/mkosaji utapigika milele. Otherwise hama upande nenda kwenye ushirikina. Kule faster tu ila gharama zake ni kubwa Sana. Kupanga ni kuchagua.
 
Mkuu kwa kuwa hapo mwisho umemtaja Yesu mwokozi, basi na Mimi nitakujibu kiyesu Yesu. NI hivi, Mungu humkirimia mtu kadili impendezavyo Wala huwezi kumpangia. Kama fungu lako lilikuwa ni kupata utapata tu, ila Kama fungu lako ni kuwa mtumwa/mkosaji utapigika milele. Otherwise hama upande nenda kwenye ushirikina. Kule faster tu ila gharama zake ni kubwa Sana. Kupanga ni kuchagua.

Asante sana... sitofanya njia yoyote haramu ili nifanikiwe wanao fanya acha waendelee tu kama kukosa basi acha iwe hivyo.
 
Mkuu kwa kuwa hapo mwisho umemtaja Yesu mwokozi, basi na Mimi nitakujibu kiyesu Yesu.
NI hivi, Mungu humkirimia mtu kadili impendezavyo Wala huwezi kumpangia. Kama fungu lako lilikuwa ni kupata utapata tu, ila Kama fungu lako ni kuwa mtumwa/mkosaji utapigika milele. Otherwise hama upande nenda kwenye ushirikina. Kule faster tu ila gharama zake ni kubwa Sana. Kupanga ni kuchagua.

Hivi ni kweli usemayo Kama Mungu hajapanga upate hutapata?..mie hapa ndo nachokaga....Sasa kwanini wengine wapate wengine wasipate? Au ndo ana sababu zake😭😭!

Ila ukisoma vitabu vya dini inasisitiza Sana sadaka na zaka..nadhan tunasahau hizo kanuni
 
Mkuu kila upande una kanuni zake...upande wa Giza unakanuni zake na upande wa nuru una kanuni zake hakuna kitu kama fungu LA kukosa au fungu la kupata ...fata kanuni za upande uliopo kama upo upande wa nuru fata kanuni za huko hakika utaona matunda ya kazi yako.

Hakikisha humuibii Mungu zaka na sadaka ya mapato yako ...katika kila jambo mtangulize Mungu usizitegemee akili zako nae atakunyooshea mapito yako....kanuni ya kupokea ni kutoa hakuna mchawi katika hilo... Na kila jambo na wakati wake trust the process.
 
Mkuu kila upande una kanuni zake...upande wa Giza unakanuni zake na upande wa nuru una kanuni zake hakuna kitu kama fungu LA kukosa au fungu la kupata ...fata kanuni za upande uliopo kama upo upande wa nuru fata kanuni za huko hakika utaona matunda ya kazi yako..hakikisha humuibii Mungu zaka na sadaka ya mapato yako ...katika kila jambo mtangulize Mungu usizitegemee akili zako nae atakunyooshea mapito yako....kanuni ya kupokea ni kutoa hakuna mchawi katika hilo... Na kila jambo na wakati wake trust the process..

Ewaa...mie nayaishi haya...! Kila kitu kina kanuni....! Ukikosa steps moja ndo hayo matokeo!..mie naamini kwenye ulichoandika sana Sana hadi nakwazana kbs na watu
 
Hivi ni kweli usemayo Kama Mungu hajapanga upate hutapata?..mie hapa ndo nachokaga....Sasa kwanini wengine wapate wengine wasipate? Au ndo ana sababu zake😭😭!
Ila ukisoma vitabu vya dini inasisitiza Sana sadaka na zaka..nadhan tunasahau hizo kanuni
Ndio mana wengine wanapiga short cut (ushirikina, ufisadi, ujambazi nk), maana kwa Mungu hakuna guarantee mana hakuambii utapata au hutapata.
 
Hakuna mtu aliyeandikiwa atakuwa masikini hii dunia.Hata Mungu wa Mbinguni anachukia masikini.
Tafuta,tafuta ipo siku utapata hata kama usipokifaidi sana wewe watakifaidi wanao.Watajiuliza dogo yule kapataje mali? Karithi kutoka kwa baba yake.Wataanza kutafuta kuhusu wewe ulifanikiwaje.Yawezekana ukawa ushaondoka duniani ila utafungua fahamu za wengi huku nyuma.Mimi nina malengo yangu.Nataka ninavyohangaika hivi,sitaki wanangu wahangaike kabisa.Najitahidi kuwawekea misingi toka wadogo yaani.Nawaanda wawe wasimamizi wa miradi ikitokea nimerudi mavumbini.Nataka wajivunie mimi kuwa baba yao hata nisipokuwepo.
Achana na njia za giza.Zitakugharimu wewe.Na kibaya zaidi wanao.Yaani bora usipopata uwaache tu wakue watapata zao.
 
Nimefurahia sana aya ya mwisho.
Mungu akufungulie njia za kipato chako.
Mkuu unaifahamu hadithi ya Daniel na vile maombi yake yalichelewa kujibiwa??Unapafahamu pale majibu yake yalikozuiliwa?

12Ndipo yeye akaniambia, ‘Danieli, usiogope. Mungu alilisikia ombi lako tangu siku ile ya kwanza ulipoamua kujinyenyekesha mbele yake ili upate ufahamu. Mimi nimekuja kwa ajili ya ombi lako hilo. 13Mkuu wa ufalme wa Persia alinipinga kwa muda wa siku ishirini na moja. Lakini Mikaeli, mmoja wa wakuu, akaja kunisaidia, kwa hiyo nikamwacha huko pamoja na mkuu wa ufalme wa Persia, 14nami nimekuja kukusaidia uyafahamu mambo yatakayowapata watu wako wakati ujao

Basi pale pana hazina zetu zote, shida inakuja how to access that, nguvu zetu katika maombi ya kutoboa upenyo lakini pia namna ya kuishi katika utakatifu ili shetani asipate cha kutushtaki nacho.
 
Sijui ndiyo nimeanza kukata tamaa kwa kweli sijielewi! Zamani niliamini uwezekano wa kupata pesa kwa njia halali ni mkubwa sana, niliamini uchawi si chochote lakini sasa naanza kuingiwa na kaimani, watu tunataabika miaka mingi kutafuta mali kwa njia halali tunawahi kuamka daily, tunapiga kazi bila kuchagua, tunajibana kula na kuvaa, hatuna mademu wakali, hatuni nyumba, magari, tumechelewa kuzaa na kuoa.

Lakini tunaowaona wazembe kila siku wanapiga hatua tu wanaenjoy maisha vyote tunavyojizuia kufanya ili tufanikiwe wao wanafanya tena kwa speed kama yote hata hivyo mafanikio yanaendelea kuwafuata (sina maana sipendi wengine wafanikiwe ila ni mfano wa kulinganisha na sisi tunao hastle).

Naanza kuamini upepo wa pesa, nuksi, mikosi na chuma ulete nk, tunapata pesa haikai na ukiangalia hatuna majukumu mengi kama kusomesha, kutunza wazazi, kutunza familia cha ajabu zaidi hatuna matumizi ya anasa, lakini bado hela haikai kila siku umaskini unaongezeka makali.

Niliamini nitakuja kuwa tajiri siku moja lakini kadiri siku zinavyosonga mbele mambo yanachange, naamini pia vijana wengi wa kati ya 18-27 wanaamini watakuja kuwa matajiri pia.

Angalizo! Usiamini kama mimi inawezekana mimi nimenza kukata tamaa au kuna maarifa fulani sahihi nimekosa katika harakati zangu, hebu na wewe jipe muda kufanya utafiti kabla hujaanza kuwaza kama mimi.

Yesu mwokozi naomba nisaidie nisiingie kwenye ushirikina angalau nipe ishara za kwenda peponi niridhike kuwa sitakuwa tajiri lakini nitaenda peponi kuliko hivi sasa. Sijui nikifa nitaenda kuteseka katika moto wa milele au nitaenda peponi. Naogopa nisije nikawa nimeteseka duniani na mbinguni nikateseka pia nikiwa moja ya viumbe vilivyoumbwa kwa ajili ya kuteseka.
Work smart mkuu.
 
Mkuu kwa kuwa hapo mwisho umemtaja Yesu mwokozi, basi na Mimi nitakujibu kiyesu Yesu. NI hivi, Mungu humkirimia mtu kadili impendezavyo Wala huwezi kumpangia.

Kama fungu lako lilikuwa ni kupata utapata tu, ila Kama fungu lako ni kuwa mtumwa/mkosaji utapigika milele. Otherwise hama upande nenda kwenye ushirikina. Kule faster tu ila gharama zake ni kubwa Sana. Kupanga ni kuchagua.
Ki Yesu Yesu zaid au sio.ahahahah.
 
Back
Top Bottom