Life After Life: Je, Wafu huwaita watu kifoni? Kuna walio hai huamua kuwafuata Wafu? Wapenzi mmoja akitangulia, mwenzake anafuata!

KeyserSoze

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
5,755
2,000
Pale sisi ambao hatujafa kujaribu ku - explain kuhusu what happens to a dead individual zaidi ya mwili kuoza ni suala la ki - imani tu na assumptions,
 
Eng Kahigwa

JF-Expert Member
Feb 18, 2014
778
1,000
Wanabodi,
Kifo cha Ephraim Kibonde kimeibua simanzi kubwa kwa sababu katika uhai wake hakuwahi kuugua, amekufa ghafla, hivyo watu kubaki na maswali mengi.
Katika bandiko la Tribute to Kibonde, kuna mwana JF kaandika maneno haya kumhusu Kibonde.

Kufuatia kuyasoma hayo, nimeona nizungumze kitu kuhusu uhai, kifo na maisha baada ya kifo.

Uhai ni Nini na Kifo ni Nini?.
Mwili wa binadamu una sehemu mbili, sehemu ya kwanza ni huu mwili wa nyama, ambao umeumbwa kwa mavumbi, na siku ukifa, kinachokufa ni mwili huu wa nyama, unazikwa kaburini, humo ndani unaoza na kurudi kuwa mavumbi. Sehemu ya pili ya mwili ni uhai, uhai hii ni pumzi Mungu aliyoipulizia kwenye ule udongo hivyo mwili kupata uhai. Hii ni Roho ya Mungu, the spiritual body, the astra body, mwili unapokufa, roho haifi, bali huacha mwili na kurudi kwa Mungu. Hivyo kifo ni kitendo cha roho kuacha mwili.

Jee Baada ya Kifo, hiyo Roho inakwenda Kuishi Wapi?.
Kama ulivyo mwili una sehemu mbili ya mwili wa nyama na mwili wa roho, vivyo hivyo dunia ina sehemu mbili, Ulimwengu wa Kidunia, the physical world, na Ulimwengu wa Roho, the Spiritual World, mtu akifa, roho ikiacha mwili, mwili unabaki kwenye ulimwengu wa dunia, unazikwa unaoza na kugeuka kuwa mavumbi, Roho inakwenda kwenye ulimwengu wa Roho kuendeleo kuishi milele, being mbinguni, peponi, kuzimu, toharani, au jehanum kwenye moto wa milele, hii subject nyingine lakini roho hazifi kwa sababu roho ni Mungu.

Jee Roho za Waliokufa Zinaweza Kuwaita Walio Hai?.
Jibu ni yes, ndio maana kwa baadhi ya mila, wamama wajawazito hawaruhusiwi kwenda makaburini, ili waliolala wasije wakaviita vichanga, na matokeo yake vikaitika na kupata still born.
Kwenye mahusiano kuna kitu kinaitwa Soul Mates, na hii ndio subject matter ya uzi wangu huu.

Mahusiano ya Mapenzi, ya Aina Tatu, Kuna Mapenzi ya Mwili, Ya Raha na Mapenzi ya Roho ambayo Ndio Mapenzi ya Kweli.
Kama ulivyo mwili una mwili wa nyama, na mwili wa roho, vivyo hivyo kwenye mapenzi, kuna mapenzi ya mwili, physical love, na mapenzi ya moyo, spiritual love, emotional love.
Mapenzi ya physical love, ni yale mapenzi ya mambo ya mwilini, yanajumuisha mapenzi ya kutamani mwili na kufanya lile tendo la sex, sometimes ni needs, tamaa, infatuation, kila kiumbe mwenye viungo timilifu vya uzazi, anaweza kufanya physical love na kuridhika na tendo na kutoshesha mechanically, lakini hakuna emotional na spiritual love, na hiki ndicho mara nyingi hufanyika kwenye biashara ya mapenzi, wale wadada wanaojiuza, hufanya physical love tuu kwa uhitaji wa pesa, lakini hakuna emotional love wala spiritual love.

Mapenzi ya Kweli ni zaidi ya Sex, ni Emotional na Spiritual.
Ili kupata mpenzi wa kweli na kufanya mapenzi ya kwenzi, yule mpenzi unaekutana nae lazima awe ndie soul mate wako. Yaani mtu uliyeumbiwa wewe kuwa parner wako wa maisha ya kimwili na kiroho, hivyo mkifanya sex, sio tuu mnafanya tendo, bali mnaunganika na kuwa mwili mmoja in spiritual body, hivyo mahusiano ya hivi, mmoja akitangulia, yule aliyebaki duniani hawezi kuishi muda mrefu, atamfuata tuu mwenzake, na mapenzi yao yataendelea kwenye the spiritual world.

Je Utajuaje Mpenzi Uliyenae Kama Ndie Soul Mate Wako?.
Haya sasa ni mambo ya Roho, naomba nisiyazungumze hapa.

Roho za Wafu, Zinaweza Kuziita Roho za Walio Hai Au Walio Hai, Wakajipeleka Wenyewe Kifoni.
Watu walikufa ambao roho zao zinaishi kwenye ulimwengu wa Roho, wanaweza kuwaita watu wowote wenye strong bond nao, kutoka duniani na kuwafuata kifoni, wengi wa watu wanaitwa kwa namna hii, hufa ghafla. Wengi ni pale mmoja anapotangulia, mwingine hawezi ku recover hivyo ni ama ni yeye mwenyewe aliye hai anaona maisha bila ya mwenzake hayana maana, hivyo kutamani kumfuata, ama aliyekufa anamuita mwenza wake kifoni, hivyo mwenza kumfuata.

Hivyo kama ni kweli Ephraim Kibonde alisema mke wake ni soul mate wake, usikute Ruge ndio alikuwa kila kitu kwa Ephraim Kibonde, hivyo baada ya kifo cha mke wake, Ephraim aliweza kuendelea kuishi kwa vile Ruge yupo, ilipotokea Ruge amekufa, katika kuushughulikia msiba huo, roho ya Ruge na Roho ya Mke wa Kibonde, zikakutana na kumuita Ephraim kuwa sisi tuko huku, wewe huko unangoja nini?, hivyo Roho ya Ephrain=m, ikasikia saiti hizo, na yeye mwenyewe ku will, kuwa nitawafuata. Baada ya ku will kuwa uko tayari kuwafuata, powers of will hutafuta sababu yoyote ya kukuchomoa, kikawaida ikikosekana sababu yoyote, iwe ni ugonjwa wa ghafla, ajali, or majanga yoyote ya kuondoa roho, then mtu alikuwa ni mzima, analala usingizini, kesho yake haamki.

Hitimisho.
Kwa vile kwa sisi binadamu wote hapa duniani tuko safari tuu, kuelekea kwenye maisha ya milele, tusiwalilie waliotangulia na kuhuzunika kuwa kosa, bali tujiangalie sisi wenyewe, jee tumejiandaa kuitika wito wakati siku yetu na saa yetu ikitakapofika?.

Kesheni mkiomba kwa maana hamjui siku wala saa.
RIP Ephraim Kibonde na Ruge Mutahaba na wengine wote waliotangulia, nyinyi mbele sisi tuko nyuma yenu, sote sisi ni kwake tutarejea.

Paskali
Namngojea Dr mshana jr aje anielezee vizuri aisee.
 
Freyzem

JF-Expert Member
Jun 29, 2013
8,985

Kifo cha Ephraim Kibonde kimeibua simanzi kubwa kwa sababu katika uhai wake hakuwahi kuugua
...kwa maneno hayo mkuu, sijui ulimaanisha nini!??
..Yaani Keb hakuwahi kuugua maishani mwake?
Hebu pitia hapa kwanza...!!

Halafu mkuu, mbona siku hizi mashati hayakukai sawasawa...!? Unafanya diet mkuu?
Madaktari wamponda Kibonde kupitia mtandao wa FB - JamiiForums

Sent using Vertu Signature Cobra
 
mangatara

JF-Expert Member
Jul 6, 2012
14,542
2,000
Leo Paskali naomba nitofautiane na wewe kidogo. Haswa kuhusu uwezo wa kuitwa na wafu. Hata wangekuita mkaenda kutembea, unarudi tu na kuendelea na usingizi wako bila shida. Wafu hawana mamlaka yeyote juu yao walio hai.
Hivi wewe, wadhani jinsi watu siku hizi wamejaa roho mbaya na wanavyo wafanyia hiana wenzao. Si hao waliouliwa bila sababu wangeshaanzisha chama chao huko waje kuwafuata walio wapeleka huko kabla ya muda wao??
Muumba aliweka ukomo wa hilo. Kwanza kuna bonde kubwa sana kati ya walio hai na waliokufa. Hakuna roho iwezayo kuvuka na kurudi duniani. Nakataa. Wabongo wengi wangesharudi kwetu walipize visasi.
Chukulia hivi, Hakuna mtu ajuaye saa yake hivyo ikitokea coincidence unakuta tumeandikiwa saa inayo karibiana au saa moja. Mfano ni ajali. Jamaa yangu mmoja alikuwa anaendesha gari lenye familia yake. Mke na watoto 4 na yeye. Gari iliingia chini ya lori wakasagika wala hakuna aliyeweza kumtambua mtu. Jamaa alitolewa unconscious/hajitambui kwa wiki 3.
Tuliwazika wale wengine wote ila mtu akatoka na kuishi tena.
Nasemea saa ya kuitwa. Tulizika watu 4 siku moja. Huwezi sema ati mama aliwaita watoto wake wote siku hiyo. Kifo hakina saa wala siku ni muda wako ukifika. Kila sekunde kuna mtu anakufa mahali fulani.
Ruge na Efraim walikuwa marafiki ila hawawezi kuitana ili kufa pamoja. Mbona mmoja aliugua sana na mwingine hakuugua?? Tena ulivyo unganisha hicho kifo cha mkewe Ephraim na Ruge sio vizuri hata kidogo. Waweza kuwa ni rafiki yangu wa dam lakini nisikukute hata unamtoa mwiba shemejio akiwa hata sebuleni. Hapo napo umeniudhi. Wataka kuniambia kuwa huyo mdada alinini ati??
 
Smart911

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
65,618
2,000
"Yaani mtu uliyeumbiwa wewe kuwa parner wako wa maisha ya kimwili na kiroho, hivyo mkifanya sex, sio tuu mnafanya tendo, bali mnaunganika na kuwa mwili mmoja in spiritual body, hivyo mahusiano ya hivi, mmoja akitangulia, yule aliyebaki duniani hawezi kuishi muda mrefu, atamfuata tuu mwenzake, na mapenzi yao yataendelea kwenye the spiritual world."

Hatari sana... ndiyo maana vifo vya ghafla nje nje... ngoja nikae kimya...

Cc: mahondaw
 
lukesam

JF-Expert Member
Feb 23, 2015
10,681
2,000

Nimeusoma huu uzi nikamaliza na sikuamini kama huyu ni Pasco. Ikabidi nirudi juu kuona kama ni yeye kweli au ni Mshana Jr
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom