Life After Life: Je, Wafu huwaita watu kifoni? Kuna walio hai huamua kuwafuata Wafu? Wapenzi mmoja akitangulia, mwenzake anafuata!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,434
113,444
Wanabodi,
Kifo cha Ephraim Kibonde kimeibua simanzi kubwa kwa sababu katika uhai wake hakuwahi kuugua, amekufa ghafla, hivyo watu kubaki na maswali mengi.
Katika bandiko la Tribute to Kibonde, kuna mwana JF kaandika maneno haya kumhusu Kibonde.
Sikumfahamu zaidi ya kumuona kwenye Mkasi akihojiwa na Salama Jabir. Alisema mke wake ni soul mate wake, siwezi kusahu nilivyo sisimkwa kusikia mwanaume akimsifia mke wake vile.
R.I.P both of you.

Kufuatia kuyasoma hayo, nimeona nizungumze kitu kuhusu uhai, kifo na maisha baada ya kifo.

Uhai ni Nini na Kifo ni Nini?.
Mwili wa binadamu una sehemu mbili, sehemu ya kwanza ni huu mwili wa nyama, ambao umeumbwa kwa mavumbi, na siku ukifa, kinachokufa ni mwili huu wa nyama, unazikwa kaburini, humo ndani unaoza na kurudi kuwa mavumbi. Sehemu ya pili ya mwili ni uhai, uhai hii ni pumzi Mungu aliyoipulizia kwenye ule udongo hivyo mwili kupata uhai. Hii ni Roho ya Mungu, the spiritual body, the astra body, mwili unapokufa, roho haifi, bali huacha mwili na kurudi kwa Mungu. Hivyo kifo ni kitendo cha roho kuacha mwili.

Jee Baada ya Kifo, hiyo Roho inakwenda Kuishi Wapi?.
Kama ulivyo mwili una sehemu mbili ya mwili wa nyama na mwili wa roho, vivyo hivyo dunia ina sehemu mbili, Ulimwengu wa Kidunia, the physical world, na Ulimwengu wa Roho, the Spiritual World, mtu akifa, roho ikiacha mwili, mwili unabaki kwenye ulimwengu wa dunia, unazikwa unaoza na kugeuka kuwa mavumbi, Roho inakwenda kwenye ulimwengu wa Roho kuendeleo kuishi milele, being mbinguni, peponi, kuzimu, toharani, au jehanum kwenye moto wa milele, hii subject nyingine lakini roho hazifi kwa sababu roho ni Mungu.

Jee Roho za Waliokufa Zinaweza Kuwaita Walio Hai?.
Jibu ni yes, ndio maana kwa baadhi ya mila, wamama wajawazito hawaruhusiwi kwenda makaburini, ili waliolala wasije wakaviita vichanga, na matokeo yake vikaitika na kupata still born.
Kwenye mahusiano kuna kitu kinaitwa Soul Mates, na hii ndio subject matter ya uzi wangu huu.

Mahusiano ya Mapenzi, ya Aina Mbili Kuna Mapenzi ya Mwili, na Mapenzi ya Roho ambayo Ndio Mapenzi ya Kweli.
Kama ulivyo mwili una mwili wa nyama, na mwili wa roho, vivyo hivyo kwenye mapenzi, kuna mapenzi ya mwili, physical love, na mapenzi ya Roho, spiritual love, emotional love.
Mapenzi ya physical love, ni yale mapenzi ya mambo ya mwilini, yanajumuisha mapenzi ya kutamani mwili na kufanya lile tendo la sex, sometimes ni needs, tamaa, infatuation, kila kiumbe mwenye viungo timilifu vya uzazi, anaweza kufanya physical love na kuridhika na tendo na kutoshelezeka, mechanically, lakini hakuna emotional na spiritual love, na hiki ndicho mara nyingi hufanyika kwenye biashara ya mapenzi, wale wadada wanaojiuza, hufanya physical love tuu kwa uhitaji wa pesa, lakini hakuna true love, emotional love wala spiritual love.

Mapenzi ya Kweli ni zaidi ya Sex, ni True love, Emotional na Spiritual.
Ili kupata mpenzi wa kweli na kufanya mapenzi ya kweli, yule mpenzi unaekutana nae lazima awe ndie soul mate wako uliyepangiwa ile siku unazaliwa. Yaani mtu uliyeumbiwa wewe kuwa parner wako wa maisha ya kimwili na kiroho, hivyo mkifanya sex, sio tuu mnafanya tendo, bali mnaunganika na kuwa mwili mmoja in spiritual body, na kutengeneza a special bond, hivyo mahusiano ya hivi, mmoja akitangulia, yule aliyebaki duniani hawezi kuishi muda mrefu, atamfuata tuu mwenzake, na mapenzi yao yataendelea kwenye the spiritual world kutokana na ile bond ambayo haiwezi kukatika.

Je Utajuaje Mpenzi Uliyenae Kama Ndie Soul Mate Wako?.
Haya sasa ni mambo ya Roho, naomba nisiyazungumze hapa.

Roho za Wafu, Zinaweza Kuziita Roho za Walio Hai Au Walio Hai, Wakajipeleka Wenyewe Kifoni.
Watu walikufa ambao roho zao zinaishi kwenye ulimwengu wa Roho, wanaweza kuwaita watu wowote wenye strong bond nao, kutoka duniani na kuwafuata kifoni, wengi wa watu wanaitwa kwa namna hii, hufa ghafla. Wengi ni pale mmoja anapotangulia, mwingine hawezi ku recover hivyo ni ama ni yeye mwenyewe aliye hai anaona maisha bila ya mwenzake hayana maana, hivyo kutamani kumfuata, ama aliyekufa anamuita mwenza wake kifoni, hivyo mwenza kumfuata. Hii pia hutokea kwa identical twins kama wanaushi karibu, na twin mmoja akitangulia, kuna mila inafanywa ili kumkinga twin aliyebaki asimfuate.

Hivyo kama ni kweli Ephraim Kibonde alisema mke wake ni soul mate wake, usikute Ruge ndio alikuwa kila kitu kwa Ephraim Kibonde, hivyo baada ya kifo cha mke wake, Ephraim aliweza kuendelea kuishi kwa vile Ruge yupo, ilipotokea na Ruge amekufa, katika kuushughulikia msiba huo, roho ya Ruge na Roho ya Mke wa Kibonde, zikakutana na kumuita Ephraim kuwa sisi tuko huku, wewe huko unangoja nini?, hivyo Roho ya Ephraim, ikasikia sauti hizo, na yeye mwenyewe ku will, kuwa nitawafuata. Baada ya ku will kuwa uko tayari kuwafuata, powers of will hutafuta sababu yoyote ya kukuchomoa, kikawaida ikikosekana sababu yoyote, iwe ni ugonjwa wa ghafla, ajali, or majanga yoyote ya kuondoa roho, then mtu alikuwa ni mzima, analala usingizini, kesho yake haamki. Pamoja na uwepo wa hiyo bond, ili kumfuata aliyetangulia ni lazima will yako ikubali.

Hitimisho.
Kwa vile kwa sisi binadamu wote hapa duniani tuko safari tuu, kuelekea kwenye maisha ya milele, tusiwalilie waliotangulia na kuhuzunika saana kwa kuwakosa, tuhunike kibinaadamu, tulie kwa kiasi, maisha ni lazima yaendelee, bali tujiangalie sisi wenyewe, kwa nafsi zetu, jee tumejiandaa kuitika wito wakati siku yetu na saa yetu ikitakapofika?.

Kesheni mkiomba kwa maana hamjui siku wala saa.
RIP Ephraim Kibonde na Ruge Mutahaba na wengine wote waliotangulia, nyinyi mbele sisi tuko nyuma yenu, sote sisi ni wa Kwake na Kwake tutarejea.

Paskali
Rejea
Life after Death: What Happens after Death? - JamiiForums

Psychic Powers: Ni Nguvu za Kufanya Miujiza. Wengi wanazo bila kujitambua. Je, Wewe Unazo? - JamiiForums

"Will Powers!", "Faith Healing!"-Nguvu za Kufanya Miujiza Ya Uponyaji kwa Imani!. -Kila Mtu Anazo! - JamiiForums

Life After Life: Regia Mtema (RIP) Amerejea Bungeni Kiaina? - JamiiForums
 
Wanabodi,
Kifo cha Ephraim Kibonde kimeibua simanzi kubwa kwa sababu katika uhai wake hakuwahi kuugua, amekufa ghafla, hivyo watu kubaki na maswali mengi.
Katika bandiko la Tribute to Kibonde, kuna mwana JF kaandika maneno haya kumhusu Kibonde.

Kufuatia kuyasoma hayo, nimeona nizungumze kitu kuhusu uhai, kifo na maisha baada ya kifo.

Uhai ni Nini na Kifo ni Nini?.
Mwili wa binadamu una sehemu mbili, sehemu ya kwanza ni huu mwili wa nyama, ambao umeumbwa kwa mavumbi, na siku ukifa, kinachokufa ni mwili huu wa nyama, unazikwa kaburini, humo ndani unaoza na kurudi kuwa mavumbi. Sehemu ya pili ya mwili ni uhai, uhai hii ni pumzi Mungu aliyoipulizia kwenye ule udongo hivyo mwili kupata uhai. Hii ni Roho ya Mungu, the spiritual body, the astra body, mwili unapokufa, roho haifi, bali huacha mwili na kurudi kwa Mungu. Hivyo kifo ni kitendo cha roho kuacha mwili.

Jee Baada ya Kifo, hiyo Roho inakwenda Kuishi Wapi?.
Kama ulivyo mwili una sehemu mbili ya mwili wa nyama na mwili wa roho, vivyo hivyo dunia ina sehemu mbili, Ulimwengu wa Kidunia, the physical world, na Ulimwengu wa Roho, the Spiritual World, mtu akifa, roho ikiacha mwili, mwili unabaki kwenye ulimwengu wa dunia, unazikwa unaoza na kugeuka kuwa mavumbi, Roho inakwenda kwenye ulimwengu wa Roho kuendeleo kuishi milele, being mbinguni, peponi, kuzimu, toharani, au jehanum kwenye moto wa milele, hii subject nyingine lakini roho hazifi kwa sababu roho ni Mungu.

Jee Roho za Waliokufa Zinaweza Kuwaita Walio Hai?.
Jibu ni yes, ndio maana kwa baadhi ya mila, wamama wajawazito hawaruhusiwi kwenda makaburini, ili waliolala wasije wakaviita vichanga, na matokeo yake vikaitika na kupata still born.
Kwenye mahusiano kuna kitu kinaitwa Soul Mates, na hii ndio subject matter ya uzi wangu huu.

Mahusiano ya Mapenzi, ya Aina Tatu, Kuna Mapenzi ya Mwili, Ya Raha na Mapenzi ya Roho ambayo Ndio Mapenzi ya Kweli.
Kama ulivyo mwili una mwili wa nyama, na mwili wa roho, vivyo hivyo kwenye mapenzi, kuna mapenzi ya mwili, physical love, na mapenzi ya moyo, spiritual love, emotional love.
Mapenzi ya physical love, ni yale mapenzi ya mambo ya mwilini, yanajumuisha mapenzi ya kutamani mwili na kufanya lile tendo la sex, sometimes ni needs, tamaa, infatuation, kila kiumbe mwenye viungo timilifu vya uzazi, anaweza kufanya physical love na kuridhika na tendo na kutoshesha mechanically, lakini hakuna emotional na spiritual love, na hiki ndicho mara nyingi hufanyika kwenye biashara ya mapenzi, wale wadada wanaojiuza, hufanya physical love tuu kwa uhitaji wa pesa, lakini hakuna emotional love wala spiritual love.

Mapenzi ya Kweli ni zaidi ya Sex, ni Emotional na Spiritual.
Ili kupata mpenzi wa kweli na kufanya mapenzi ya kwenzi, yule mpenzi unaekutana nae lazima awe ndie soul mate wako. Yaani mtu uliyeumbiwa wewe kuwa parner wako wa maisha ya kimwili na kiroho, hivyo mkifanya sex, sio tuu mnafanya tendo, bali mnaunganika na kuwa mwili mmoja in spiritual body, hivyo mahusiano ya hivi, mmoja akitangulia, yule aliyebaki duniani hawezi kuishi muda mrefu, atamfuata tuu mwenzake, na mapenzi yao yataendelea kwenye the spiritual world.

Je Utajuaje Mpenzi Uliyenae Kama Ndie Soul Mate Wako?.
Haya sasa ni mambo ya Roho, naomba nisiyazungumze hapa.

Roho za Wafu, Zinaweza Kuziita Roho za Walio Hai Au Walio Hai, Wakajipeleka Wenyewe Kifoni.
Watu walikufa ambao roho zao zinaishi kwenye ulimwengu wa Roho, wanaweza kuwaita watu wowote wenye strong bond nao, kutoka duniani na kuwafuata kifoni, wengi wa watu wanaitwa kwa namna hii, hufa ghafla. Wengi ni pale mmoja anapotangulia, mwingine hawezi ku recover hivyo ni ama ni yeye mwenyewe aliye hai anaona maisha bila ya mwenzake hayana maana, hivyo kutamani kumfuata, ama aliyekufa anamuita mwenza wake kifoni, hivyo mwenza kumfuata.

Hivyo kama ni kweli Ephraim Kibonde alisema mke wake ni soul mate wake, usikute Ruge ndio alikuwa kila kitu kwa Ephraim Kibonde, hivyo baada ya kifo cha mke wake, Ephraim aliweza kuendelea kuishi kwa vile Ruge yupo, ilipotokea Ruge amekufa, katika kuushughulikia msiba huo, roho ya Ruge na Roho ya Mke wa Kibonde, zikakutana na kumuita Ephraim kuwa sisi tuko huku, wewe huko unangoja nini?, hivyo Roho ya Ephrain=m, ikasikia saiti hizo, na yeye mwenyewe ku will, kuwa nitawafuata. Baada ya ku will kuwa uko tayari kuwafuata, powers of will hutafuta sababu yoyote ya kukuchomoa, kikawaida ikikosekana sababu yoyote, iwe ni ugonjwa wa ghafla, ajali, or majanga yoyote ya kuondoa roho, then mtu alikuwa ni mzima, analala usingizini, kesho yake haamki.

Hitimisho.
Kwa vile kwa sisi binadamu wote hapa duniani tuko safari tuu, kuelekea kwenye maisha ya milele, tusiwalilie waliotangulia na kuhuzunika kuwa kosa, bali tujiangalie sisi wenyewe, jee tumejiandaa kuitika wito wakati siku yetu na saa yetu ikitakapofika?.

Kesheni mkiomba kwa maana hamjui siku wala saa.
RIP Ephraim Kibonde na Ruge Mutahaba na wengine wote waliotangulia, nyinyi mbele sisi tuko nyuma yenu, sote sisi ni kwake tutarejea.

Paskali
Pascal hapo ulipoanza kusema roho ni mungu umenifanya niache kusoma uzi wote..
 
Mkuu Pascal umeandika mada ngumu sana leo, japo umejitahidi ionekane rahisi.

Kuna kitu umeandika kwa kufumbia fumbia kinaitwa majeshi ya wafu...
Hiki ndicho hasa kinachosumbua familia nyingi za Kiafrika, na huenda hata Kibonde.
Kimsingi ni ushetani tu.
 
Siamini hayo mambo, mtu akishakufa hahusiki kwa namna yoyote na kinachoendelea duniani. Kinachotokea ni kuwa walio hai ndio wanaojenga hisia kuwa wafu wanaweza kufanya kitu kibaya au kizuri katika maisha yao ya hapa duniani, na mara zote fikra zako ndo matokeo kwako.
Kitu kingine ni kuwa, jiulize kwa nini kuna wajane wengi kuliko wagane....
 
Mkuu pascal umeandika kitu kizoto sana japo kimejaa mikanganyiko mingi sana.Unasema mtu akifa mwili hubaki duniani(physical world) na roho huenda kuishi katika spiritual world ambako huko haifi milele.

Unataka kusema wale wote waliokufa na watakaokufa badae wote wataishi huko vipi kuhusu hizo roho zinaweza kuishi bila miili.

iPhone 7plus
 
Siamini hayo mambo, mtu akiila mwenyewhakufa hahusiki kwa namna yoyote na kinachoendelea duniani. Kinachotokea ni kuwa walio hai ndio wanaojenga hisia kuwa wafu wanaweza kufanya kitu kibaya au kizuri katika maisha yao ya hapa duniani, na mara zote fikra zako ndo matokeo kwako.
Kitu kingine ni kuwa, jiulize kwa nini kuna wajane wengi kuliko wagane....
Mkuu kutokuamini kwakp hakufanyi hilo jambo lisiwepo.
Wapo wasioamini ukimwi upo Ila waju upo. Wapo wasio amini kuna uchawi nk nk
 
Mkuu kutokuamini kwakp hakufanyi hilo jambo lisiwepo.
Wapo wasioamini ukimwi upo Ila waju upo. Wapo wasio amini kuna uchawi nk nk
Unajua sisi binadamu tuna shida moja, huwa hatuwezi kukubali kuwa kuna jambo fulani hatuwezi kulitolea ufafanuzi na hivyo huwa tunalazimisha kujipa majibu ambayo kwa namna moja ama nyingine yanatufariji na kufanya hata tufurahie maisha au kutatua maswali ambayo mwanzo yalikuwa yanatutatiza. Hivyo ndivyo tulivyo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom