Lifanyike Hili Kwa Maslahi ya Nchi!

Wateule

JF-Expert Member
Sep 17, 2010
390
368
Katiba imezuia marais wastaafu wasishtakiwe, lakini sio wasijadiliwe. Tena majadiliano muhimu, ambayo yamejikita kuangalia uwezekano wa kuondoa kinga, ili wafikishwe mahakamani kutoa maelezo zaidi. Binafsi, sioni lazima wafungwe (kwani hili lina mazingira magumu sana), lakini wakikutwa na hatia watuombe msamaha watanzania kwa ubinafsi wao na tusonge mbele kama taifa.

Lakini, kinga ya rais kutoshtakiwa iondolewe kwenye hiyo katiba mpya, ili marais wajao (akiwemo na Magufuli wa sasa) wawe na hofu na heshima juu ya mali za Watanzania. Akisimamia hili, Magufuli atakuwa amefanya la maana sana kwa nchi yake, kwani atakuwa ametusafishia njia kwa siku za usoni na pia hatokuwa na mtihani mgumu wa kulazimika kuwashtaki na pengine kuwafunga marais waliomtangulia. Hata utawala wa Waafrika ulivyofanikiwa kushika dola kule South Afrika, hawakuhubiri kuwakamata wazungu waliowatesa nchini mwao na kuwafunga au kuwaua, bali waliunda tume ya "Maelewano na Mapatano" ili kusameheyana kwa yaliyopita na kusonga mbele.

Na sisi Watanzania tuwe wepesi wa kukubali kusamehe na kusonga mbele baada ya majadiliano kufanyika. Utaratibu wa sasa wa kuwatisha watu wasiwajadili marais wastaafu ambao ni dhahiri wamehusika kwa njia moja au nyingine katika ubadhirifu huu mkubwa wa mali za Watanzania, sio mzuri na hauna mwisho mwema. Kuendelea kutisha watu hakumpi sifa Magufuli ya u "hero" kama anavyotaka, na badala yake kunamfanya aonekane mtu aliyedandia basi bila kujua linapoelekea.
 
Umeandika vema sana ila umeharibu hapo uliposema WATANZANIA TUSAMEHE NA KUSONGA MBELE...kwa akili yako unaweza msamehe mtu ambae haoneshi hata chembe ya kujudia kosa lake...!!!!Acha mambo ya uoga na siasa za ajabu
 
Umeandika vema sana ila umeharibu hapo uliposema WATANZANIA TUSAMEHE NA KUSONGA MBELE...kwa akili yako unaweza msamehe mtu ambae haoneshi hata chembe ya kujudia kosa lake...!!!!Acha mambo ya uoga na siasa za ajabu

Haujasoma vizuri ndugu yangu, punguza jazba. Nimesema tusamehe na kusonga mbele baada ya majadiliano kufanyika. Yaani tusitishwe juu ya kuwajadili marais hawa na wao wahojiwe na wakiri makosa yao ndio na sisi tunasamehe na kusonga mbele. Tofauti na hivyo, ni geresha tu anayofanya Magufuli. Hawa hawawezi kuonyesha "chembe ya kujutia kosa" kwasababu sasa hivi Magufuli anawalinda, na mimi ndio nasema aache hizo...avute tu taulo na sisi tukabiliane nao...
 
Back
Top Bottom