paul sylvester
JF-Expert Member
- Mar 18, 2020
- 3,504
- 3,499
Hii hoja haijawalenga Sana wale wenzangu na mimi ambao Wao wamechanjwa chale za vyama vyao
Sasa karibu katika mjadara!
Najua kuna wale ambao liwe jua ama mvua Wao ni CCM Tu, lakini kuna wengine ambao hata ukimwamsha usiku wa manane Kutokea usingizini umuulize, wewe ni Chama gani, atakujibu huku akipiga miayo ya usingizini kuwa yeye ni CHADEMA tu
Siyo vibaya kuwa mwanachama wa kudumu, lakini nikutahadharishe kuwa, huwenda ndio sababu za Watanzania wengi kuwa masikini wa kutupwa ili Hali watu wachache wakineemeka na utajiri wa Taifa letu
Mawazo yangu ni ingelikuwa kheri iwe hivyo Kwa viongozi tu wa vyama kuwa wanachama wa kudumu Ila raia tukawa tuko katikati,
Nahisi kwamba, kuendekeza uvyama na kung'ang'ania mavyama badala ya kuchagua viongozi Bora tu Kutokea Chama chochote kile, ndio sababu pia ya umasikini tulionao wengi,
Yaani uchaguzi kama huu, tungelifanya upembuzi wa kuchagua mayai yote tokea Chama chochote na sio mayai viza eti tu Kwa sababu linatokea Chama chako,
Wagombea nafasi ya urais, ukiiruhusu nafsi yako itawale ukweli wa moyo wako, utakubaliana na mimi kwamba, wote ni vifaaa, mayai haswaa, majembe haswaa, wapambanaji na wasiokubali kushindwa kirahisi, wote ni majasiri na wapambanaji, wote wanakiu ya kutupeleka mahali, tofauti zao ni ndogo saana,
Ni ndogo Kwa sababu, watu hawawezi kufanana Kwa kila kitu,
Kuzidiana huko, ndio kunatufanya kila mmoja aseme, atampa furani Kura yake, nikiwemo na Mimi, na niseme wazi kuwa, Kura yangu nitampa Magufuli, ingawa msimamo wangu haupo katika Chama, napenda mtu Bora, Jasiri asiyeogopa, na hata Mungu Baada ya Musa kufa, alimwambia Joshua kuwa, awaongoze Israel kwenda Kanani, asigeuke nyuma Wala asiogope, Kwa kuwa Mtu Jasiri ndio sifa ya Ushindi,
Sasa basi, Kwa kuwa tuna watu mashuhuri hasa hao wawili pekee, Kwa maana ya Mh Lisu na Mh Magufuli, na ijapokuwa mmoja hasa Mh Lisu ndiye atakaye shindwa" na kushindwa kwake si Kwa sababu ni hatufai kutuongoza, hapana, anashindwa tu Kwa sababu ni lazima katika kushindana awepo mshindi na mshindwa
Sasa basi, hawa majemedari wa nyakati za leo, Sisi Watanzania, tuwalazimishe wafanye kazi pamoja,
Kama Magufuli akiwa ndiye Rais, Waziri Mkuu awe ni Mh Lisu, hiyo isiwe ombi kwao,
Kama ni kuandamana kama nchi ili kuwashinikiza wafanye kazi pamoja, basi tuwe na maandamano yasiyokoma,
Tanzania inamhitaji Magufuli na inamhitaji Lissu pia, na Mungu amewaleta Kwa wakati mmoja na wakati utufaao Sisi kama nchi
Toa maoni yako, Matusi ni kukosa hekima