Licha ya kukimbia kero nyumbani, anaapa kamwe hatamuacha mkewe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Licha ya kukimbia kero nyumbani, anaapa kamwe hatamuacha mkewe

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mbunge wa CCM, Dec 15, 2009.

 1. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #1
  Dec 15, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waungwana,
  Kuna mwanaume mmoja aliyefanikiwa kimaisha kwa kiasi cha kuridhisha, alinisimulia kisa chake kikanisikitisha sana.

  Alipokuwa anatafuta mchumba wa kuoa, bila kutarajia alipata maradhi mabaya ya mfumo wa uzazi yaliyopelekea kufanyiwa upasuaji katika taasisi ya mifupa muhimbili (MOI). Kwa mujibu wa madaktari, kulikuwa na uwezekano mdogo sana wa kupata watoto maishani mwke.
  Hii haikuwa habari nzuri kwake, akachanganyikiwa, akaazimia kuwa lazima apate motto/mimba haraka iwezekanavyo hata kabla hajapona upasuaji aliofanyiwa!

  Ndio, alikurupuka akaongea na binti mmoja waliyekutana nae kwa jirani yake suku za nyuma na ambaye hakupata kuwa mpenzi wake kabla, amsaidie kumzalia motto angalau wa kumbukumbu ya maisha yake, na yeye yuko tayari kwa lolote. Binti alimpa sharti la kumuoa, akakubali kama kufumba na kufumbua na kumtaka siku hiyohiyo apeleke taarifa kwao na ikawa hivyo.

  siku hiyohiyo wakakutana kitandani Yule bwana akiwa bado kafungwa bandeji sehemu nyeti alikofanyiwa upasuaji na kwa kukiuka ushauri wa madaktari wake waliomzua kufanya ngono hadi watakaridhika kuwa afya yake imetengemaa, wakafanya shughuli kwa uangalifu mkubwa kuzuia asitoneshwe na waliendelea hivyo hadi walipopata walichokuwa wakikitafuta yaani mimba. ndoa ikafungwa, mtoto akazaliwa, mume akashusha pumzi kwa shukrani

  Kabla ya mwaka mmoja wa ndoa maisha yakabadilika. Kila wanapopishana jambo, mwanamke anatishia kuwa atatoa siri yake na kujiua yeye pamoja na mtoto kwani anasema hawezi kufa peke yake akamuacha mwanae alelewe na mwanmke mwingine. ugomvi ukavuka mipaka ya nyumba yao, ukafika kazini, polisi, ustawi wa jamii, mahakamani, yaani kila mahali. Wakawa vituko mbele za watu
  Huku akimpenda mwanae kupita kiasi, visa navyo viliongezeka. Akaamua kupanga chumba maeneo ya magomeni. Kila akichoka kero za mkewe, anaaga kuwa kasafiri kikazi na kujipunzisha hadi wiki moja kwenye chumba chake cha kupanga kisha anarudi kumwona mwanae.

  Anaongeza kuwa hatamuacha mwanamke huyo kamwe licha ya visa vyote anavyomtendea kwa kuheshimu jinsi alivyompa faraja pale alipokubali kuzaa nae wakati ambapo alianza kupoteza matumani ya kuwa baba wa mtu maishani wake.

  niliposikia habari zake kwanza nilimhurumia nikamtafuta nizungumze nae kuangalia kama kama naweza kumsaidia. Tunaendelea na mashauriano na wote wawili wanatoa ushirikiano wa kutosha,
  mnawashauri nini hawa?
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Dec 15, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  </p>
  Mbona ghafla mambo yameenda mbali namna hii....Kwanini kuongelea habari za kujiua? .. Kuna kisa kikubwa sana hapa ambacho UMEKIRUKA..hujasimulia...PIA NINACHOSHINDWA KUELEWA, KWANINI HUYO MWANAMKE ASEME ATATOA SIRI,,kuna siri gani?..maana kama ni ile ishu ya ku'do huku akiwa na mabandeji kwenye naniliu, mi sioni kama ni siri ya tishio kihivo!.....Iko kitu hapa...N/W/Searching~~~~~~~~~~~~~~~~~</p>
   
 3. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #3
  Dec 15, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mi nilivyoongea nao ,sikuona kosa kubwa la mtu kutishia kujiua. nilichokiona ni kuwa mama alitaka kumfunga mzee mdomo, hivyo ilikuwa kama kutishia nyau! nasema hivyo kwa sababu kabla mama hajakubali kukutana na mimi niliwahi kumshauri mzee kupuuza tishio hilo na asimamie suala lolote analoamini kuwa sawa, baada ya mama kuona mzee hatishiki tena na tishio lake, ndio akaanza kusemasema ovyo nje kuhusu kila wanchogombania huku akimkomoa kwa kufika kazini mara kwa mara na mwanae kwa kisingizio cha kufuata matumizi hata pale ambapo ameishaachiwa matumizi nyumbani!

  siri anayotishia kutoa ni kuhusu maumbile ya mzee, kwani yalibadilika baada ya upasuaji. naona ni upungufu tu wa hekima kumnyanyapaa mwenzi wake kwa matatizo ua ugonjwa!
   
 4. c

  compressor Member

  #4
  Dec 15, 2009
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ilikuwa ni mtoto mapatano yao,mtoto ndo kashapatikana,baba hana mapenzi na mama,na mama hana mapenzi na baba.na hiyo njemba inampenda mwanae tu na si mkewe.mi nadhani ushauri mzuri ambao utakuwa na faida kwao ni kuwashauri hawa watu wajifunze kupendana kazi ambayo ni ngumu sana tena sana.kwa sababu kaz hiyo ni ngumu ni vyema wafanye kitu rahisi ambacho ni kuachana.kuna namna nyingi ya kulipa hisani si lazima kumng'ang'ania mtu ambae humpendi na yeye hakupendi.mwache aende zake.inaelekea vituko vinakuja kwa kuwa huyo mwanamama kashaona mapenzi hakuna baada ya njemba kupata alichotaka.
   
 5. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #5
  Dec 15, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mimi naona tofauti kidogo mkuu

  kwa kuwa tatizo ni tabia, linaweza kurekebishwa na ushauri nasaha, tabia hubadilika na naamini hata huyu mama atabadilika. pia naona kuwa mapenzi yapo, na commitment pia zipo za kutosha.

  naona baba anafanya vyema kuheshmu wema wa mama na ni hii hii heshima ndiyo itakayomleta mama miguuni kwa baba kuomba msamaha siku moja, ni suala la muda tu ndugu yangu. na watu hawa bado wako kwenye mchakato wa kujenga mapenzi na kuheshimiana. kumbuka walifunga ndoa chini ya shinikizo la kimaumbile, kwa hiyo hawajawahi kupendana kwa dhati hadi nyoyo zao zikaridhika na sasa ndio wanajenga mapenzi wakiwa tayari na mtoto. naamini huyu mtoto atayakoleza zaidi mapenzi yao pindi yatakapoanza.
   
 6. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #6
  Dec 15, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Huenda huyo mwanamke anadhani anaweza kum-blackmail jamaa. Kwani kuna maumbile mazuri ya kike au kiume? Kama huyo bwana aliweza kumega mpaka kumpa ujauzito hapo hata akitoa hiyo siri namwambia we toa tu sioni kama kuna tatizo..
   
 7. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #7
  Dec 15, 2009
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  hii khabbar ni kweli? jamaa kapindua serikali na mabendeji afta kupasuliwa?
  huyu jamaa anaitwaje? huyu ni shujaa na inabidi japo barabara moja hapa bongo tuipe jina la shujaa huyu.
   
 8. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #8
  Dec 15, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hahahahaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!!!!

  nalifikiria wazo lako mkuu.

  lakini siku zote nakumbusha kuwa usifanye mchezo na vita ya kisaikolojia, unaweza kufanya jambo ukamwacha kila mtu kinywa wazi!!!!!!!!!!!!!

  huyu jamaa alikuwa atika vita kali na saikolojia yake
   
 9. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #9
  Dec 15, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kimsingi, mimi binafsi sioni siri hapo! kwani nani asiyejua ugonjwa, au nani asiyejua maumbile yoyote hata mguu ukifanyiwa upasuaji mkubwa waweza kubadilika maumbile, sembuse nanihii????

  ndio maana moja ya ushauri wangu kwake ni kupuuza hofu hiyo ya siri na tishio la mama kwa mtoto
   
 10. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #10
  Dec 15, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  hivi wewe ulisoma IJMC?
   
 11. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #11
  Dec 15, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  man, you need time to understand higher issues!!!!!!!!!!!
   
 12. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #12
  Dec 15, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  eeh!jibu swali ww
   
 13. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #13
  Dec 15, 2009
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Huyo mama hana cha kumtisha huyo bwana, hofu kubwa ni hapo tu anasema kujiua na kuua mtoto. Hakuna siri dunia hii yeyote anaweza pata maradhi, mbona kuna watu wengi sana wako ndani ya ndoa hawana watoto na wake au waumeza zao hawana vitisho.

  Tatizo la huyo bwana hakuangalia nani apate ane mtoto kwa wakati ule. Wanawake wengine ni Primitive especially unapowambia ukweli kuhusu yanayokusibu. Hatuna subira wala nini tunavehave differently. Huyo bwana akaze uzi tu, akitishiwa aende zake magomeni akirudi mambo shwari. Aombe Mungu amuonyeshe njia, kama anatishia kuua mtoto ni police case, apimwe akili anayang'anywe mtoto au aache vitisho.
   
 14. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #14
  Dec 15, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  sasa huyu mama ajiue sababu ya nini? mbona mie sioni cri hapo....ndoa zina majaribu jamani, na huyu baba kinachomuhamisha kwake ni nini?....mgombea ubunge samahani ni visa gani huyu mama anavifanya kwa huyu baba mpaka ahame kwake wiki nzima?
   
 15. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #15
  Dec 15, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kuna visa vingi sana na thread nimeifupisha tu, vipo vinavyohusu simu, housegirl wao, jirani yake mmoja, ndugu za mkewe wanaokaa pale, mashoga zake wa barabarani nk. mfano kuna siku amepiga mlango kwa mawe usiku mzima kumshinikiza akiri kuwa anatembea na jirani yao mmoja na haikuwa kweli, siku nymingine kamkuta ananunua bidhaa dukani akamshambulia kwa mawe hadi akamjeruhi mkono kwa sababu amepitia dukani kabla hajafika nyumbani nk. ni visa vingo sana
   
 16. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #16
  Dec 15, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni kweli mambo haya yameishawafikisha polisi, ustaw wa jamii mahakamani nk. mimi niliwashauri waondoe shauri lao huko kwenye vyombo vya sheria tuliangalie kijamii zaidi, walikubali na tunaendelea na mazungumzo vizuri
   
Loading...