konda msafi
JF-Expert Member
- Sep 5, 2018
- 1,666
- 8,582
Kwa kweli nimejikuta nampenda Magufuli ghafla. CCM ndio imetufikisha hapa tulipo lakini kwa jinsi alivyowachana hawa mafisadi wa hela za wafanyakazi amenifanya nipate imani juu ya utendaji wake.
Kama ningekuwa na uwezo wa kumuomba Mwenyezi Mungu na akatekeleza maombi yangu, ningemuomba wapinzani wote wa Tanzania wamsamehe rais chochote kile ambacho wanadhani anahusika.
Na yeye rais awasamehe kwa yote waliyomkosea na ningemuomba kesi zote zilizopo mahakamani dhidi ya wapinzani zisizokuwa na kichwa wala miguu azifute (kama anayo hayo mamlaka). Pia ningeomba ushirikano kati ya Tanzania na jumuia ya kimataifa uimarishwe kwa ajili ya maslahi mapama ya nchi. Tuungane tujenge Tanzania moja. Hakuna sababu ya kupingana ilihali wote tunajenga taifa moja.
Ningeomba viongozi wote wa upinzani wafanye kazi pamoja na serikali kwa manufaa ya taifa. Kama inawezekana wakina Tundu Lisu, Freeman Mbowe, John Mnyika, Godbless Lema na wapinzani wengine wenye uwezo na wawajibikaji wapewa nyadhifa serikalini. Wasameheane, wajenge Tanzania moja. Umoja wa kitaifa uanzie kwa viongozi wetu wa vyama na serikali ushuke hadi huku chini kwa raia wa kawaida.
Kwa kweli Magufuli ameongea ukweli kabisa tena kwa kupiga mulemule. Tunahitaji rais wa namna hii, anayejua kero na matakwa ya raia wake. Kila mtu anajua hakuna mkamilifu chini ya jua.
Hivyo rais ni binadamu kama mimi na wewe, anaweza kukosea pia. Hivyo tuangalie mazuri yake. Leo kawasemea wafanyakazi vizuri sana.