Libya yakataa kulipa fidia kwa waathirika wa Mabomu ya IRA

Hofstede

JF-Expert Member
Jul 15, 2007
3,577
1,107
Mwanawe rais wa Libya Kanali Muamar Gaddafi amesema nchi yake itapinga vikali uamuzi wa kuwalipa fidia familia za watu waliouwawa kwenye mashambulio ya mabomu yaliyotekelezwa na kundi la IRA.

Vifaa vya kutengeneza mabomu hayo vilitoka nchini Libya.
Akijibu tangazo la uingereza kuwa itawasaidia waathiriwa wa mashambulio hayo katika harakati zao za kutaka haki itendeke kwa waliotekeleza mashambulio hayo, Bwana Gaddafi amesema Libya haiwezi kukubali uamuzi huo na kusema ni mahakama tu, ambayo inaweza kutoa uamuzi kama huo.
Tangazo la Libya limejiri baada ya shutuma kutoka kwa makundi mbali mbali kuwa Uingereza haitaki kusaidia familia za waathiriwa wa mashambulio hayo ili kutoharibu uhusiano wake wa kibiashara na Libya.
Hata hivyo serikali ya uingereza imekanusha madai hayo.
Zaidi ya watu mia moja waliathirika kutokana na ghasia za kundi la IRA miaka ya 80 na 90 na wamekuwa wakiitaka serikali ya Libya kuwalipa fidia.
Bwana Brown amesema jopo la kutoka wizara ya mambo ya ndani litawasaidia wale wanaotaka kulipwa fidia.

My take: Hii sasa ni aibu kubwa sana kwa Uingereza yaani baada ya kuona waathirika wa Lockerbie bombed plane wamelipwa fidia basi sasa hivi wanaona kuwa Libya ina hela za kumwaga. Je na wapelestina nao wakisema marekani iwalipe kutokana na mashambulizi ya Islael yanayotokana na silaha zilizotokea Marekani, Vivyo hivyo Iraq, Afghanistan na maeneo yote yenye vurugu ni nani atanusurika?.

Hii ni aibu kubwa kwa nchi zilizoendelea kulazimisha fidia kwa nchi ya Afrika kisa tu wanahazina ya mafuta. LOL!!
 
Uingereza nao waanze kuwalipa waanga wa Mau Mau, na nchi zote walizo zitawala nazo zilipwe fidia kwa kudhalilishwa na kubaguliwa ikiwemo Ireland. Kisha ndio iwageukie wengine kutafuta kulipwa fidia... sic
 
Back
Top Bottom