Libya: Waziri Mkuu aonya kutokea kwa mgogoro baada ya miundombinu ya mafuta kufungwa

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Waziri mkuu wa Libya Fayez al-Serraj anayeongoza serikali inayoungwa mkono na jumuiya ya kimataifa amesema kufungwa kwa miundombinu ya mafuta nchini humo kutasababisha mgogoro mkubwa wa kifedha.

Akizungumza na waandishi habari mjini Tripoli, Al-Serraj amesema hasara iliyokwishapatikana kutokana na kufungwa miundombinu hiyo ni zaidi ya dola bilioni 1.4 na tarakimu hizo zinaongezeka.

Mnamo mwezi Januari Waandamanaji tiifu kwa mbabe wa kivita Khalifa Haftar aliye hasimu wa serikali ya Al-Farraj waliyafunga mabomba na bandari za kusafirishia mafuta hatua iliyopunguza uzalishaji na usafirishaji nje bidhaa hiyo.

Al- Sarrij amesema kuendelea kufungwa vituo hivyo tayari kumeleta athari kwa bajeti ya serikali ambayo kwa mwaka huu itakabiliwa na nakisi.

Usafirishaji nje wa mafuta ni chanzo kikuu cha mapato nchini Libya, taifa amablo limetumbukia kwenye machafuko tangu kuuwawa kwa aliyekuwa kiongozi wa muda mrefu Muammar Ghadafi mwaka 2011.
 
Gaddafi and islamization of Africa kwa mgongo wa utajiri wa mafuta! Go to hell.
 
Ni lazima keki ya taifa igawanywe sawa kwa utaratibu maalum huduma za afya elimu chakula na malazi...lakini mkiendelea kujineemesha ktk kikundi kidogo mlichokitengeneza mkila kwa niaba ya yetu, ni Bora kinuke kukitulia tutaheshimiana.....kazi yenu kusifia tu ili kulinda ulaji wenu wakati watanzania wanazidi kuwa na Hali ngumu haikubaliki hata kidogo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Poleni Libya maana "majuto ni mjukuu"
Mzungu ajawahi mpenda mtu mweusi na awezi kumuacha salama ndicho akina zitto na genge lake wanakitafta kwa tanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wa-Libya wataendelea kupata "Mavuno" ya walichokipanda kwa mikono yao wenyewe, wakisaidiwa na watu wa mataifa ya kishetani.
Hiki ndicho Zitto na wenzake wanatamani kiipate Tanzania.
Hvi watanzania reasoning zetu zimeenda wapi kila kitu tunaongozwa na hisia. Kilichoimaliza Libya sio kumtoa Gadaffi ila VITA yaani kama Gadaffi angepisha kwa amani tu kama Mubarak nchi isingechafuka.

Nikumbushe tu hata Hitler aliifanya ujerumani kuwa moja ya taifa lenye mkubwa zaidi ulaya ila alipotolewa ujerumani iliharibiwa sana kiuchumi na kimiundombinu je nao walikosea kumtoa Hitler? Idd Amin alipokua Rais uganda ilipaa kiuchumi kuliko wakati wowote ule Je nyerere alipomtoa mnafahamu nchi haikutawalika tena na uchumi ukafa Je alifanya makosa kumtoa??

Jamani madhara ya vita huwa hayaangalii sababu za vita, kwahiyo hapa wa kulaumiwa ni Gadaffi sababu aligoma kung'ooka kwa amani kama wenzie wa Tunisia au Algeria
 
Angalau wewe Zitto unapakukimbilia in case kukitokea Vita. Je, umewahi kuwaza Bibi yangu wa Kalenge na Kidahwe watajificha wapi siku mkiivuruga amani ya nchi hii kwa uroho wenu wa madaraka? Simkubali Anko Magu na nikir nimekuwa mfuas wa Zitto wa Muda Mrefu, lakin kwa uelekeo uliochukua hasa baada ya usajili wa Maalim Seif na team yake, nimeanza kupata mashaka na Uzalendo wako. Mungu anisaidie nisiwe nakuwazia opposite.
 
Back
Top Bottom