beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,877
- 6,326
Waziri mkuu wa Libya Fayez al-Serraj anayeongoza serikali inayoungwa mkono na jumuiya ya kimataifa amesema kufungwa kwa miundombinu ya mafuta nchini humo kutasababisha mgogoro mkubwa wa kifedha.
Akizungumza na waandishi habari mjini Tripoli, Al-Serraj amesema hasara iliyokwishapatikana kutokana na kufungwa miundombinu hiyo ni zaidi ya dola bilioni 1.4 na tarakimu hizo zinaongezeka.
Mnamo mwezi Januari Waandamanaji tiifu kwa mbabe wa kivita Khalifa Haftar aliye hasimu wa serikali ya Al-Farraj waliyafunga mabomba na bandari za kusafirishia mafuta hatua iliyopunguza uzalishaji na usafirishaji nje bidhaa hiyo.
Al- Sarrij amesema kuendelea kufungwa vituo hivyo tayari kumeleta athari kwa bajeti ya serikali ambayo kwa mwaka huu itakabiliwa na nakisi.
Usafirishaji nje wa mafuta ni chanzo kikuu cha mapato nchini Libya, taifa amablo limetumbukia kwenye machafuko tangu kuuwawa kwa aliyekuwa kiongozi wa muda mrefu Muammar Ghadafi mwaka 2011.