Liberia President, George Weah declares free tuition in all public universities

Ni hatua nzuri na muhimu zaidi kwao. Hata hivyo hatuwezi kuiga kila kitu kutoka kwa wenzetu kutokana na sababu za hapa na pale.
 
Rais George Weah wa Liberia jana ametangaza kufuta ada kwa vyuo vikuu vyote vya umma nchini humo kwa wanafunzi wa shahada ya kwanza (undergraduate). Pia ameeleza kuwa serikali yake inapanga kutoa ruzuku kwa vyuo vikuu binafsi ili kuvipa unafuu viweze kupunguza ada kwa wanafunzi wanaosoma vyuo hivyo.

Liberia ina vyuo vikuu 9 vya umma na 10 vya binafsi ambavyo vingi vinamilikiwa na mashirika ya dini. Liberia imekuwa nchi ya kwanza barani Afrika kufuta kabisa ada kwa wanafunzi elimu ya juu, licha ya kupigana vita ya wenyewe kwa wenyewe kwa karibu miaka 20 iliyoharibu kabisa uchumi wa nchi hiyo.

Rais Ellen Johnson Sirleaf aliyeingia madarakani mwaka 2006 alianza kuisuka upya nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika inayotegemea madini, uvuvi na mazao ya misitu kuendesha uchumi wake.

Kwa kipindi cha miaka michache tangu kukoma kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchi hiyo imepiga hatua kubwa kimaendeleo na kuzizidi nchi nyingi zilizokuwa na amani ikiwemo Tanzania.

Kwa mfano waka 1990 wakati nchi hiyo ikiwa katika vita, shilingi moja ya Tanzania ilikua sawa na dola 65 za Liberia. Lakini kwa sasa Dola 1 ya Liberia ni sawa na shilingi 14.6 za Tanzania. That means sarafu yao imezidi kuimarika siku hadi siku na yetu ikizidi kuporomoka mara dufu.

Rais Weah ametoa rai kwa nchi nyingine za Afrika kufuta ada kwa vyuo vikuu vya umma na kutoa ruzuku kwa vyuo vikuu binafsi ili kupunguza gharama ya elimu. Amesema wanafunzi wengi barani Afrika hupoteza fursa ya kusoma elimu ya juu kutokana na kukosa uwezo wa kulipa ada. Hivyo basi katika karne hii ambapo bara la Afrika linahitaji sana wataalamu mbalimbali, gharama za elimu hazipaswi kuwa kizuizi cha mtu kusoma.!
 
Wee jamaa chagua nchi za maana kujenga hoja achana na hizo useless countries like liberia
 
Nenda kwenye vyanzo uone - Mwaka 2017 Tanzania ina idadi ya watu takriban 54M wakati Liberia ina watu 4.6M - kwa ufupi ni kuwa nchi ya Liberia ina idadi ya watu sawa na mkoa wa Mwanza.

Lakini pia rais wa Liberia ameondoa ada vyuo vikuu lkn ada ktk shule za awali, msingi na sekondari ziko palepale tofauti na nchi ya Tanzania

Sisi tunawaacha mbali Liberia kwa ubora wa huduma za umma
Acha uzAlendo uliopitiliza

Mkuu .54 million people ni jambo zuri sana sababu we got enough man power pia walipa kodi ni wengi

So sisi ndio tungefaa tuwe na free universty.
Hao 4million people mapato nchi inayopata ni madogo
 
Hongera zake kwa kuwa na dhamira ya kuwasaidia watu wake. Lakini siamini kama kuna kitu kinaitwa free education. Awaambie vizuri ni wapi atatoa pesa za kugharimia elimu.
 
Hata huku kwetu elimu ya msingi ni bure na tumefanikiwa kupata mwanafunzi bora std7 toka chato ambae alikua amesimamishwa miezi 3 kwa kukosa ada,maajabu tutaona mengi kutoka chato
 
Back
Top Bottom