Liars!

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,005
We need the breakdown of those numbers and in which industries those 437, 205 'new jobs' we created from January 2005 to June 2008

Opposition: Govt figures on job creation wrong

By Samuel Kamndaya, Dodoma
THE CITIZEN

A cabinet minister and the opposition bench in Parliament engaged in a heated argument yesterday over claims that the fourth phase Government has created over 400,000 jobs since it came to power.

Labour, Employment and Youth Development minister Juma Kapuya said 437,205 jobs had been created, but the opposition spokesman for the ministry, Mr Salim Khalfani, said the figures were wrong.

The opposition wants the minister to tell the National Assembly where these 400,000 jobs are, said Mr Khalfani, the Civic United Front MP for Tumbe. President Jakaya Kikwete pledged to create one million jobs in the first five years of his administration and Prof Kapuya yesterday told Parliament the Government was on course to honour the promise.

Records indicate that until June 2008, 437,205 jobs had been created. This is equivalent to 43.7 per cent of the goal of creating one million jobs by 2010, said the minister while presenting budget estimates for his ministry for the financial year 2008/09.

The opposition said some 1,700 jobs might have been created contrary to what the Government was saying. Mr Khalfani said he based his assessment on a publication on the state of the national economy for 2007 which showed that employment in the industrial sector rose from 89,316 jobs in 2005 to 91,112 in 2007.

But Prof Kapuya said the informal sector created 195,017 jobs during the last two years while the private sector created 183,789 jobs. The public sector created 58,399 jobs.Mr Khalfani asked the Government to carry out a comprehensive study over employment in the country. He claimed that there were reports that telecommunication companies had employed foreigners illegally.

Meanwhile, the Government has said it plans to complete a study to establish effects of the new minimum wage on the growth of the private sector.Labour, Employment and Youth Development minister Juma Kapuya told the House yesterday that the study to establish the impact of the Sh80,000 minimum wage on the private sector would be conducted in the current financial year.

The Government established the private sector wage board that proposed new minimum wage for the private sector from Sh40,000 to Sh80,000 a month. The rate sparked a war of words between the private and the public sectors. There had been reports of massive retrenchments and closures of some companies due to the inability to pay the wages.

We will establish the effects in a study and propose new measures to be taken in accordance with what the report will tell us, Prof Kapuya said. But the chairman of the Parliamentary Committee on Community Development, Mrs Jenista Mhagama (CCM - Peramiho), said it was high time another comprehensive study on the wages was carried out to enable it to arrive at a rate agreed by all parties.
 
More breakdown is needed e.g. for those 58,399 jobs that were created by public sector:
10 jobs were created by Home affairs
20 by Foreign Ministry rather than a blanket figure of 58,399
 
Ukiona mtu anaanza kukuwekea figures za informal sector ujue hapo kuna uongo unatengenezwa. Ukimuuliza Kapuya swali kwamba Tanzania ina wamachinga wangapi? Mama/Baba Lishe wangapi? Hawezi kukupatia jibu la swali hilo kwa kuwa hawana takwimu sahihi za informal sector. Hata ukienda National Bureau of Statistics nao hawawezi kukupatia jibu lenye uhakika. Swali langu kwa Kapuya ni kwamba je hizo takwimu kwamba kuna new jobs ambazo zimekuwa created kwenye informal sector amezipata wapi?

Kama atasema ni mabilioni JK basi huo utakuwa ni uongo kwa kuwa mojawapo ya conditions ya kukopeshwa ni kwamba mtu awe alikuwa na ka-biashara fulani kanakoeleweka na pia awe na eneo specific anapofanyia biashara ili benki zinazokopesha ziweze kujua huyo mtu anapatikana wapi. Kwa hiyo akipewa mkopo lengo ni kwenda kupanua bishara yake na siyo kwenda kuanzisha biashara.

Hapa ndipo ambapo unaona wazi kwamba kuna failure kubwa katika upande wa uongozi. Pamoja na kuanzisha wizara hiyo na makeke ya kuweka manaibu waziri 2 (mmoja ashughulikie ajira pekee, bado alishindwa mpaka hiyo nafasi ilipofutwa). Huwezi ukasema unakopesha wamachinga wakati maeneo ya kufanyia hizo biashara zao hayapo ama kazi za umachinga zinapingana na sheria za halmashauri za majiji/manispaa na miji. Hakuna hata Halmashauri moja ambayo inakubaliana na umachinga za kuweka kijiwe mahali popote ili ufanye biashara. Wizara ya Kazi ilitakiwa kukaa na wizara ya tawala za mikoa pamoja na viongozi wa majiji/manispaa/miji ili waangalie namna ya kuweka mazingira mazuri ya kuwasaidia wamachinga. Wamachinga wakiwekwa pamoja ni rahisi sana hata kuwalipisha kodi badala ya jinsi wanavyohanja kama kuku wa kienyeji wakijaribu kutafuta chakula.

Swali la nyongeza kwa Prof. Kapuya ni kwamba je ajira alizoahidi JK ni pamoja na hizi za wamachinga ambao wanakimbizana na mgambo wa jiji kila kukicha?

Nitakubaliana na takwimu za ajira kwenye sekta binafsi na ajira za serikalini, lakini hizo za sekta isiyo rasmi hapo ni uongo mkubwa na ni dalili za kuanza kuvuta kasi kuelekea 2010 maana JK anajua tutamuuliza zile ajira ni aje?
 
More breakdown is needed e.g. for those 58,399 jobs that were created by public sector:
10 jobs were created by Home affairs
20 by Foreign Ministry rather than a blanket figure of 58,399

Bubu,

Hizo ajira inawezekana ikawa kweli maana zile shule za Lowassa (sekondari za kata) zimejitahidi sana kuajiri Yebo yebo a.k.a Voda Fasta. Labda kwenye sekta binafsi ndiyo unaweza kutia mashaka.
 
Ukiona mtu anaanza kukuwekea figures za informal sector ujue hapo kuna uongo unatengenezwa. Ukimuuliza Kapuya swali kwamba Tanzania ina wamachinga wangapi? Mama/Baba Lishe wangapi? Hawezi kukupatia jibu la swali hilo kwa kuwa hawana takwimu sahihi za informal sector.Hata ukienda National Bureau of Statistics nao hawawezi kukupatia jibu lenye uhakika. Swali langu kwa Kapuya ni kwamba je hizo takwimu kwamba kuna new jobs ambazo zimekuwa created kwenye informal sector amezipata wapi?

Kama atasema ni mabilioni JK basi huo utakuwa ni uongo kwa kuwa mojawapo ya conditions ya kukopeshwa ni kwamba mtu awe alikuwa na ka-biashara fulani kanakoeleweka na pia awe na eneo specific anapofanyia biashara ili benki zinazokopesha ziweze kujua huyo mtu anapatikana wapi. Kwa hiyo akipewa mkopo lengo ni kwenda kupanua bishara yake na siyo kwenda kuanzisha biashara.

Hapa ndipo ambapo unaona wazi kwamba kuna failure kubwa katika upande wa uongozi. Pamoja na kuanzisha wizara hiyo na makeke ya kuweka manaibu waziri 2 (mmoja ashughulikie ajira pekee, bado alishindwa mpaka hiyo nafasi ilipofutwa). Huwezi ukasema unakopesha wamachinga wakati maeneo ya kufanyia hizo biashara zao hayapo ama kazi za umachinga zinapingana na sheria za halmashauri za majiji/manispaa na miji. Hakuna hata Halmashauri moja ambayo inakubaliana na umachinga za kuweka kijiwe mahali popote ili ufanye biashara. Wizara ya Kazi ilitakiwa kukaa na wizara ya tawala za mikoa pamoja na viongozi wa majiji/manispaa/miji ili waangalie namna ya kuweka mazingira mazuri ya kuwasaidia wamachinga. Wamachinga wakiwekwa pamoja ni rahisi sana hata kuwalipisha kodi badala ya jinsi wanavyohanja kama kuku wa kienyeji wakijaribu kutafuta chakula.

Swali la nyongeza kwa Prof. Kapuya ni kwamba je ajira alizoahidi JK ni pamoja na hizi za wamachinga ambao wanakimbizana na mgambo wa jiji kila kukicha?

Nitakubaliana na takwimu za ajira kwenye sekta binafsi na ajira za serikalini, lakini hizo za sekta isiyo rasmi hapo ni uongo mkubwa na ni dalili za kuanza kuvuta kasi kuelekea 2010 maana JK anajua tutamuuliza zile ajira ni aje?

Perspicacious...!
 
..JK aliahidi ajira milioni 1 kila mwaka.

..sasa naona wamekuja na marekebisho kwamba in the 1st 5 yrs.

..Waongo wakubwa hao.
 
Bubu,

Hizo ajira inawezekana ikawa kweli maana zile shule za Lowassa (sekondari za kata) zimejitahidi sana kuajiri Yebo yebo a.k.a Voda Fasta. Labda kwenye sekta binafsi ndiyo unaweza kutia mashaka.

Ndugu yangu Keil, hii siri kali mimi siiamini hata kidogo katika kutengeneza fictitious numbers ili waonekane ni watendaji kazi wazuri machoni mwa Watanzania. Si unakumbuka sakata la Meremeta na Tangold kama siyo kuwabana basi tungeamini uwongo wao kuhusiana na waliyoyasema, lakini hadi hii leo kwenye sirikali hakuna anayeweza kuthibitisha kwamba makampuni hayo yalikuwa owned na sirikali.

Pia kama utakumbuka juzi juzi Mkulo alitaka kutuzuga Watanzania kwamba pesa za EPA zilizoibwa shilingi bilioni 155 si za siri kali ya Tanzania bali ni za 'wafanya biashara binafsi' wengine wameshakufa na wengine wanaishi nchi za nje. Pamoja na kuwa katibu wa Rais, Luhanjo alishatoa kauli hadharani kwamba zile pesa ni za siri kali. Baada ya kubanwa sana Mkulo ili atuthibitishie kauli yake akaingia mitini na kuwa bubu kuhusu swala la peza za EPA.

Wakatwambia wamekusanya bilioni 60 toka kwa mafisadi waliokupua BoT, tulipowaomba majina ya mafisadi hao na kiasi kilichokusanywa na pia zimewekwa katika benki ipi ili tupate uthibitisho toka benki hiyo kweli kuna account kama hiyo wakawa na kigugumizi na hatimaye kuwa mabubu.

Kwa mantiki hiyo basi tukimbana huyu Kapuya ili azinyambue hizo figure further basi utaona ataanza kuwa na kigugumizi halafu kuwa bubu. Siamini kabisa katika kipindi cha hicho kinachosemwa Tanzania 'imecreate' kazi nyingi kiasi hicho. Sijui ni ngapi tulizopoteza katika sekta mbali mbali. Maana inatakiwa uchukue jumla ya kazi zilizokuwa created katika kipindi hicho halafu utoe kazi ambazi zimepotea katika kipindi hicho ili upate number ambayo inaweza ikawa negative au positive, sidhani kama hili lilifanywa.
 
Watuambie mafisadi wetu wamefika nao wapi hizi longolongo mara hili mara lile wanatuchelewesha kupandisha gurudumu la maendeleo mlimani,Wanachotaka WaTanzania kwa muda huu wa miaka miwili ni hili kundi la mafisadi limewekwa kwenye kiwango gani lipo wapi na linafanya nini au linafanyiwa kazi gani ni lini Watanzania wataridhika na hatua zitakazochukuliwa tunahitaji time frame hapa mambo ya kaimati hayamjengei Muungwana bali yanam'bomolea ,mafisadi anaocheza nao watakuja kumpiga dafrau aipate wa kumuinua ,shauli lake,yeye Muungwana naona amewatuliza WaTanzania lakini mafisadi wanajikusanya kama roboti la sinema ni mfano tu lakini ndivyo inavyoonekana wanajaribu kugonga kila ukuta waone kama kuna sauti ya kubomoka.
 
Bubu,

Hizo ajira inawezekana ikawa kweli maana zile shule za Lowassa (sekondari za kata) zimejitahidi sana kuajiri Yebo yebo a.k.a Voda Fasta. Labda kwenye sekta binafsi ndiyo unaweza kutia mashaka.

Hao voda fasta nadhani idadi yake inajulikana..Waziri Mage aliwahi kutoa idadi yao wanaohitajika; nadhani ilikuwa around 6,000 kwa mpango mzima kama sijakosea.
 
..JK aliahidi ajira milioni 1 kila mwaka.

..sasa naona wamekuja na marekebisho kwamba in the 1st 5 yrs.

..Waongo wakubwa hao.

Yaani tatizo hatujapata transcript ya Msanii mkuu aka Vasco daGama aliyotoa bungeni alipoingia madarakani na kutoa ahadi 100, maana kulikuwa na ahadi hiyo ya ajira milioni 1 kila mwaka, lakini within 1 week walirekebisha wakasema eti milioni 1 katika miaka 5. Whichever way ni uzushi tu na usanii. Wabunge wa upinzani wameshaaibisha sirikali, sasa tuendelee na mada ya maana ya ufisadi! Hivi unategemea msanii Kapuya aende kufafanua takwimu, anaelewa nini?
Hii ajira ni ile ya kuwatimuatimua vijana wetu mitaani wamachinga na kuwaweka katika masoko na kuwalazimisha wasajiliwe katika masoko sasa zile 'takwimu' wanatuambia ni ajira mpya, do you get it? Yaani ni usanii kwelikweli.
 
Mkuu Susuviri,
kwani unadhani ile transcript ya vasco da Gama hatuna?kama unabisha haya mi nakupigia attachment hapa chini na kwa faida ya mijadala ya humu jf inayomhusu vasco da Gama itatusaidia sana kumpima kwa haki to what extent amefanikiwa au kufeli katika agenda zake.

Naomba Kuwasilisha
 
Attachments

  • HOTUBA YA RAIS KIKWETE BUNGENI[1].doc
    102 KB · Views: 105
Yaani tatizo hatujapata transcript ya Msanii mkuu aka Vasco daGama aliyotoa bungeni alipoingia madarakani na kutoa ahadi 100, maana kulikuwa na ahadi hiyo ya ajira milioni 1 kila mwaka, lakini within 1 week walirekebisha wakasema eti milioni 1 katika miaka 5. Whichever way ni uzushi tu na usanii. Wabunge wa upinzani wameshaaibisha sirikali, sasa tuendelee na mada ya maana ya ufisadi! Hivi unategemea msanii Kapuya aende kufafanua takwimu, anaelewa nini?
Hii ajira ni ile ya kuwatimuatimua vijana wetu mitaani wamachinga na kuwaweka katika masoko na kuwalazimisha wasajiliwe katika masoko sasa zile 'takwimu' wanatuambia ni ajira mpya, do you get it? Yaani ni usanii kwelikweli.

That appears to be the case.

Asante Augustoons kwa hii transcript ya hotuba.

.
 
Walioondoka kwenye AJIRA kule TRC, DAWASCO,... ameitaja idadi yao? Kitengo cha TAKWIMU tumekizembea muda mrefu tu badala yake tuka-opt kutoa RUZUKU kwa Vyama vya SIASA!
 
Watanzania, tunakubali kudanganyika kirahisi hivi? Hizo ajira wanazodai hawa watu mbona hatuzioni? Je ni ajira walizotoa kwa wasomi katika levels mbalimbali? wametumia vigezo gani katika hili?
Nimejaribu kutafuta data za waliomaliza vyuo vya juu vya elimu mbalimbali kuanzia huo mwaka waliotaja nimekosa bahati mbaya ila nimepata kuanzia mwaka 2000/2001-2004/2005. Ila zinaweza kutoa projections za aina fulani.
Katika miaka hiyo nitawapa total sum ya wanafunzi walio enroll
UDSM - 39,496
MUCHS - 6,356
UCLAS - 4185
SUA - 10,667
OUT - 37,762*- wengi ni waajiriwa tayari
Mzumbe - 7,686
SUZ - 446
MUCCoBS- 2029

Jumla ni 108,627 expected graduates in consecutive years 2004/2005-2007/2008.

Sasa hypothetically tuseme hakuna aliyefariki, hakuna aliyefeli, hakuna aliyeahirisha masomo na hakuna aliyekosa ajira wala kurudia mwaka wa masomo. Hao waajiriwa wapya 328,578 wametokea wapi? Form 4? Form 6? Professional colleges? Vocational colleges? TTCs? Continuing education? Wanahesabu na machinga pia kama ajira? Kama wanafanya hivyo basi then its a realistic figure to a certain extent.

We certainly need a breakdown waheshimiwa. Nitajaribu kutafuta figures za vyuo vidogo mbalimbali na nijumlishe hapo tuone kama idadi inakuja au haiji.Nitatafuta pia idadi ya waliomaliza sekondari tuone kuna lipi linaloendelea hapa.
 
Back
Top Bottom