LHRC yatoa ufafanuzi wa kisheria juu ya sakata la mwenyekiti wa mtandao wa wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo

Bibi Kijo Bisimba ana uhusiano gani na Nondo? LHRC ina uhusiono gani na TGNP ya Nondo? Wakili wa Nondo anatokea wapi ? Huyu mama ni wa kumuweka karibu, anatumika.
Samahani kukuuliza hili swali..

Una elimu gani mkuu??
 
Kwenye hii issue ya Abdul Nondo, I can smell something fishy!.
Hili za mtuhumiwa kuwa mikononi na polisi bila kuruhusiwa kuonekana, kutembelewa na kupata uwakilishi, linanitatiza, maana hawa wenzetu hawachelewi kutuletea taarifa kama hizi...
IGP Kamanda Sirro, Usiruhusu Vifo Vya Uzembe Kama Huu Kuchafua Jeshi Letu Safi la Polisi!.
Vifo vya Mahabusu Mwanza, IGP Mangu, Usikubali Kudanganywa!, Polisi Wako Ni Wauaji!. P'se Stop This
Tumuombee Abdul Nondo salama, na kweli afikishwe mbele ya vyombo vya sharia.

Paskali
Police Brutality in Tanzania: The World has a Right to know!
Mhe.Kaimu Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma, Naomba Usiruhusu Udhalilishaji Huu Ndani ya Mahakama Zetu!.

Pascal,
Kwa hali hii tunavoenda huko mbeleni itakuwa ni majanga wallah....!!
Abdul, Nondo ni kijana mwanafunzi mwaka 3 UDSM lakini kwa Serikali imeamua kumshiikilia kana kwamba ni Jambazi. Mhaini au Kibaka fulani pasi na sababu za msingi....!!Huu ni ujinga na pumbafu wa Jeshi la Polisi na hawa Viongozi wa CCM...!!
Nimemskia Mwigulu Nchemba akiongea na Wanachuo wa Vyuo Vikuu akimnanga kijana Abdul Nondo...!!Ati kwamba Nondo aliposema Waziri wa Mambo ya Ndani yeye Nchemba alifikiri ati alimmanisha Waziri wa Serikali ya Wanafunzi....Nonsense...!!
Huyu jamaa kwa sasa anajiita ati Dokta lakini ukweli ni kuwa kichwani kwake kumejaa kamasi na siyo ubongo.....!!
Yaani Waziri mzima unaongea pumba mbele ya Wasomi ukimshambulia tena Mwanachuo mwenzao kuwa ATI KUKOSOA SERIKALI YA MAGUFULI NI USALITI...Kweii???? Huyu Nyaturu man hajielewi perce.
 
Mungu apishie mbali maana sijuhi watakuja na utetezi gani this time kama yakitokea hayo, na kibaya zaidi ni Mjuavyo Nondo akitoka hata acha kusema labda wamakate ulimi(najua ataandika)
 
Pascal,
Kwa hali hii tunavoenda huko mbeleni itakuwa ni majanga wallah....!!
Abdul, Nondo ni kijana mwanafunzi mwaka 3 UDSM lakini kwa Serikali imeamua kumshiikilia kana kwamba ni Jambazi. Mhaini au Kibaka fulani pasi na sababu za msingi....!!Huu ni ujinga na pumbafu wa Jeshi la Polisi na hawa Viongozi wa CCM...!!
Nimemskia Mwigulu Nchemba akiongea na Wanachuo wa Vyuo Vikuu akimnanga kijana Abdul Nondo...!!Ati kwamba Nondo aliposema Waziri wa Mambo ya Ndani yeye Nchemba alifikiri ati alimmanisha Waziri wa Serikali ya Wanafunzi....Nonsense...!!
Huyu jamaa kwa sasa anajiita ati Dokta lakini ukweli ni kuwa kichwani kwake kumejaa kamasi na siyo ubongo.....!!
Yaani Waziri mzima unaongea pumba mbele ya Wasomi ukimshambulia tena Mwanachuo mwenzao kuwa ATI KUKOSOA SERIKALI YA MAGUFULI NI USALITI...Kweii???? Huyu Nyaturu man hajielewi perce.

CC: Mwigulu Nchemba
Ina kuhusu!
 
LHRC Yatoa Ufafanuzi wa Kisheria juu ya Sakata la Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP) Abdul Nondo

Katika kudumisha haki za binadamu na utawala wa sheria nchini Tanzania, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kimeendelea kufanya uangalizi wa utendaji kazi wa serikali ili kuhakikisha inatekeleza majukumu yake bila kukiuka misingi ya haki za binadamu na utawala wa sheria.

Mnamo Machi 7, 2018 Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kilipata taarifa za kushtusha za kutokuonekana kwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP) Ndugu Abdul Nondo na kufarijika baada ya kupata taarifa za kupatikana kwake mapema.

Hata hivyo taarifa za shutuma zilizoelekezwa kwa Abdul Nondo kutoka kwa jeshi la Polisi, Waziri wa Mambo ya Ndani pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam baada ya kujisalimisha kwa Jeshi la Polisi huko Iringa zimekishitua Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu na kuona ni vyema kufanya kumbushi ya kisheria kwa jeshi la polisi na viongozi hao kwa kukiuka sheria kama inavyofafanuliwa;
Dhana ya Kutokuwa na Hatia (Presumption of Innocence)
Kwa mujibu wa Ibara ya 13 (6) (b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Sura No.2 kama ilivofanyiwa marejeo mwaka 2002:-
“Ni marufuku kwa mtu yeyote aliyeshtakiwa kwa kosa la jinai kutendewa kama mtu mwenye kosa hilo mpaka itakapothibitika kuwa anayo hatia ya kutenda kosa hilo.”

Ni kosa kumhukumu mtu yeyote bila ya chombo chenye mamlaka hayo kuthibitisha kuwa mtu huyo amefanya kosa hilo. Viongozi wa kisiasa na serikali kuzungumza baadhi ya masuala kama maamuzi ya mwisho na kuingilia muhimili wa mahakama na kuwaita watu wahalifu na kusahau dhana pana ya kutokuwa na hatia hadi imethibitishwa ni ukiukwaji wa Katiba.

Kuingiliwa kwa muhimili wa Mahakama
Mahakama ndio chombo chenye mamlaka ya juu zaidi katika utoaji haki kama ilivyofafanuliwa katika Ibara ya 107A (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977:-
“Mamalaka yenye kauli ya mwisho ya utoaji haki katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Mahakama.”

Viongozi wa serikali na jeshi la polisi watafanya kosa kumshutumu mtu yeyote yule na kuingilia uhuru na kazi ya mhimili wa Mahakama kinyume cha Katiba walioapa kuilinda.

Ukiukwaji wa Haki ya Kupata Dhamana
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzanaia imetoa haki ya mtu kupata dhamana pale ambapo suala lake lipo katika vyombo vya utaoji wa haki. Ibara ya 13 (6) (a) inaeleza:-
“Wakati haki na wajibu wa mtu yeyote inapohitajika kufanyiwa maamuzi na mahakama au chombo kingine chochote kinachohusika, basi mtu huyo atakuwa na haki ya kupewa fursa ya kusikilizwa kiukamilifu, na pia haki ya kukata rufani au kupata nafuu nyingine.”

Wakati Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi lilipaswa kutoa dhamana kwa Abdul Nondo. Mahakama imeweza kutangaza vipengele vya sheria vinanvyokinzana na Katiba katika kumnyima mtuhumiwa kupata dhamana pale ambapo shauri lake linapokuwa linasikilizwa au anapokuwa chini ya upelelezi wa Jeshi la Polisi.

Tumeshuhudia hivi karibuni Mahakama ya Rufani ya Tanzania katika kesi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Mtobesya, ambapo Mahakama imetangaza kifungu namba 148 (4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai Sura No. 20 kuwa batili kwani kinampa mamalaka Mkurugenzi wa Mashtaka mtuhumiwa haki ya kupata dhamana. Si sahihi kumuweka mtu kizuizini bila dhamana au kufikishwa mahakamani kwa zaidi ya siku saba wakati sheria imeweka masaa 24 .

Haki ya kupata Uwakilishi
Mtu anapokuwa ameshikiliwa na Jeshi la Polisi kama mtuhumiwa anayo haki ya kupata mwanasheria ili aweze kumwakilisha mahakamani wakati wa kusikiliza kesi. Ibara ya 13 (6) (b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, imeeleza kwamba wakati haki na wajibu wa mtu yeyote inapohitajika kufanyiwa maamuzi na mahakama au chombo kingine chochote basi mtu huyo atakuwa na haki ya kupewa fursa ya kusikilizwa kiukamilifu na kuweza kupata nafuu au nafuu nyingine ya kisheria.

Mahakama zimetoa tafsiri juu ya Haki ya Uwakilishi kwa mtuhumiwa yeyote. Mtuhumiwa anapaswa kuelekezwa kuwa ana haki ya kupata haki ya uwakilishi toka kwa Wakili haya yalisemwa katika kesi ya Thomasi Mjengi & Wenzake dhidi ya Jamhuri 1992 TLR 157, ambapo Jaji Mwalusanya enzi za uhai wake alisema:-
“Haki ya uwakilishi inahusisha pia haki ya mtuhumiwa kuambiwa kuwa ana haki ya kupata uwakilishi na hayo yasipofuatwa basi maamuzi ya awali yaliyotolewa huwa batili.”

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu hakiafiki kitendo cha Polisi chini ya kitengo cha Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai (DCI), kuwakatalia Mawakili kuweza kumwona mtuhumiwa Abdul Nondo na kuweza kupata haki ya uwakilishi mbele ya vyombo vya utoaji haki.

Msimamo wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu
Ili kudumisha utawala wa sheria na haki za binadamu nchini, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinawataka viongozi wa serikali na vyombo vya dola kufuata sheria na kuheshimu haki za binadamu katika utekelezaji wa majukumu yake.

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinaitaka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHRAGG) kutumia mamlaka iliyopewa kwa mujibu wa sheria kuwachukulia hatua viongozi wanaokiuka misingi ya haki za binadamu na utawala bora.

Imetolewa Machi 15, 2018 na,
Dkt. Helen Kijo-Bisimba
Mkurugenzi Mtendaji
Hizi ni moja kati ya idara ambazo zimetendewa haki kwa watu walioko hapo. Yaani inaonyesha ni jinsi gani walivyo na weledi na kazi yao
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom