LHRC yalaani polisi kumdhalilisha mwanamke Igunga

Ng'wanza Madaso

JF-Expert Member
Oct 21, 2008
2,268
333
KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimelaani kitendo kilichofanywa na Jeshi la Polisi nchini cha kumdhalilisha mwanamke mmoja ambaye alikuwa akifanya maandamano ya kushinikiza kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi mdogo wa jimbo la Igunga, mkoani Tabora.

Akizungumza na Tanzania Daima Jumatano, Ofisa Ueleweshaji Umma, Jinsia na Watoto wa LHRC, Edna Lushaka, alisema kitendo kilichofanywa na polisi wanaume ni cha udhalilishaji, kinyama na kinyume na kanuni za adhabu.

Alisema kisheria polisi wana uwezo wa kuwakamata wananchi, lakini sio kwa kutumia nguvu ya ziada na kwamba sheria inaruhusu polisi wa jinsia inayofanana na mtuhumiwa kumpekua endapo anatuhumiwa.


"Kitendo cha polisi wa kiume kumbeba juujuu na kumweka kwenye gari mwanamke yule, ni udhalilishaji wa haki za binadamu na si sahihi," alisema.

Naye Mkuu wa Huduma za Polisi Jamii, Isaya Mngulu, alikiri kuwa si sahihi kwa polisi wa kiume kumnyanyua mtuhumiwa mwanamke na kwamba kitendo hicho kilifanywa baada ya kutokuwepo polisi wanawake katika eneo hilo la tukio.


Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbrod Slaa, alishangazwa na kitendo cha Baraza Kuu la Kiislamu nchini (BAKWATA), kukaa kimya bila kuzungumzia tukio hilo wakati katika tukio la kudhalilishwa kwa Mkuu wa Wilaya, Fatma Kimario, walitoa tamko.


"Nilitegemea BAKWATA leo watatoa tamko kwa kuwa mwanamke amedhalilishwa. Hapo ndipo tutajua BAKWATA wanatetea haki za watu au walikuwa na ajenda yao nyingine. Huwezi kulinganisha kitendo cha jana na kile cha hijabu," alisema Dk. Slaa.



Chanzo: HAPA
 
Watoe tamko kwani kuna manufaa kwao au kwa Magamba?

Hawa si matarumbeta ya magamba haya na hakuna tarumbeta la kupiga kelele kinyume na anaelimiliki.........ni ndoto
 
Igungadem.jpg
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom