LHRC yaitisha Maandamano nchi nzima kupinga malipo ya DOWANS

luckman

JF-Expert Member
Oct 11, 2010
1,211
371
Kituo cha haki za binadamu kimeitisha maandamo nchi nzima kuitaka serikali isilipe tuzo ya tzs 111bil kwa dowans, wanaharakati hao wamesema maandamo yatkwenda siku kumi mfululizo iwapo serikali itashindwa kutoa tamko juu ya malipo hayo!

Wamewaomba wananchi kuvaa nguo nyeusi na kujifunga bendera ya nchi kichwani kuashiria maombolezo juu ya yale yanayofanyika nchini!

Mama Ananilea Nkya amesema nchi yetu haina deni, na hizi pesa ni zawadi au charges kwa kuvunja mkataba ambao haukuwa na nguvu kisheria!

WARATIBU WA HAYO MAANDAMO NADHANI WATATUELEZA WAPI TUNAANZIA NA KUISHIA!

NAOMBA TUENDELEE KUPASHANA HABARI NA TUTOKE MAJUMBANI KWETU NA KUTETEA HAKI YETU NA KUPINGA MAMBO YOTE YA HOVYOHOVYO! HATIMA YA NCHI IKO MIKONONI MWETU KWANI VIONGOZI TULIOWAAMNI WAMESHINDWA KUTUFANYIA TULIYOWATUMA!

NAWASILISHA!
 
Kituo cha haki za binadamu kimeitisha maandamo nchi nzima kuitaka serikali isilipe tuzo ya tzs 111bil kwa dowans, wanaharakati hao wamesema maandamo yatkwenda siku kumi mfululizo iwapo serikali itashindwa kutoa tamko juu ya malipo hayo!wamewaomba wananchi kuvaa nguo nyeusi na kujifunga bendera ya nchi kichwani kuashiria maombolezo juu ya yale yanayofanyika nchini! mama Ananilea Nkya amesema nchi yetu haina deni, na hizi pesa ni zawadi au charges kwa kuvunja mkataba ambao haukuwa na nguvu kisheria! WARATIBU WA HAYO MAANDAMO NADHANI WATATUELEZA WAPI TUNAANZIA NA KUISHIA!NAOMBA TUENDELEE KUPASHANA HABARI NA TUTOKE MAJUMBANI KWETU NA KUTETEA HAKI YETU NA KUPINGA MAMBO YOTE YA HOVYOHOVYO! HATIMA YA NCHI IKO MIKONONI MWETU KWANI VIONGOZI TULIOWAAMNI WAMESHINDWA KUTUFANYIA TULIYOWATUMA!NAWASILISHA
 
Safi sana. Tena nina hamu sana na maandamano maana toka nimeondoka Mlimani mwaka 2007 sijawai kuandamana. Jamani kwa wale ambao ni wageni wa maandamano tunawakumbusha kubeba chupa zenye maji kukabiliana na polisi kama wakifyatua yale mabomu yao ya machozi.
 
naomba mtuachie tarehe 14 yetu tuna matembezi ya hisani ya kuchangisha ujenzi wa ward ya watoto wenye cancer na pia tunataka kuomboleza msiba wa Baba wa Taifa kwa amani.
 
Safi sana. Tena nina hamu sana na maandamano maana toka nimeondoka Mlimani mwaka 2007 sijawai kuandamana. Jamani kwa wale ambao ni wageni wa maandamano tunawakumbusha kubeba chupa zenye maji kukabiliana na polisi kama wakifyatua yale mabomu yao ya machozi.

Serikal ya CCM,hakuna kipindi ambacho wanapaswa kutumia busara katika maamuzi kama kipindi hiki cha sasa.Kitendo cha kuibuka kuyazuia maandamano haya Kiharakati ni kujichimbia kaburi la msiba kabla ya msiba.Manake wasivyoaminika kwa maamuzi yanayoleta dukuduku la utata dakika za mwisho mwisho usishangae polisi wanaibuka dakika za lala salama masaa machache kabla ya wanaharakati hao kuwepo barabara na kusema YATA HATARISHA AMANI ya raia wengine.
 
Safi sana. Tena nina hamu sana na maandamano maana toka nimeondoka Mlimani mwaka 2007 sijawai kuandamana. Jamani kwa wale ambao ni wageni wa maandamano tunawakumbusha kubeba chupa zenye maji kukabiliana na polisi kama wakifyatua yale mabomu yao ya machozi.

Mlima gani kuna milima mingi Kitonga, Sekenke, Nyashana, fafanua baada ya kutoka Mlimani wapi?
 
Natoa Tamko: kabla ya maandamano unaaga kabisa nyumbani maana haifahamiki nani atarudi salama au vipi..
 
Usingekuwa wizi wa gege lenu la majambazi hiyo ward ingejengwa na pesa zetu 152mil per day+111bil tunazolazimishwa kulipa!mawazo yako mazuri ila lazima uangalie katika wigo mpana!
 
Me nasema wawalipe kwa 7bu hayo ndo Matokeo ya kuwa na Serikali Mbovu, Wala hakuna haja ya Mwananchi kuandamana, Mangapi tulipinga lkn serikali yetu ikayafanya kwa nguvu? Cha msingi tukubaliane na kila hali, NGUVU kubwa tuilekeze kwe Uchaguzi wa 2015, tuwafyatue hawa Magamba. "NCHI IMECHAKAA INAHITAJI UKARABATI WA HALI YA JUU IRUDISHE HESHIMA YAKE"
 
Mie mwenyewe tokea nilipotoka pale kwa Udsm 2009 kitu ambacho nilisikitika ntakimis ni maandamano a.k.a kunji,sasa ni mda muafaka wa kurudi barabarani
 
Kusema kweli inauma sana kuona serikali inawaunga mkono WEZI HAWA 'DOWANS'. Kama DOWANS wametokana na RICHMOND (kampuni hewa), iweje wawe ENTITY ya kufungua kesi na kudai FIDIA? Fidia kwa nani? Huu wizi BASI.
 
Ndugu zangu kwa wale wenye mali, tujaribu kuacha kabisa barua za urithi kwenye familia zetu.

Uwezi kujua kama tutarudi salama baada ya maandamo kama mnavyojua askari wetu na FFU.

Tujitokezeni kwa wingi vifo vya wengi ni harusi
 
Waunganishe na ya CDM, na madai yaongezeke! Wekeni na la umeme, mikopo ya wanafunzi, Nyumba za polisi na mishahara yao, madai ya waalimu pamoja na mikataba mibovu kama ya UDA, Kiwira na zile 3T za mnajimu.
 
inawezekana kutumia maandamano hayo kumuondoa yule dhalimu pale magogoni....siku kumi mfululizo ni nyingi sana...tutumie mda huu
 
15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom