Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 2,488
- 6,861
Akizungumza wakati wa kuwasilisha matokeo ya utafiti huo, Afisa Utafiti wa Legal and Human Rights Centre (LHRC), Fundikira Wazambi, amesema wanaume wameongoza kwa kuathirika na ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Tanzania mwaka 2025, kutokana na matukio ya machafuko ya Oktoba, ukiwemo ukiukwaji wa haki za kiraia pamoja na kukamatwa na kuwekwa kizuizini kinyume na sheria
“Kwa mwaka 2025, waathirika wakuu wa ukiukwaji wa haki za binadamu walikuwa watoto na wanaume. Wanaume waliathiriwa zaidi na machafuko ya Oktoba, ukiukwaji wa haki za kiraia, pamoja na ukamataji na uwekaji kizuizini kinyume na sheria na kanuni za nchi,” alisema Wazambi.
Aidha, ripoti hiyo ilibainisha kuwa kwa upande wa watoto, changamoto kubwa ilikuwa ni ukatili, hususan ukatili wa kingono na kimwili.
Haki Tano Zinazovunjwa Zaidi
Katika kuweka sawa takwimu hizo, Wazambi aliorodhesha haki tano kuu ambazo zimekuwa zikivunjwa mara kwa mara katika kipindi cha mwaka 2025:

- Haki ya kuishi
- Haki ya kuwa huru na salama
- Haki ya usawa mbele ya sheria
- Uhuru dhidi ya ukatili
- Uhuru wa kuabudu