LHRC wapo kisiasa na hawana msaada kwa wananchi wa kawaida

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,708
5,711
Hichi kituo cha kutetea haki za binadamu hakina msaada wowote kwa raia wa kawaida na inaonekana wao wapo kisiasa tu na kujaza matumbo yao kwa misaada ya pesa wanayopata toka huko nje.

Wapo tayari kupiga kelele na kulaani pale wanasiasa wa upinzani wanapokamatwa au alipokamatwa mfanyakazi wao Tito Magoti wameenda mbali mpaka kufungua kesi Mahakama Kuu. Lakini raia wa kawaida na wanyonge hawasaidiwi kabisa na hawa jamaa.

Mfano, kuna mama kule Mwanza mume wake aliteswa na migambo na wanajeshi mpaka kufa. Alivyowafuata hakuna msaada waliompa. Mwakilishi wao kule Mwanza anasema eti kesi ngumu kisa Mwanajeshi na migambo walitesa na kuua.

Je, Mgambo au mwanajeshi ana kinga ya kuua?
Kwa ujumla LHRC ni ajili ya propaganda tu.
 
We ulishawahi kujiuliza ni kwanini nafasi Scholarship za kusoma nchi za ulaya zinakuwa ni kwa sector ya uongozi tu....

Yaani hata hivi Leo ukisema unataka ukasome masters ulaya based on Leadership coarse utapata scholarship za kutosha plus meals, accommodations n.k
Ila sasa sema unataka ukajifunze ujasiriamali uone kama kuna mtu atakupa support...

Wazungu ni watu wa kulinda maslahi yao, Siku zote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom